Mtatangaza sana idadi ya wagonjwa wapya. Wakazi wengi sana wa miji mikubwa kama Dar es salam, Arusha na Moshi, Mwanza, Morogoro, Dodoma na visiwani Zanzibar wataku wamesha ambukizwa tayari. Na kwa hali hiyo hakuna kitu ambacho serikali inaweza ikafanya kuzuia watanzania wasiendelee kuambikizana.
Haya yote tungekuwa tayari tumesha yaepuka kama toka awali tahadhari kubwa zingekuwa zimesha chukuliwa. Ubishi wetu na kujifanya kujua kwetu ndiyo umetufanya tufike hapa tulipo.
Sasa hivi sio mda wa kulaumiana tena ni muda ambao unatakiwa tukae pamoja na kushauriana nini cha kufanya. Na naomba viongozi wetu wasiwe watu wa kuhubiri tu mambo ya kiroho, hapana hapa sasa inatakiwa science na utawala uchukue mkondo wake wa kutekeleza majukumu kwa kushirikiana na wataala na kuona jinsi gani Logistic ina work.
Haya mambo ya kuhubiri hubiri tu kuwa watanzania wachukie tahadhari kwa kuosha mikono yao kwa maji yanayo tiririka na sabuni na kuzingatia umbali hiyo peke yake haita work. Inatakiwa ijulikane pia kuwa maambukizi ya Virusi vya Corona sio tu pale mtu anapo kohoa au kupiga chafaya na kushikana mikono na mtu mwingine ndiyo yanatokea bali hata kuongea. Tunapo ongea kuna vitone vidogo vidogo vya mate tuna vitoa na kuvirusha hewani ambavyo vina contain hivi vijidudu, vikimfikia mtu tayari maambukizi yanatokea. Hiyo ni science.
Kinachotakiwa hivi sasa ni serikali kufunga haraka sana mipaka kati ya mikoa na mikoa na wilaya kwa wilaya kwa kuweka vizuizi kwenye njia zote watu wanazitumia kuingia au kutoka kwenye mikoa au wilaya hizo na kuhakikisha watu wote wanao pita kwenye hivyo vizuizi lazima wawe ni watu ambao wamesha pimwa ili kupunguza kuenea kwa huu ugonjwa kwa kasi hadi vijijini. Ugonjwa ukitapakaa vijijini itabaki kuokota mizoga tu.
Serikali inatakiwa kwenye mipaka yote ya kuingia mikoani na wailayani iweke testing instrumentes na sio kupima joto tu.
Tumesha ona vifaa vya kupima jota pekee yake havisaidii kitu, kwani kuna watu wana vijidudu vya COVID-19 lakini hawaonyeshi dalili zozote zile. Watu kama hawa watakuwa wengi sana Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Na Rais anatakiwa Arudi Ikulu ya Chamwino au Magogoni na sio kujichimbia huko Chato wakati wananchi wanateketea. Chato sio Ikulu. Yeye ndiye aliye sababisha haya yote kwa kutopokea ushauri wa watu wengi walio toa ushauri hasa wanadiaspora ambao walilamika sana kujiwa kwa mkupuo wa wachina kule KIA.
Hivyo asilikimbie hili janga. Hili janga ni letu sisi sote na yeye kama kiongozi anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuzungumza na wananchi moja kwa moja na sio kuwaachia Waziri mkuu na Mawaziri wa Afya wa Zanzibar na Bara peke yao. Nchi nyingine zote zinafanya hivyo.
Sent using
Jamii Forums mobile app