PreGE2025 CP Mkumbo: Jeshi la Polisi lipo tayari kikamilifu kulinda amani kwenye Uchaguzi 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kamishna wa Intelijensia ya Jinai kutoka Makao Makuu ya Polisi, CP Charles Mkumbo, amesema jeshi hilo lipo tayari kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya kulinda raia na mali zao na kuzuia vitendo vyote vya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha 20 cha maafisa habari wa Serikali kilichofanyika Zanzibar Aprili 3-6, 2025, CP Mkumbo amesema "tayari tuko timamu hata kama uchaguzi ungekuwa keshokutwa tayari tupo timamu kuhakikisha kwamba tunausimamia vyema ili uweze kuendeshwa kwa utaratibu ambao umepangwa na tume ya uchaguzi"

CP Mkumbo ameongeza kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi jeshi hilo litahakikisha usalama kwa watu wote ikiwemo waandishi wa habari wakati wanatekeleza majukumu yao.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha amesisitiza uzalendo katika kipindi chote cha uchaguzi kwani uzalendo ukiwepo basi usalama utaweza kuwa mkubwa kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa letu.

CP Mkumbo ametoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka ya haki pamoja na kutambua wajibu wa kila mmoja katika kutekeleza majukumu yao na kulinda amani ya taifa kwa pamoja.

Ni Wajibu wangu kikatiba kupiga kura.

Nategema pia polisi kunilinda siku naenda kupiga kura.

Nategemea hawa polisi wanilinde kutokana na vurugu na vurumai ambazo CHADEMA wataenda kuzifanya na hatimae kuninyima haki yangu ya kupiga kura.

CHADEMA isiruhusiwe kuvunja sheria za nchi na uchaguzi kuninyima haki yangu ya msingi.
 
Je ni Wajibu wako kuangalia Kura zikiibiwa na Tume FEKI na Mapolisi wanaofanya Siasa?!

Je Jeshi la Polisi lilianzishwa kwa ajili ya kuiba Kura?! hebu wasikilizeni hapa Mapolisi wa CCM.

Ndio maana kuna uchaguzi. Uchaguzi unanipeleka kumpigia kura mwakilishi wangu ambae wajibu wake ni kuangalia kama kura zimeibiwa n.k Ndivyo katiba inavyosema.
Je Jeshi la Polisi lilianzishwa kwa ajili ya kuiba Kura?! hebu wasikilizeni hapa Mapolisi wa CCM.
Unatambua kabisa, polisi ilianzishwa na Wazungu kulinda wenye nazo. Mimi kama muafrika nimerithi na naambiwa 'it is part of democracy' and social cohesion😂😂😂😂😜

Sasa niikatae demokrasia?

Unatambua kabisa, polisi ilianzishwa na Wazungu kulinda wenye nazo. Mimi kama muafrika nimerithi na naambiwa 'it is part of democracy' and social cohesion
Polisi wa Sultani wa Kiarabu huko Zanzibar pia walitimuliwa na People's Power hapa Bara tuko milioni 60.
 
imhotep 👇🏿🔥🐼🐒

jamiiforums1556955921_540x378-jpg.2639634

...kama itakupendeza basi
Polisi wa Sultani wa Kiarabu huko Zanzibar pia walitimuliwa na People's Power hapa Bara tuko milioni 60.
Peoples power ama Okello bana. Hebu mpeni maua yake loh.

Sasa unasema tunatawaliwa Kifalme.

Turudi kwenye mada tu mkuu, huko kwa wafalame ni vichakani.
 
Kamishna wa Intelijensia ya Jinai kutoka Makao Makuu ya Polisi, CP Charles Mkumbo, amesema jeshi hilo lipo tayari kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya kulinda raia na mali zao na kuzuia vitendo vyote vya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha 20 cha maafisa habari wa Serikali kilichofanyika Zanzibar Aprili 3-6, 2025, CP Mkumbo amesema "tayari tuko timamu hata kama uchaguzi ungekuwa keshokutwa tayari tupo timamu kuhakikisha kwamba tunausimamia vyema ili uweze kuendeshwa kwa utaratibu ambao umepangwa na tume ya uchaguzi"

CP Mkumbo ameongeza kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi jeshi hilo litahakikisha usalama kwa watu wote ikiwemo waandishi wa habari wakati wanatekeleza majukumu yao.

Aidha amesisitiza uzalendo katika kipindi chote cha uchaguzi kwani uzalendo ukiwepo basi usalama utaweza kuwa mkubwa kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa letu.

CP Mkumbo ametoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka ya haki pamoja na kutambua wajibu wa kila mmoja katika kutekeleza majukumu yao na kulinda amani ya taifa kwa pamoja.

View attachment 3297173
Je na chama dola kikifanya njama za kuiba kura nao mtawachukulia hatua za kisheria?
 
Uchaguzi wa kiini macho, unaenda kupiga kura kumbe tayari Wana jina la mshindi
 
Polisi kwenye uchaguzi uliopita tuliona wakijaza kura feki kwenye maboksi ya kura, tuliona OCD mmoja akimwambia Mbowe hushindi kwa vyovyote huku wakifanya kila hila kuzuia mikutano na mawakala wa vyama vya upinzani
Huyu njagu hazungumzii hayo.
 
Kwa namna nyingine ya kusema ni kuwa wako tayari, kulinda fisiem katika uchaguzi. Ni mpuuzi pekee atakayeamini hilo alisemalo. Kila mtu anajua uchaguzi wa Tz unavyokuwa, ni aibu.
 
Kamishna wa Intelijensia ya Jinai kutoka Makao Makuu ya Polisi na wenzake ni watumishi wa umma ila ni jambo la ajabu sana kuona wakiwa wanafuata maagizo ya watu wachache.

Mamlaka ambayo amepewa yapo chini ya katiba na wala sio neno la Waziri ama Rais! Yeye ni mtumishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo.

Jambo la uchaguzi sio uhaini wala msiba kiasi kwamba utangazie umma kama tunajiandaa na vita! Uchaguzi ni jambo la heri kwa kila mwananchi ila kwa hali iliyopo sasa inaonesha kuwa Kamishna wa Intelijensia ya Jinai kutoka Makao Makuu ya Polisi pamoja na wenzake wanapokea maelekezo kutoka kwa viongozi wa CCM ilihali mamlaka mliopewa ni kutoka kwa umma ama watanzania.
 
Amani hailindwi na mtutu wa bunduki aache kiherehere.

Back
Top Bottom