CRDB na NMB zimelala sana ukifananisha na Equity Bank

Nilikuwa mteja wa crdb aiseee kupata card rahisi ila mambo ya kurenew na huduma za mtandaoni ni ovyo kabisa miamala mingi ya njee ilikuwa inakataa sio yote ....nikajaribu equity dahhh experience yake ni bab kubwa kwenye kila huduma big up kwao
That's nice. Hama kabisa mkuu. CRDB inabidi ipate mpinzani mkali zaidi ili ijifunze kuwa na ufanisi
 
Mpaka tuheshimiane
 
Prof Luoga akili zake kamkabidhi Magufuli!!
Tatizo la maprofesa walioingia chuoni kupitia “Mature age “ ni hilo, hawana confidence. Ndio hao wakina Kabudi, Mwakyembe na huyo Luoga!!! Waliokotwa jalalani; they have totally surrendered themselves to Jiwe.
 
Mm nauliza; mtu anaweza akakutumia hela kwa wakala wa NMB kwenda kwenye account yako ta Equity? Au kutoka wakala wa AIRTEL MONEY kwenda Equity bank? Kama inawezekana, gharama zao zikoje?
 
Wapo Morogoro?
 
NMB ni jipu nime renew line yangu ya bank tangu mwanzo wa mwezi mpaka sasa nikifatilia bado kadi haijaja na hapo ni mjini hivi kwanini hii bank haitaki kubadilika na kuendana na wakati, no wonder watanzania wengi hutumia simu zaidi ya hayo ma Visa kadi zao, too much uzembe
 
CRDB nao siku hizi wamekua hovyo kweli. Huduma zao zinasinzia balaa na taratibu lakini kwa uhakika nimeanza kuona baadhi ya watu wakihamia Equity bank
Mimi naenda kufungua account yangu equity Yani haiishi lisaa una kadi yako mkononi
 
Equity inakaribia kufa, imekopesha watu na haitaki ku-vary madeni yao ili watu walipe
 
Siku moja nilitaka kufanya malipo nje ya nchi. Ilikuwa weekend. Nikatumia NMB master kadi ikagoma, nauliza watu naambiwa mpaka uende ofisini kwao ndiyo wakuruhusu kutumia. Nikasema ngoja nitumie equity. Nikahamisha hela kwenda equity. Kutuma nako ikagoma. Kucheki salio halijafika wakati NMB nimekatwa.

Nikawapigia NMB wananiambia miamala ya benki na benki inachukua hadi siku tatu kukamilishwa. Nikatoa hela Mpesa na kuweka Equity ndipo nikafanikiwa. Baada ya siku tatu ndiyo ile pesa toka NMB inaingia account ya Equity.
Nilisikitika sana mwenendo wa benki zetu siku ile.
 
Mbona kama unanivuruga? Hela ilisharudishwa CRDB sasa iweje tena hao paypal waipeleke Equity?
 
Mbona umewasahau na wenzao benk ya posta tpb
 
Napenda nyuzi kama hizi zinazolinganisha huduma katika taasisi/kampuni mbalimbali.

Kwa ufupi taasisi nyingi ambako serikali ina hisa nyingi au inamiliki jumla zinaendeshwa kwa ufanisi mdogo sana, hadi inakera. Haziko kiushindani. Bado zinaendeshwa kwa falsa na mitizamo ya 'Kijamaa' badala ya kufukiri jinsi ya kushindana kwenye 'Soko'.

Jaribu kulinganisha huduma za vituo vya petroli vya Puma na zile za Total. Au Airtel vs Vodacom; TTCL vs Vodacom/tiGo; Agakhan vs Muhimbili n.k. utagundua tofauti kubwa.

Wafanyakazi wanafanya wanavyotaka kwa sababu watalipwa anyways, na hakuna mifune imara ya kufuatilia utendaji wao. Kwa mfano, kama mfanyakazi wa mapokezi angelipwa kulingana na idadi ya wateja aliowapa huduma ni wazi angechakarika na foleni zingepungua.

Tuendelee kusema, labda siku moja wafanyakazi, na hasa vijana, wataelewa na kubadilika kimtizamo (attitude).
 
Hizi bank zetu ubunifu zero kwanini kuamisha muamala ichukue siku tatu hyo si wastage of time, na time ni resource muhimu, kwanini nchi hii taasisi ni ngumu kubadilika kulingana na matwaka ya mda ka tu ku renew card mpya inachukua miezi sembuse hzo huduma nyingine. Very shame to our local banks.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…