CRDB wakanusha bank statement iliyodaiwa kuwa ya Mbowe

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994

Taarifa kwa Umma

Kumekuwa na taarifa ya akaunti ya kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayosambaa mitandaoni ikionyesha miamala iliyofanywa kwenye akaunti yake ya benki.

Tunapenda kujulisha umma kuwa taarifa hiyo ya akaunti ambayo imeihusisha Benki yetu ya CRDB si ya kweli na kuendelea kuisambaza ni kosa la jinai.

Benki yetu imeshairipoti kwa vyombo husika vya dola ili uchunguzi wa kina ufanyike na hatua stahiki zichukuliwe dhidi wote wanaohusika na kitendo hiki.

Benki ya CRDB inapenda kuwakumbusha wateja wake na umma kuwa Benki inaendeshwa kwa misingi ya kanuni na sheria na siku zote taarifa za mteja zitabaki kuwa kati ya mteja na Benki.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano na Uhusiano
Benki ya CRDB
 
WanaCCM wamebakia kusambaza Fake News hahaa...
Kumbe hujui propaganda za CCM. Yaani hapo watakuwa walifanya kusudi ili kupima uwezo wa kuhimili propaganda kwa vijana wa CHADEMA!

Kule kukosewa kwa jina tu kusingewashughulisha Bavicha, badala yake wamejikuta wanaingia kwenye mtego!
Siasa inahitaji akili
 
Nani aliingia kwenye mtego ?
Wanaharakati wa chadema kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo hao crdb wamejitahidi sana kukanusha! kiuhalisia hakukuwa na sababu zozote za kukanusha kwasababu hata chadema nao wanaoongoza kwa propaganda zisizo za kweli. Utakuta picha ya miaka ya nyuma wanaitumia kuelezea tukio la sasa!
Hizo zote ni propaganda tu za kisiasa. Hazina tija
 
Wanapumulia mashine🀣
 
Kwa mfano hii ni picha ya mwaka gani ?

 
CRDB wasituone wote wajinga. Kama siyo bank statement ya kweli kwanini serikali ihusishwe na ufanyike uchunguzi?

Au niulize, uchunguzi wa nini? Kubainisha kuwa siyo ya ukweli?

Haiingii akilini.
CRDB wasituone wote wajinga. Kama siyo bank statement ya kweli kwanini serikali ihusishwe na ufanyike uchunguzi?

Au niulize, uchunguzi wa nini? Kubainisha kuwa siyo ya ukweli?

Haiingii akilini.
Yan we ajuza tatzo ubongo umeubana na hijabu thats why unafikiria mavi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…