CRDB VS NMB: Watani wa Jadi (Simba na Yanga) katika sekta ya Kibenki Tanzania

CRDB VS NMB: Watani wa Jadi (Simba na Yanga) katika sekta ya Kibenki Tanzania

Benki zetu nyingi hapa nchini swala la huduma kwa wateja bado sana. Unakuta benki/tawi lina madirisha saba lakini yanayotoa huduma ni mawili au matatu, hili tatizo ni kwa benki zote nchini.
 
Gawio kwa wanahisa ni kiasi gani? Mfano NMB hisa moja ni 4500. Unapata faida kiasi kwa hisa moja? CRDB ni 450, faida ni Tsh ngapi kwa hisa?
 
Mwaka jana gawio Crdb 45 Nmb 100
Hapana NMB ilizidi hapo ilikua 286.25
1690224129879.jpg
 
Ni ukweli usiopingika kwamba kwa sasa hizi Bank mbili ni wababe ktk sekta ya Biashara ya kibenki Tanzania na hii ni kutokana na ukubwa waliokua nao na pia kutopishana sana kwny baadhi ya takwimu zao muhimu kama zinavyojieleza hapa chini..[emoji116][emoji116][emoji116]

1.THAMANI YA MALI WANAZOMILIKI(ASSETS VALUE)
CRDB:-Tsh13.2 Trilion
NMB:-Tsh12.165 Trilion

2.AMANA ZA WATEJA(CUSTOMER DEPOSITS)
CRDB:- Tsh 8.9 Trillion
NMB:- Tsh 8.4 Trilion

3.SHAREHOLDERS VALUE
CRDB:- Tsh 1.8 Trilioni
NMB:- Tsh 2.25 Trilioni

4.FAIDA BAADA YA KODI
CRDB:- Tsh 424Bn
NMB:- Tsh 542Bn

5.BEI KWA HISA MOJA DSE
CRDB:- Tsh 460
NMB:- Tsh 4500

6.BRANCHES(MATAWI)
CRDB:- 243(2022)
NMB:- 226(2022)

7.WAFANYAKAZI
CRDB:- 3700+
NMB:- 3500+

8.KUANZISHWA
CRDB:- 1996
NMB:- 1997

9.FOLLOWERS INSTAGRAM
CRDB:- 275K
NMB:' 270K
Unaeza kuongezea chochote cha ushndani pia kuhusu hzi benki mbili kubwa nchini binafsi nawakubali sana NMB kwny kitengo cha HUDUMA KWA WATEJA[emoji91].

Nini kinakufurahisha na kipi kinakukera kutoka kwa hawa miamba wa sekta ya Bank na ni Bank ipi inayokuvutia zaidi ya hzo mbili hapa nchini...[emoji120]
Nina swali mkuu,
Mfano nimewekeza katika hisa
Crdb - 4.600.000/=
Nmb - 4.500.000/=
Je naweza kupata gawio sh ngapi kwa mwaka? Kama crdb walipata faida ya tsh 424bn na Nmb tshs 542bn?
 
Nina swali mkuu,
Mfano nimewekeza katika hisa
Crdb - 4.600.000/=
Nmb - 4.500.000/=
Je naweza kupata gawio sh ngapi kwa mwaka? Kama crdb walipata faida ya tsh 424bn na Nmb tshs 542bn?
Kwanza kabisa utoaji wa Gawio haujawahi kuwa constant unategemeana na faida kiasi gani kampuni imetengeneza katika mwaka wa fedha husika lakini pia inategemea na malengo ya kampuni katika mwaka wa fedha unaofuata kama kampuni ina mpango wa kujitanua zaidi(kuanzisha branch nyingi ktk mwaka unaofuata) basi kiasi kidogo sana kitatolewa gawio na kingine kitatumika km mtaji wa kujipanua zaidi..

Pili, Kiasi cha gawio utachopata inategemea pia na idadi ya hisa ulizonazo katika kampuni husika kuzidisha kwa bei ya gawio kwa hisa moja..
Kwa mfano wa kiasi uliotoa na kwa kiasi cha gawio kwa hzo kampuni kwa mwaka 2023 itakua hivi..[emoji116][emoji116]

1.CRDB
Ukiwekeza hyo 4.6m utakua na idadi ya hisa(4.6m÷460)= Hisa 10,000
Gawio= 10000*45= Tsh 450,000

2.NMB
Ukiwekeza hyo 4.5m utakua na Hisa 1000 za NMB
Gawio= 1000*286.25= Tsh 286,250
 
Back
Top Bottom