CRYPTO-FUNZO KWA WAKURUPUKAJI: Luna coin ilikua ni sawa na $85 wiki ilopita lkn kwa sasa ni takataka(trash coin)

Naomba kuuliza swali wataalam wa ma cyrpto currency.
1. Kwenye hii biashara, bidhaa ni nini?
2. Risk Mitigation ikoje kwenye hii biashara?, since haiko regulated?
3. Kila mtu akiamua ku convert fedha zake back to USD, faida itatokea wapi kwa wale watakaopaswa kulipwa faida kwa bei ya kipindi hicho?
4. Kwa nini hii sio scam or pyramid scheme?
 
1. Bidhaa ni sarafu. Kama unavyonunua dollar kwa kutumia tsh basi ndivyo hvo mtu alinunua Luna coin kwa kutumia tsh.

2. Risk mitigation ni kwa wanaoifanya hii bizness kitaalam. Inshort ni buy low sell high au reverse kwa shortselling. So kabla ya kuamua kununua unaangalia kama sarafu mtandao(crypto) unayonunua ina potential ya kuongezeka value. Kucontrol risk ni ile namna unajipanga kwamba uiuze ikifika value ipi incase isipo ongezeka value, yaan ikashuka. Ni kama stop loss na take profit

3. Watu wakisell crypto zote ofcoz crypto zitakua worthless coz value zao zinaongozwa na sheria ya supply and demand. LAKINI hio haiwezekani mkuu, the only currency kwenye dark web ni hz crypto. So theoretically kuuzwa ni sawa ila practically ni ngumu. Kuna mda itatokea tu watu wengi(japo sio wote) wakaziuza na hio imetokea now coz crypto karibia zote zimeshuka thamani kiasi kikubwa lkn complete sell off ni ngumu kutokea.

4. kama umenielewa basi utaona crypto ni financial instrument kama vle stock. The earlier you buy, the lower quote you get. hapo ndo panakuchanganya ukadhani ni pyramid scheme. If crypto is scam then NYSE & NASDAQ nazo ni scam coz zinapokea IPOs za Crypto exchanges.
 
1. Bidhaa ni sarafu. Kama unavyonunua dollar kwa kutumia tsh basi ndivyo hvo mtu alinunua Luna coin kwa kutumia tsh.
I thought that way but naona ni unfair comparison kwa sababu USD iko backed up na US Central Bank while hizo zingine hazina guarantee. So I don't think ni fair comparison. Kama reasoning yangu ni sawa, then swali bado linasimama. Na kama siko sahihi, nasimama kukubali kurekebishwa!
Kama nimeelewa ni sort ya kamari, unabahatisha kwa kuangalia trend na vitu kama hivyo. Kama niko sahihi, tofauti yake na kucheza kamari kama betting ni ipi?

Naelewa kwamba hilo haliwezekani kutokea kwa pamoja, ila lengo ni kujua kama ni pyramid scheme ama la. Kwenye biashara product ndio inatunza thamani ya kitu. Mfano nikiwa na maembe watu wakawekeza, ikifikia kipindi cha kuwarudishia pesa zao tutahesabu maembe na kuwapa wakauze wajilipe au tutawapa maembe wakale na familia. Sasa kwa sababu CC zinanunuliwa kwa dollar, wakitakiwa kum refund kila mtu inawezekana au kuna watakaoondoka mikono mitupu kwa sababu hela zao wamelipwa wengine?

Hisa ni government sanctioned kind of scam. Sema yenyewe at least kuna kampuni unanunua hisa na zinaeleweka. Ila kuna kuumia kwingi huko pia!

Nashukuru kwa majibu yako, kuna vitu nimejifunza. Ila ukiweza ku comment on followup comments zangu nitashukuru!
 
Mkuu ukipata muda ingia hapa www.teachyourselfcrypto.com its free knowledge is power!
 
hii yote imesababishwa na mkorea Do Kwon alipewa tahadhali ya wazi kabisa kuwa mtu mwenye capital ya $1billion angeweza kuidepeg UST ila yeye akashupaza shingo yake ona sasa mpaka watu wamejinyonga kisa ukiburi wake
 
Sasa sijaona mahali ambapo mteja angegundua kama sarafu yake itashuka bei.
hebu tuambie hapo huwa wanasema? Au Kuna viashiria gani?
 
Unfortunately kwa sasa sina muda, umebana sana. Nitajifunza kwa wanaojua tu!
Programmer gani wewe wa ajabu unakua eti huna muda wa kujifunza!!

Yaani ndio kusema umesharidhika kabisaaa na hiyo level of knowledge ulionayo sasa!

Yaani ushaamua utakufa na Laravel, Flute, Django library pamoja na MongoDB! Vingine vipite kuleee!

Learning is a continuous process.
 
Ni programmer wa ajabu ajabu mie...!
 
Hata mie ninashangaa sana yaani,
 
Japo kuna vitu vinaitwa stable coins hzo ndo utakuta ziko backed up na assets kama vle gold au real dollar. Mfano kuna tether ambayo value yake inamatch na 1 dollar. So provider wa hio coin wako na dollar reserve plus dollar backed assets ili kuipa backup tether
 
Kweli kabisa Mkuu
Unategemea kukusanya RENEC ngapi hadi July? Kuna zawadi sasa hivi zinatolewa na Remitano kwa Watz mtu akijiunga kwa refferal code yako anapata USDT 4 na wewe unapata moja. Je ulishalisikia hilo?
 
Haya mambo ya pegging ndiyo bwana George Soros aliwafanya mbaya Uingereza na Pound yao. Haiwezekani na huku siku moja watu wakalazwa na viatu?
 
Unategemea kukusanya RENEC ngapi hadi July? Kuna zawadi sasa hivi zinatolewa na Remitano kwa Watz mtu akijiunga kwa refferal code yako anapata USDT 4 na wewe unapata moja. Je ulishalisikia hilo?
Aisee
 
Safi elimu nzur umewapatia.
Kwa wale watakao kuwa interest watembelee Link hii wajiunge wapate Fursa mbali mbali za Uwejezaj wa fedha zao ktk mfumo wa Digital Currency hakika watanikumbuka.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…