zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
- Thread starter
- #81
1. Mkuu kwenye hiyo page nilioambatanisha tafsiri ya kiebrania kwa mawingu ni ANAN alafu upinde RESHIYT hivyo ndio nimetofautisha kwa kutumia maana hizi za kiebrania kwa hiyo upinde na mawingu ni vitu viwili tofauti ila vyote kwa pamoja vilitumika kama alama ya makubaliano baada ya gharika.Nisaidie kwa nini tunasema yako mawingu ya mvua na mawingu yasiyo ya mvua?
Na kwa nini hiyo solid state ya anga au mawingu isiwe ndio hiyo cannopy iliyo tajwa kiembrania?
Unatumia kigezo gani kuto tofautisha upinde wa mvua na mawingu?
Nini kinachokufanya ujihakikishie kuwa mvua na mawingu vilianza wakati wa gharika ya Nuhu? Kumbuka katika uumbaji Mungu alitenga maji na kupata ya angani na yaliyo katika nchi chini ya anga? Lakini tunambiwa pia kuwa Mungu alifanya ardhi ikawa na unyevu ikachipusha mimea. Huo unyevu ulitokana na maji ya angani au ya chini ya anga? Ndio tunarudi kule kule yako mambo ambayo Mungu kwa utashi wake hakutaka kutufunulia.
2. Mkuu hoja hapa sio mawingu ya mvua au yasiyo mawingu ya mvua ila hoja hapa ni kwanini waliyapa majina yenye maana tofauti kabisa ni sawa na mtu aseme simba na nyati ni wanyama wakali sana alafu mtu useme huyo ni mnyama mmoja.... Inaingia kweli?? IRON DOME haiwezi kuwa sawa na WINGU maana kwa waebrania hyo canopy wanaitambua kabisa hata ukisoma kitabu cha antiquites Book 1 verse 1 utakutana na story ya creation ya msomi myahudi Josephus Flavius ana conclude kwamba kulikuwepo na FIRMAMENT/Canopy juu ya anga ambayo ilikuwa ikiizunguka dunia kama chuma sababu iliganda huku akiitofautisha kabisa na wingu..... Pia MABABA wa kanisa la kwanza kina Thomas Aquinas,Agustine of Hippo wote kwa nyakati tofauti wanakiri uwepo wa canopy sasa sitaki kuamini hawa wakristo wa kwanza hawafahamu biblia kiasi wapotoshe.
3. Kinachonihakikishia kuwa ni vitu viwili tofauti ni sababu ni vitu viwili tofauti!!....kwanza uwepo wa canopy umezungumziwa hata nje ya biblia kwenye vitabu vya kiyahudi na neno lililotumika kwa maandiko ya kiebrania ndio hilo hilo linatumika kwenye bible ikimaanisha kwamba muandishi wa biblia alikuwa anafahamu kabisa imani za kiebrania ndio maana akatofautisha kati ya Raqia na Anan hivyo hilo neno Raqia ukienda kwenye translation ya kiebrania ndio itakueleza dunia ilikuwa imezungukwa na uzio wa chuma n.k sasa unataka uniambia Musa hakufahamu tofauti hizi wakati ana compile hichi kitabu cha mwanzo??
4. Solid state ya mawingu ni mawingu bado na ndio maana daudi kwenye sura zinazofuatana kaeleza kuwa kuna MAWINGU na UZINGO WA CHUMA sababu alifahamu tofauti hii kwa kusoma imani za mababu zao wa kiyahudi na ndio maana hata waandishi wa biblia wamezitofautisha sababu ingekuwa kitu kimoja wangeipa jina mmoja mfano mawingu as mawingu kwenye biblia yamepewa majina karibu 5 ila yote yaliwa converted kwa kiingereza yanabaki mawingu je kwanini waliweka exception kwa haya MAJI JUU YA ANGA kama kweli ni concept moja na mawingu???
5. Kuhusu unyevu nimeelezea vyema kabisa kwenye post ya kwanza kwamba hata kwa uwepo wa canopy ilitengeneza unyevu mzito sana kuliko hata wa mawingu ya sasa na ndio maana Mungu alitumia unyevu kukuza mazao na hakuleta mvua soma mwanzo 2:5-6.....
6. Mvua haikuwepo kabla ya gharika sababu biblia inaonyesha hivyo kwenye mwanzo 2:5-6 hadi inapotajwa kwenye gharika na ndio maana biblia ikasema ''madirisha ya mbinguni'' yalifunguliwa haikusema mawingu or any sort sababu hayakuwepo hadi baada ya gharika ndipo mwanzo 9 inasema uwepo wa mawingu kwa mara ya kwanza
Pia kingine ni logic tu sababu unaona Nuhu kwenye maandiko mbalimbali alipuuzwa sababu walimuona anaongea kitu ambacho hakipo ila kwa mfano kama angesema MVUA inakuja kumbuka alikaa miaka zaidi ya 40 ina maanisha hapo kati kama kulikuwa na misimu ya mvua na haikuwa na gharika je ni mvua gani alitumia kutisha watu??? Yaani misimu ya mvua 80 ipite alafu bado unawaambia MVUA KUBWA ZINAKUJA sidhani kama hata wwe inakuingia akilini ila kwa kuwa mvua ilikuwa haijawahi onekana ndio maana walimpuuza sababu walijua anaongea kitu ambacho hakipo
All in all nachotaka tuelewane ni kwamba mawingu na canopy/firmament ni vitu 2 tofauti kwa waebrania hivyo tusivichanganye kabisa
Ubarikiwe