Huu mfano naujua. Sina uhakika kama practically unawezekana, lakini mantiki yake naielewa.
Lakini huu mfano hau-apply kwa Bitcoin yenyewe kama Crypto, bali unaweza ku-apply kwa "Crypto Banks" au "Crypto Exchanges". Hizi Crypto exchanges zinamilikiwa na kusimamiwa na watu, lakini crypto yenyewe kama Bitcoin hakuna anaeimiliki - kwa kiingereza tunasema ni de-centralized.
Hata huyu anaeitwa Satoshi Nakamoto yeye ni Mvumbuzi wa Bitcoin, lakini sio mmiliki wa Bitcoin wala hawezi "Kui-control" Bitcoin. Na sio Satoshi Nakamoto tu, bali hakuna mtu yeyote, wala serikali yoyote, wala taasisi inayoweza kumiliki na ku-control crypto.
Satoshi sio wa kwanza kuja na concept ya Crypto, bali yeye alisaidia kutatua changamoto ambayo watangulizi wake walishindwa kuitatua, ambayo hiyo ndio imefanikisha kulifanya wazo la Crypto liwe viable. Ni kweli, waleti yake ina 5% ya Bitcoin zote - ila hajawahi kuzitoa wala kufanya muamala wowote tangu mwaka 2009. Mara ya mwisho alituma ujumbe kuwa "Nimeingia kwenye mambo mengine" mwaka 2010, tangu hapo hajasikika tena na wala waleti yake haijawahi kufanya muamala wowote.
Kwahiyo, crypto hazina wamiliki na haiwezekani kuzimiliki, bali zina waanzilishi. Makampuni mengi yanayowatapeli watu yanatumia utapeli ule ule ambao unatumika kutapeli pesa za kawaida; mfano hii kampuni niliyoielezea kwenye uzi - Celsius, na nyingine inaitwa Quadriga CX, na nyingine inaitwa FTX.
BOTTOM LINE
Shida sio crypto, shida ni kampuni zinazofanya biashara ya kutunza, na kufanikisha miamala ya crypto.