#COVID19 COVID19: Watanzania tusipuuzie Corona; si lazima tutangaziwe vifo na maambukizi kila siku ili kujilinda

#COVID19 COVID19: Watanzania tusipuuzie Corona; si lazima tutangaziwe vifo na maambukizi kila siku ili kujilinda

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Baadhi ya wananchi wamelalamikia suala la watu mitaani kupuuzia ugonjwa wa #COVID19 na kuacha kuchukua tahadhari muhimu zinazoelekezwa kila siku na Wataalam wa Afya duniani

Inaelezwa kuwa wanunuzi maeneo ya masoko hawachukui tahadhari ikiwa ni pamoja na kunawa mikono hadi ugombane nao. Wengine wakipewa elimu wanasema kuna dawa tayari kutoka Madagascar na wengine wanadai wanajifukiza

Kwa mujibu wao, kupuuzwa kwa ugonjwa huu ni kutokana na kutotolewa kwa takwimu mpya hivyo watu wanadhani ugonjwa umeisha Tanzania na kuendelea na maisha kama kawaida

Wiki iliyopita, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisisitiza kuwa #COVID19 bado ipo na inaua na kuwa takwimu mpya zitatolewa baada ya ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kukamilika kufuatia Rais Magufuli kutilia shaka upimaji katika Maabara baada ya sampuli zinazodaiwa kuwa za matunda, wan

Soma Kutoka Chato: Rais Magufuli amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria - JamiiForums

Waziri Ummy: Serikali haitoi taarifa za COVID-19 kutokana na zoezi la uhakiki wa maabara ya Taifa - JamiiForums

ANGALIZO

Wananchi tuendelee kuchukua tahadhari, nawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka, vaa barakoa unapotoka ndani, kaa umbali wa mita 2 na mwenzako na toka ndani pale inapokulazimu. Kuushinda ugonjwa huu inahitaji ushirikiano wetu sote

#JamiiForums #JamiiTalks #COVID19TZ #JFCOVID19_Updates #JFCOVID19
 
mi sioni makali ya corona maana kama mpaka sasa duniani kote hatujafa hata laki 5 hv sasa hii ndio mnaita janga la dunia ?

yaani tasmini yangu nilijua ndani ya mwezi mmoja hapa kwetu tuko zaidi ya milioni 60 kwa haraka haraka mpaka sasa nilijua tungekua tumeshaondoka hata milioni 10 hivi ila mpaka sasa mimi katika ndugu,jamaa na marafiki naowajua hakuna hata mmoja mwenye ana corona au amekufa kwa corona.

sasa yowe za nini ?
 
Kiukweli corona inabebwa sana haihitaji promo inayopewa na media kabisa yani kuna magonjwa yanaua sana na hatuulizii taarifa ya idadi ya vifo kwanini corona tu yani mi sioni hata sababu ya kutangaza hizo cases ni kama tunauzidishia umaarufu hivi
 
Maralia akuuu wakati ndo inaua kuliko hiyo Corona
 
Takwimu zinasaidia kupanga mipango bora ya afya, zinasaidia kuchochea au kulegeza umuhimu wa tafiti zitakazoleta kinga na tiba.

Jiulizeni kwanini tunafahamu kuwa Tanzani kuna watu milioni 55?
 
Takwimu zinasaidia kupanga mipango bora ya afya, zinasaidia kuchochea au kulegeza umuhimu wa tafiti zitakazoleta kinga na tiba.

Jiulizeni kwanini tunafahamu kuwa Tanzani kuna watu milioni 55?
Waweke na kutangaza kila siku takwimu za maralia na mgonjwa mengine sugu kwa tz
 
Takwimu zinasaidia kupanga mipango bora ya afya, zinasaidia kuchochea au kulegeza umuhimu wa tafiti zitakazoleta kinga na tiba.

Jiulizeni kwanini tunafahamu kuwa Tanzani kuna watu milioni 55?
Dah...Kwani April kulikuwa na vifo vingapi vya saratani? Malaria? Utapiamlo? Ajali? Mbona havitangazwi?...au hatuhitaji kuvijua ili tujilinde navyo?...Au vifo vya corona ndiyo muhimu zaidi? [emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Kw
Kwanini hazitangazwi kilasiku ya mungu?unafahamu kuwa watoto wengi Sana hufa kwa maralia kilasiku kuliko Corona?kwanini Maralia haipewi promotion kubwa kiasi hiki wakati ndo inatuangamiza Sana? Au kwasababu tayari dili la kusambaza dawa na vifaa tayari mabeberu wamesha lilamba
Corona ni gonjwa jipya na bado linafanyiwa utafiti. Takwimu zinawasaidia wataalamu katika utafiti huo.
 
Sioni uhusiano wa kutangaziwa vifo na kujilinda ili hali ushajua ugonjwa upo. Kwani unahitaji kujua takwimu za maleria ili ushushe neti? Au unahitaji kujua idadi ya kina mama wanaokufa wakijifungua ili ujishauri ubebe mimba au laa? Au takwimu za wenye kisukari na presha ili uchukue hatua?
 
mi sioni makali ya corona maana kama mpaka sasa duniani kote hatujafa hata laki 5 hv sasa hii ndio mnaita janga la dunia ?

yaani tasmini yangu nilijua ndani ya mwezi mmoja hapa kwetu tuko zaidi ya milioni 60 kwa haraka haraka mpaka sasa nilijua tungekua tumeshaondoka hata milioni 10 hivi ila mpaka sasa mimi katika ndugu,jamaa na marafiki naowajua hakuna hata mmoja mwenye ana corona au amekufa kwa corona.

sasa yowe za nini ?
ila kamdudu [emoji23]

Mkulima wa mahindi
 
Kiukweli corona inabebwa sana haihitaji promo inayopewa na media kabisa yani kuna magonjwa yanaua sana na hatuulizii taarifa ya idadi ya vifo kwanini corona tu yani mi sioni hata sababu ya kutangaza hizo cases ni kama tunauzidishia umaarufu hivi
Vichwa vya watanzania kama vyote vimeharibika vile; hivi kweli mtu unatilia shaka umuhimu wa takwimu; eeeh Mungu tuondolee huyu Kofuli maana amefanya hii nchi kuwa ya mambumbu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom