Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
1. Kijitanua: kwa East Africa Equity nafikiri ni bank inayoongoza kwa kujitanua. ipo nchi zote za EAC na imeingia kwa nguvu kubwa DRC na inanyemelea kuingia Ethiopia. Hizi zetu zipozipo tu. Nilisikia CRDB wana tawi Burundi, bado lipo.
2. Ufasta wa huduma: Equity ukiwa na namba au kitambulisho cha NIDA unarudi nyumbani una account na ATM card. Picha wanakupiga wenyewe, kila hatua iko fasta. Ukitaka cheque book ni fasta na bei rahisi mno, wanakupigia simu ikitoka.
3. Wahudumu: Kwa kweli wahudumu wa hizi benki zetu wanauzembe sana. Utakuta benki inaproduct mpya lakini ukienda uliza wale watumishi unakuta hawaelewi na wanaanza kuulizanaulizana, sijui hawapewi semina? Ukiona wanatembea harakahara wanaliza viatu unaweza dhani ni watu waelewa. Pia, ni kama wahudumu/maafisa mikopo wa hizi benki zetu hufurahi sana mtu asipotimiza vigezo vya mkopo.
4. Kingine naona Equity wanashirikiana sana na na "mabeberu", Kwenye kujitanua kwa wanashirikiana sana na mashirika ya kifedha kutoka nje.
Ushauri wangu ni kuwa hizi benki zitafute consultants wawasaidie namna ya kujiendesha na kujitanua nje vitu vidogo kama kumpiga mteja picha badala ya kumwambia aje na passport vina impact kubwa sana, mambo yanabadilika.