CRDB na NMB zimelala sana ukifananisha na Equity Bank

CRDB na NMB zimelala sana ukifananisha na Equity Bank

Nilikuwa mteja wa crdb aiseee kupata card rahisi ila mambo ya kurenew na huduma za mtandaoni ni ovyo kabisa miamala mingi ya njee ilikuwa inakataa sio yote ....nikajaribu equity dahhh experience yake ni bab kubwa kwenye kila huduma big up kwao
That's nice. Hama kabisa mkuu. CRDB inabidi ipate mpinzani mkali zaidi ili ijifunze kuwa na ufanisi
 
Selcom imekufa baada ya serikali kuanzisha mfumo wa malipo wa Control number unaosimamiwa na serikali yenyewe. Mfano kama ni faini ya trafiki unapewa control number unaenda kulipa, charges mbalimbali unalipa sasa Selcom ya nini tena na kuna wale Maxmalipo nao kwisha habari yao
Mpaka tuheshimiane
 
Prof Luoga akili zake kamkabidhi Magufuli!!
Tatizo la maprofesa walioingia chuoni kupitia “Mature age “ ni hilo, hawana confidence. Ndio hao wakina Kabudi, Mwakyembe na huyo Luoga!!! Waliokotwa jalalani; they have totally surrendered themselves to Jiwe.
 
Mm nauliza; mtu anaweza akakutumia hela kwa wakala wa NMB kwenda kwenye account yako ta Equity? Au kutoka wakala wa AIRTEL MONEY kwenda Equity bank? Kama inawezekana, gharama zao zikoje?
 
Equity baba lao . Wako very professional Hakuna zile tabia za kiswahili unaenda bank unapata wafanyakazi wapo very slow na nyodo nyingi.

Unataka kufungua account Mara leta barua ya mtendaji, wao Ni chap kwa haraka. Hapo hapo Unafungua account yako NIDA inatosha
Wapo Morogoro?
 
NMB ni jipu nime renew line yangu ya bank tangu mwanzo wa mwezi mpaka sasa nikifatilia bado kadi haijaja na hapo ni mjini hivi kwanini hii bank haitaki kubadilika na kuendana na wakati, no wonder watanzania wengi hutumia simu zaidi ya hayo ma Visa kadi zao, too much uzembe
 
CRDB nao siku hizi wamekua hovyo kweli. Huduma zao zinasinzia balaa na taratibu lakini kwa uhakika nimeanza kuona baadhi ya watu wakihamia Equity bank
Mimi naenda kufungua account yangu equity Yani haiishi lisaa una kadi yako mkononi
 
1. Kijitanua: kwa East Africa Equity nafikiri ni bank inayoongoza kwa kujitanua. ipo nchi zote za EAC na imeingia kwa nguvu kubwa DRC na inanyemelea kuingia Ethiopia. Hizi zetu zipozipo tu. Nilisikia CRDB wana tawi Burundi, bado lipo.

2. Ufasta wa huduma: Equity ukiwa na namba au kitambulisho cha NIDA unarudi nyumbani una account na ATM card. Picha wanakupiga wenyewe, kila hatua iko fasta. Ukitaka cheque book ni fasta na bei rahisi mno, wanakupigia simu ikitoka.

3. Wahudumu: Kwa kweli wahudumu wa hizi benki zetu wanauzembe sana. Utakuta benki inaproduct mpya lakini ukienda uliza wale watumishi unakuta hawaelewi na wanaanza kuulizanaulizana, sijui hawapewi semina? Ukiona wanatembea harakahara wanaliza viatu unaweza dhani ni watu waelewa. Pia, ni kama wahudumu/maafisa mikopo wa hizi benki zetu hufurahi sana mtu asipotimiza vigezo vya mkopo.

4. Kingine naona Equity wanashirikiana sana na na "mabeberu", Kwenye kujitanua kwa wanashirikiana sana na mashirika ya kifedha kutoka nje.

Ushauri wangu ni kuwa hizi benki zitafute consultants wawasaidie namna ya kujiendesha na kujitanua nje vitu vidogo kama kumpiga mteja picha badala ya kumwambia aje na passport vina impact kubwa sana, mambo yanabadilika.
Equity inakaribia kufa, imekopesha watu na haitaki ku-vary madeni yao ili watu walipe
 
NMB ni jipu nime renew line yangu ya bank tangu mwanzo wa mwezi mpaka sasa nikifatilia bado kadi haijaja na hapo ni mjini hivi kwanini hii bank haitaki kubadilika na kuendana na wakati, no wonder watanzania wengi hutumia simu zaidi ya hayo ma Visa kadi zao, too much uzembe
Siku moja nilitaka kufanya malipo nje ya nchi. Ilikuwa weekend. Nikatumia NMB master kadi ikagoma, nauliza watu naambiwa mpaka uende ofisini kwao ndiyo wakuruhusu kutumia. Nikasema ngoja nitumie equity. Nikahamisha hela kwenda equity. Kutuma nako ikagoma. Kucheki salio halijafika wakati NMB nimekatwa.

Nikawapigia NMB wananiambia miamala ya benki na benki inachukua hadi siku tatu kukamilishwa. Nikatoa hela Mpesa na kuweka Equity ndipo nikafanikiwa. Baada ya siku tatu ndiyo ile pesa toka NMB inaingia account ya Equity.
Nilisikitika sana mwenendo wa benki zetu siku ile.
 
Kama kawaida namazoea ya kuagiza bidhaa kutoka China, nikawa natumia CRDB via paypal, bahati mbaya nilikosea Address ya kulipia, nikawasiliana na paypal kuhusu tatizo hilo nao wakarudisha pesa CRDB, sasa kimbembe kinanzia hapa nilipokwenda kuwaambia pesa imerudishwa na paypal waliniambia niwape VRN na kweli nikawapa sasa mara subiri mara njoo kesho ikawa Kama naomba kazi CRDB, nakumbuka imenichukua miezi 6 sikufanikiwa, nikapata wazo la kwenda equity bank nikafungua account ni link kadi mpya na paypal, ndipo nikawasiliana na paypal kwamba pesa iliyopo kwao waihamishie equity baada masaa 6 mzigo ukasoma equity bank
Equity bank[emoji3581]
Mbona kama unanivuruga? Hela ilisharudishwa CRDB sasa iweje tena hao paypal waipeleke Equity?
 
Hongera kwa huyo mdada mzuri mweupe kwa kuwahudumia vizuri, aendelee na moyo huo huo wa kuonesha wanawake tunaweza.

back to topic, umekuwa very narrow kwenye reply yako, Tatizo la CRDB na NMB si suala la wafanyakazi kwa ujumla wao wala si la mfanyakazi mmoja mmoja, matatizo yapo lukuki ndio yanayopelekea ziendelee kuitwa “Local banks” .
Mbona umewasahau na wenzao benk ya posta tpb
 
Napenda nyuzi kama hizi zinazolinganisha huduma katika taasisi/kampuni mbalimbali.

Kwa ufupi taasisi nyingi ambako serikali ina hisa nyingi au inamiliki jumla zinaendeshwa kwa ufanisi mdogo sana, hadi inakera. Haziko kiushindani. Bado zinaendeshwa kwa falsa na mitizamo ya 'Kijamaa' badala ya kufukiri jinsi ya kushindana kwenye 'Soko'.

Jaribu kulinganisha huduma za vituo vya petroli vya Puma na zile za Total. Au Airtel vs Vodacom; TTCL vs Vodacom/tiGo; Agakhan vs Muhimbili n.k. utagundua tofauti kubwa.

Wafanyakazi wanafanya wanavyotaka kwa sababu watalipwa anyways, na hakuna mifune imara ya kufuatilia utendaji wao. Kwa mfano, kama mfanyakazi wa mapokezi angelipwa kulingana na idadi ya wateja aliowapa huduma ni wazi angechakarika na foleni zingepungua.

Tuendelee kusema, labda siku moja wafanyakazi, na hasa vijana, wataelewa na kubadilika kimtizamo (attitude).
 
Siku moja nilitaka kufanya malipo nje ya nchi. Ilikuwa weekend. Nikatumia NMB master kadi ikagoma, nauliza watu naambiwa mpaka uende ofisini kwao ndiyo wakuruhusu kutumia. Nikasema ngoja nitumie equity. Nikahamisha hela kwenda equity. Kutuma nako ikagoma. Kucheki salio halijafika wakati NMB nimekatwa.

Nikawapigia NMB wananiambia miamala ya benki na benki inachukua hadi siku tatu kukamilishwa. Nikatoa hela Mpesa na kuweka Equity ndipo nikafanikiwa. Baada ya siku tatu ndiyo ile pesa toka NMB inaingia account ya Equity.
Nilisikitika sana mwenendo wa benki zetu siku ile.
Hizi bank zetu ubunifu zero kwanini kuamisha muamala ichukue siku tatu hyo si wastage of time, na time ni resource muhimu, kwanini nchi hii taasisi ni ngumu kubadilika kulingana na matwaka ya mda ka tu ku renew card mpya inachukua miezi sembuse hzo huduma nyingine. Very shame to our local banks.
 
Back
Top Bottom