COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

Kuepuka hili gonjwa mbona simpo tu

1.Vaa mask muda wote. Hapa najua kuna wataoanza visingizio na kuhoji bei ya hizo mask ni shilingi ngapi na wangap watamudu kununua, nami nawajibu kabisa hamna anaeweza kuununua uhai.

2.Epuka misongamano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtatangaza sana idadi ya wagonjwa wapya. Wakazi wengi sana wa miji mikubwa kama Dar es salam, Arusha na Moshi, Mwanza, Morogoro, Dodoma na visiwani Zanzibar wataku wamesha ambukizwa tayari. Na kwa hali hiyo hakuna kitu ambacho serikali inaweza ikafanya kuzuia watanzania wasiendelee kuambikizana.

Haya yote tungekuwa tayari tumesha yaepuka kama toka awali tahadhari kubwa zingekuwa zimesha chukuliwa. Ubishi wetu na kujifanya kujua kwetu ndiyo umetufanya tufike hapa tulipo.

Sasa hivi sio mda wa kulaumiana tena ni muda ambao unatakiwa tukae pamoja na kushauriana nini cha kufanya. Na naomba viongozi wetu wasiwe watu wa kuhubiri tu mambo ya kiroho, hapana hapa sasa inatakiwa science na utawala uchukue mkondo wake wa kutekeleza majukumu kwa kushirikiana na wataala na kuona jinsi gani Logistic ina work.

Haya mambo ya kuhubiri hubiri tu kuwa watanzania wachukie tahadhari kwa kuosha mikono yao kwa maji yanayo tiririka na sabuni na kuzingatia umbali hiyo peke yake haita work. Inatakiwa ijulikane pia kuwa maambukizi ya Virusi vya Corona sio tu pale mtu anapo kohoa au kupiga chafaya na kushikana mikono na mtu mwingine ndiyo yanatokea bali hata kuongea. Tunapo ongea kuna vitone vidogo vidogo vya mate tuna vitoa na kuvirusha hewani ambavyo vina contain hivi vijidudu, vikimfikia mtu tayari maambukizi yanatokea. Hiyo ni science.

Kinachotakiwa hivi sasa ni serikali kufunga haraka sana mipaka kati ya mikoa na mikoa na wilaya kwa wilaya kwa kuweka vizuizi kwenye njia zote watu wanazitumia kuingia au kutoka kwenye mikoa au wilaya hizo na kuhakikisha watu wote wanao pita kwenye hivyo vizuizi lazima wawe ni watu ambao wamesha pimwa ili kupunguza kuenea kwa huu ugonjwa kwa kasi hadi vijijini. Ugonjwa ukitapakaa vijijini itabaki kuokota mizoga tu.


Serikali inatakiwa kwenye mipaka yote ya kuingia mikoani na wailayani iweke testing instrumentes na sio kupima joto tu.

Tumesha ona vifaa vya kupima jota pekee yake havisaidii kitu, kwani kuna watu wana vijidudu vya COVID-19 lakini hawaonyeshi dalili zozote zile. Watu kama hawa watakuwa wengi sana Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Na Rais anatakiwa Arudi Ikulu ya Chamwino au Magogoni na sio kujichimbia huko Chato wakati wananchi wanateketea. Chato sio Ikulu. Yeye ndiye aliye sababisha haya yote kwa kutopokea ushauri wa watu wengi walio toa ushauri hasa wanadiaspora ambao walilamika sana kujiwa kwa mkupuo wa wachina kule KIA.

Hivyo asilikimbie hili janga. Hili janga ni letu sisi sote na yeye kama kiongozi anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuzungumza na wananchi moja kwa moja na sio kuwaachia Waziri mkuu na Mawaziri wa Afya wa Zanzibar na Bara peke yao. Nchi nyingine zote zinafanya hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo Shule

Hilo tatizo la shule si mimi peke yangu, ni shida dunia ya tatu nzima huku Sub Saharan Africa.

Bado tunaamini we can pray the virus away.

Saint Peters Basilica at the Vatican was closed for Easter Sunday. So was the Liverpool Metropolitan Cathedral of Christ the King, a world's foremost monument of organized Christianity.

Masjid al-Nabawi, the Prophet's mosque in Medina, is closed by the pandemic as well as the Grand Mosque al-Haram in Mecca, another transcendent shrine among world's muslims.

Unfortunately in Africa our heads are still in the sand, religion is open for business. Our president proclaimed that we shouldn't stop going to church because that's where healing is. A blunder and danger on par with biblical cataclysms.
 
Taso,
Ebu angalia kama hii ya huko Marekani, naona ndio kinachotokea hapa kwetu
{942520E1-76EB-4DD9-B9C8-70AD1C436FA8}.png.jpg

Why does the USA have more reported coronavirus cases than China, if the population is way smaller and the healthcare system is better?
 
tunatia mchezo na hili janga....tunakwenda kupukutika......count down ni siku 21 kuanzia leo ili tufikie kilele cha maambukizi.
 
Nasikia huu mlipuko wengi ni wale ambao walikuwa kwenye ile shughuli ya TIBISII ambayo ilichukua mwongoza kipindi, na hivi vya sasa wengi ni manesi na madaktari!
 
kuna jamaa mmoja alituambia tusitangaze.....maana ni kama tunashindana shindana hivi kuhusu idadi ya wagonjwa, maambukizi na vifo....
 
wakuu nasikia ka kifua kinabana bana ivi.......duh
 

Hapa hauwezi laumu yeyote hapo marekani, hayo mambo ya kuwaambia watu wasitoke nje sio marahisi kwao kama ilivyo china sababu ya tofauti kubwa sana kati yao katika mifumo ya uendeshaji serikali na utaratibu wa maisha yao.

CHINA
Hata kabla ya janga hili wamekuwa wakiishi chini ya maelekezo na usimamizi wa mkono wa chuma wa watawala wao ambao hawana tofauti na madictator.

MAREKANI
Trump hana mamlaka ya kuwaambia watu wa newyork wakae ndani, ama wasitoke nje ya newyork achilia hiyo, hao ma newyorker wenyewe hawategemei kitu cha namna hiyo sababu ya mifumo ya haki za raia nk.

huko nadhani hata ukimzuia mbwa wa jirani asiingie eneo lako kwa kumkaripia unaweza ukapata tabu sana.
 
Roving Journalist,
Ombi kwa Admin wa Jamii forum unaweza tutengenezea graph toka siku zilipoanza kutolewa taarifa tuone jinsi graph yetu inavyokwenda na kama tunaweza predict peak yetu kama nchi na kama Dar itafikia lini?
 
Om

Ombi kwa Admin wa Jamii forum unaweza tutengenezea graph toka siku zilipoanza kutolewa taarifa tuone jinsi graph yetu inavyokwenda na kama tunaweza predict peak yetu kama nchi na kama Dar itafikia lini?
Kucheza na takwimu kama hizi ni kutafuta ubaya na serikali 😳
 
Kingston lodge pale Kimara Baruti wamefunga siku kadhaaa

Usiniulize zaidi kama ulipitia kupewahuduma jipeleke tu
 
Back
Top Bottom