CRDB kuna shida gani? Mnachelewesha sana kutoa mikopo

Umekidhi viwango vya mkopo utakao?
Kama ukiwaridhisha kila kipengele mkopo ni massaa 72

Wana tatizo, kama una mtu huko muulize atakwambia.

Kuna jamaa yangu alienda kukopa ni takribani mwezi mzima kakamilisha kila kitu ila hela hazitoki wanasema wana vikao vyao bado muafaka haujapatikana.

Jana jamaa yangu alienda kusitisha akabeba fomu zake Branch flani Mkoani Tanga, sasa anatafuta alternative way kukamilisha jambo lake.
 

Mikopo imesitishwa nchi nzima mkuu, usimlaumu huyo ni vile alikuwa hakwambii ukweli
 
Tawi gani hilo?
 
Acha uongo bhana, CRDB wana shida na loan officer mwenye akili timamu anasema tu kwa sasa nchi nzima mzigo hautoki we uko hapa unapiga uongo unless we ni junior officer huelewi lolote huko ndani
Walishatoa tangazo la kusitisha mikopo?
 
Walishatoa tangazo la kusitisha mikopo?

Hawajatoa ila ela hazitoki wanafanya mambo yao kimya kimya ila kiuhalisia mikopo hawatoi saiv.
Jamaa yangu kabisa wa kazini ambaye nilimsainia kama referee kaomba mkopo almost mwezi umepita hawajampa kaamua kufata fomu yake atafute akili nyingine tu.
 
Binafsi mwezi wa pili huu sasa bila bila sijui wanashida gani.
 
Nimekidhi vigezo. Nimejaza fomu zao likamilifu na wamezipokea.
Kama wewe mwajiriwa serikalini na bado unaona mapicha picha nenda kaongee na mkuu wako wa kazi kunaa jambo hapo mkuu wako kasema hufai kupewa mkopo hayo mambo hufanyika kimya kimya kati ya bank na mkuu wako eneo lako la kazi
 
Kama wewe mwajiriwa serikalini na bado unaona mapicha picha nenda kaongee na mkuu wako wa kazi kunaa jambo hapo mkuu wako kasema hufai kupewa mkopo hayo mambo hufanyika kimya kimya kati ya bank na mkuu wako eneo lako la kazi
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hata mimi hawa CRDB wamenishangaza sana.Nina wiki ya pili sasa tangu niwasilishe kwao fomu zangu za mkopo lakini mpaka muda huu hamna kitu. Mimi nilitegemea kuwa watakuwa fasta kutoa hela kama walivyo niambia wakati naenda kuchukua fomu za mkopo lakini wapi. Ikifika Jmosi ya wiki hii bila pesa kutoka walahi naenda kuchukua fomu zangu, sitaki ujinga mie!
 
Hawa jamaaa nilitaka kumnasa kibao kabenki officer kamoja mkoa wa kanda ya ziwa nimejaza fomu kutuma fedha nje kanajizungusha tuuu! Vijana mkipewa kazi benki mjue mashati yenu hayo na ac tunalipia sisi acheni upumbavu!
 
Mimi waliniambia nikisharudisha form ndani ya siku tatu napata mzigo.

Ikifika Ijumaa bila bila naenda Kufata form zangu
 
Acha uongo bhana, CRDB wana shida na loan officer mwenye akili timamu anasema tu kwa sasa nchi nzima mzigo hautoki we uko hapa unapiga uongo unless we ni junior officer huelewi lolote huko ndani
Kuna mtu kapata a week ago. Na baada ya mwajiri kupitisha makato alipata hela siku hiyo hiyo. Inategemea na branch tu.
 
Umekidhi viwango vya mkopo utakao?
Kama ukiwaridhisha kila kipengele mkopo ni massaa 72
Usitetee kitu usicho kijua Kama hajakidhi vigezo angekuja kulalamika hapa!?CRDB Wana shida,siyo Kama walivyokuwa wanaharibu image yao waliyoijenga kwa gharama.
 
Siyo Mlimani city tu hata Kibaha wako hivyohivyo, unaenda kwa upole wanakujibu maandazi, Mara system imecollapse, Mara subirini sikukuu ziishe, kweli bank kuweka mkopo uliopitia process zote unasubiria sikukuu ziishe!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…