CPA ya viwango vya kimataifa (ACCA) kuanza kufundishwa katika Chuo cha Uhasibu Arusha (I.A.A)

CPA ya viwango vya kimataifa (ACCA) kuanza kufundishwa katika Chuo cha Uhasibu Arusha (I.A.A)

Another one, mkuu utakua upo hiyo kamati ya ushauri na implementation hapo chuo si bure🤔👏
Hapana mkuu. Mimi ni Taxi Driver bado ninapambana na maisha. Fungua link usome uzi wangu hapa chini;
=====
 
Naona chuo kinapigwa msasa.

1.Kuidhinishwa na acca

2.Kuungana na chuo cha jeshi Monduli kutoa kozi za diploma ya stratedy, na degree ya bachelor of millitary science ambapo jana mahafali ya kwanza ya degree yalifanyika dodoma.

3.Kuingia mkatab ana tff kuanzisha kozi za michezo

4.Kupanuka kwa chuo, saizi chuo kipo hadi USA kule kwenye hotel kali ya ngurdoto, watoto wanakula maisha kule aisee, hostel kama hekalu. pia kina matawi babati na dar

5.Kuanzishwa kwa kozi ya kisasa katika uhasibu "Bachelor in accounting and IT"..,.hii kozi imekaa poa

N.k
 
Safi 👌 na hongera Infantry Soldier, inazidi kudhihirisha namna gani mawazo yako yamekuwa bora na kiungo muhimu baina ya jamii, taasisi pamoja na serikali.

Pia ni wazi JamiiForums ni kiunganishi muhimu baina ya wabunifu na wenye maono kwenda kwa watekelezaji. Tuzidi kuchangia yaliyokuwa mema na kuendeleza jitihada za kujikomboa kama vijana na taifa, amini mazuri yaja.
 
Safi 👌 na hongera Infantry Soldier, inazidi kudhihirisha namna gani mawazo yako yamekuwa bora na kiungo muhimu baina ya jamii, taasisi pamoja na serikali.

Pia ni wazi JamiiForums ni kiunganishi muhimu baina ya wabunifu na wenye maono kwenda kwa watekelezaji. Tuzidi kuchangia yaliyokuwa mema na kuendeleza jitihada za kujikomboa kama vijana na taifa, amini mazuri yaja.
Hakika JF ni kisima cha maarifa
 
Naona chuo kinapigwa msasa.

1.Kuidhinishwa na acca

2.Kuungana na chuo cha jeshi Monduli kutoa kozi za diploma ya stratedy, na degree ya bachelor of millitary science ambapo jana mahafali ya kwanza ya degree yalifanyika dodoma.

3.Kuingia mkatab ana tff kuanzisha kozi za michezo

4.Kuoanuka kwa chuo, saizi chuo kipo hadi USA kule kwenye hotel kali ya ngurdoto, watoro wanakula maisha kule aisee, hostel kama hekalu.

5.Kuanzishwa kwa kozi ya Bachelor ina accounting and IT..,.hii kozi imekaa poa

N.k
IAA yenye muonekano mpya kabisa na wa kuvutia.
 
Habari za wakati huu jamiiforums

C.P.A ya viwango vya kimataifa (A.C.C.A) kuanza kufundishwa katika Chuo cha Uhasibu Arusha (I.A.A)

View attachment 1755447

Soma>>> Wahasibu, kwanini yanayofundishwa mitihani ya CPA yasiingizwe kwenye mitaala ya vyuoni?

View attachment 1755435

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), amemuagiza Mhasibu Mkuu wa Serikali pamoja na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kuwasimamia ipasavyo wataalamu wa kada ya uhasibu nchini ili kukomesha kasoro za kiuhasibu na upotevu wa fedha za umma unaobainishwa kila mara na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mhandisi Masauni alitoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa utiaji Saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA - Infantry Soldier alihitimu chuo hiki mwaka 2009) na Bodi ya Uhasibu ya Kimataifa (ACCA) kwa ajili ya kuanzisha mafunzo ya uhasibu wa ngazi ya kimataifa ACCA katika vituo vya chuo hicho kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Dodoma.

View attachment 1755438

Aidha, Mhe. Mhandisi Masauni alikipongeza chuo hicho kwa kupewa ithibati ya kuwa Kituo cha Mafunzo ya Uhasibu wa Kimataifa na kuratibu mitihani ya Taasisi ya ACCA itayowezesha chuo hicho kuratibu mafunzo hayo nchini.

“Ni furaha yetu kuona sasa tutaweza kuzalisha wataalamu wengi zaidi wa uhasibu wa kimataifa kupitia Chuo chetu cha Uhasibu Arusha, pia chuo kitaweza kuongeza wigo wa kuanza kudahili wanafunzi kutoka nchi jirani”, alisema Mhandisi Masauni.

Alisema kuwa mpango huo utaongeza idadi ya wataalamu wenye sifa ya uhasibu wa kimataifa na itaokoa fedha nyingi zilizokuwa zinatumika kuwasomesha wataalamu nje ya nchi. Mhe. Mhandisi Masauni aliongeza kuwa ni vizuri kuwajengea wataalamu uwezo wa kushindana kimataifa lakini pia kwenda sambamba na viwango vya kimataifa ambavyo hubadilika mara kwa mara kulingana na sayansi na teknolojia.

View attachment 1755437

Naye Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Francis Mwakapalila alisema kuwa kuanzishwa kwa kituo cha mafunzo na udahili wa mitihani ya ACCA (CPA kwa kiwango cha Kimataifa) kutaongeza wigo wa wataalamu nchini na hivyo kuboresha uandaaji wa taarifa za uhasibu.


USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hizi international certification ndio mpango mzima. The sky is the limit for smart and aggressive people. Fani nyingine waige hii kitu. Tusibweteke wenyewe wenyewe. hakuna mtu anajua haya ya ndani kwetu ila sisi wenyewe
 
Back
Top Bottom