Habari za wakati huu jamiiforums
C.P.A ya viwango vya kimataifa (A.C.C.A) kuanza kufundishwa katika Chuo cha Uhasibu Arusha (I.A.A)
View attachment 1755447
Soma>>>
Wahasibu, kwanini yanayofundishwa mitihani ya CPA yasiingizwe kwenye mitaala ya vyuoni?
View attachment 1755435
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), amemuagiza Mhasibu Mkuu wa Serikali pamoja na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kuwasimamia ipasavyo wataalamu wa kada ya uhasibu nchini ili kukomesha kasoro za kiuhasibu na upotevu wa fedha za umma unaobainishwa kila mara na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Mhandisi Masauni alitoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa utiaji Saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Bodi ya Uhasibu ya Kimataifa (ACCA) kwa ajili ya kuanzisha mafunzo ya uhasibu wa ngazi ya kimataifa ACCA katika vituo vya chuo hicho kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Dodoma.
View attachment 1755438
Aidha, Mhe. Mhandisi Masauni alikipongeza chuo hicho kwa kupewa ithibati ya kuwa Kituo cha Mafunzo ya Uhasibu wa Kimataifa na kuratibu mitihani ya Taasisi ya ACCA itayowezesha chuo hicho kuratibu mafunzo hayo nchini.
“Ni furaha yetu kuona sasa tutaweza kuzalisha wataalamu wengi zaidi wa uhasibu wa kimataifa kupitia Chuo chetu cha Uhasibu Arusha, pia chuo kitaweza kuongeza wigo wa kuanza kudahili wanafunzi kutoka nchi jirani”, alisema Mhandisi Masauni.
Alisema kuwa mpango huo utaongeza idadi ya wataalamu wenye sifa ya uhasibu wa kimataifa na itaokoa fedha nyingi zilizokuwa zinatumika kuwasomesha wataalamu nje ya nchi. Mhe. Mhandisi Masauni aliongeza kuwa ni vizuri kuwajengea wataalamu uwezo wa kushindana kimataifa lakini pia kwenda sambamba na viwango vya kimataifa ambavyo hubadilika mara kwa mara kulingana na sayansi na teknolojia.
View attachment 1755437
Naye Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Francis Mwakapalila alisema kuwa kuanzishwa kwa kituo cha mafunzo na udahili wa mitihani ya ACCA (CPA kwa kiwango cha Kimataifa) kutaongeza wigo wa wataalamu nchini na hivyo kuboresha uandaaji wa taarifa za uhasibu.
Habari zenu jamiiforums Nilihitimu elimu ya juu katika Chuo cha Uhasibu Arusha (I.A.A) mwaka 2009. Is this purely coincidental? ========== Soma>>> Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Tenga? Tunakwama wapi kama taifa...
USISAHAU:
ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.