Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kamishna wa Intelijensia ya Jinai kutoka Makao Makuu ya Polisi, CP Charles Mkumbo, amesema jeshi hilo lipo tayari kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya kulinda raia na mali zao na kuzuia vitendo vyote vya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha 20 cha maafisa habari wa Serikali kilichofanyika Zanzibar Aprili 3-6, 2025, CP Mkumbo amesema "tayari tuko timamu hata kama uchaguzi ungekuwa keshokutwa tayari tupo timamu kuhakikisha kwamba tunausimamia vyema ili uweze kuendeshwa kwa utaratibu ambao umepangwa na tume ya uchaguzi"
CP Mkumbo ameongeza kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi jeshi hilo litahakikisha usalama kwa watu wote ikiwemo waandishi wa habari wakati wanatekeleza majukumu yao.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha amesisitiza uzalendo katika kipindi chote cha uchaguzi kwani uzalendo ukiwepo basi usalama utaweza kuwa mkubwa kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa letu.
CP Mkumbo ametoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka ya haki pamoja na kutambua wajibu wa kila mmoja katika kutekeleza majukumu yao na kulinda amani ya taifa kwa pamoja.