CS Mohammed: At Namanga every day crosses 120 trucks from Tanzania vs 30 from Kenya

CS Mohammed: At Namanga every day crosses 120 trucks from Tanzania vs 30 from Kenya

Thamani ya trela moja ya bidhaa kama madawa ,ambazo ndio export kubwa ya Kenya nchini Tz, ni sawa na thamani ya trela ngapi za maharage na mahindi? 15,20,25,30? Tafakari hayo.
Hahahaha, dawa zipi ambazo Kenya mnauza kwa Tanzania, ni Flagyl na anti pains, hazifiki hata aina NNE.

Muhimu ni kwamba, Kenya mnauza bidhaa ambazo sio muhimu kwa Tanzania, kwahiyo Tanzania haiwezi kuathirika kabisa kwa kufungwa kwa mipaka wakati Kenya hamuwezi kuishi hata kwa siku kumi bila ya bidhaa toka Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jombaa kuna kitu flani kinaitwa google. Ingia humo kama unataka kufahamu majina ya kila dawa ambayo iliingia Tz kutoka Kenya. Kama unabisha kuhusu hizo takwimu za TRA zinazoashiria kwamba madawa ndio yalikuwa export kubwa ya Kenya nchini Tz mwaka jana, fika kwenye ofisi zao kesho asubuhi.
Wewe uliyesema ndiye unapaswa kuleta huo ushahidi, sio kuwapa watu home work wafanye kwa niaba yako. Kenya zaidi ya 98% ya dawa zenu mnatoa India, iweje eti ninyi mnauza madawa nchi zingine kwa wingi?.

Tanzania zaidi ya 98% ya dawa zetu zinatoka India, Kenya ni aina kama nne ya dawa (Non Essential medicines).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijua mtaingiza porojo maanake huwa mna allergy kali sana ya takwimu. Haijalishi ni bidhaa zipi haswa kutoka kwa viwanda vya Kenya. Ila natumai mmeona kwamba mwaka uliopita Kenya iliwapiga bao la kibiashara la $35.8 million(takwimu za TRA/BoT sio mabeberu). Hivi mnajua pia kwamba 70% ya mahindi ambayo Kenya huwa inaagiza kutoka nje yanatoka Uganda? K.m. mwaka huu wa 2018 baada ya Kenya kuzalisha tani 360,000 pengo la demand lilosalia nchini waliagiza tani 66,900 Uganda na Tz tani 10,000 tu. Kenyans import $31.2m maize from the region to meet demand - Kenya
Utawaua kwa presha wasingizie sukari😁😂
 
Juma na Damasi wanagombana 😁😁😁😁
 
Wewe uliyesema ndiye unapaswa kuleta huo ushahidi, sio kuwapa watu home work wafanye kwa niaba yako. Kenya zaidi ya 98% ya dawa zenu mnatoa India, iweje eti ninyi mnauza madawa nchi zingine kwa wingi?.
Tanzania zaidi ya 98% ya dawa zetu zinatoka India, Kenya ni aina kama nne ya dawa (Non Essential medicines).
Naona umepokezwa soprano kwenye hiyo kwaya yenu ya porojo. Nikikueleza ulete takwimu kuhusu hayo madai yako kwamba Kenya huwa inaagiza 98% ya madawa ambayo yanatumiwa nchini utapuuza. Kama tu ulivopuuza hizo takwimu za TRA zinazoashiria kwamba madawa ndio zilikuwa top export ya Kenya nchini Tz mwaka jana. Ila unalazimisha sana kwamba nikupe majina ya madawa yenyewe. Hizo zinaitwa sideshows ambazo huwa sikubali zinipotezee muda wala focus. Kama huna mb za kujifanya hiyo homework omba kwa jirani. Au jiliwaze tu kwamba ni madawa ya kuua fangasi kama ulivonieleza hivi majuzi. Ok?
 
Utawaua kwa presha wasingizie sukari
Aaah wapi? Sukari yenyewe madukani wanainua kilo moja kwa bei sawa na ya kilo mbili nchini Kenya. [emoji1]
2370834_professorjaytz-20200417-0001.jpg
 
Safi kabisa.. Wavuja jasho wa Afrika Mashariki tunatunishiana misuli ili hali kinchi kama Belgium [emoji1045] kenye watu takribani millioni kumi na mbili tu kina gdp ya 532usd billion wakati wavuja jasho wa Afrika Mashariki tupo zaidi ya 180 million lakini combined gdp yetu ni roughly 200usd billion.. Tuendelee tu kubishana ujinga nani yuko juu…
Huwezi izungumzia Belgium bila kuizungumzia Congo, sasa jiulize hizo nchi za Afrika Mashariki zinaingia mara ngapi kwa Congo?
 
Wewe uliyesema ndiye unapaswa kuleta huo ushahidi, sio kuwapa watu home work wafanye kwa niaba yako. Kenya zaidi ya 98% ya dawa zenu mnatoa India, iweje eti ninyi mnauza madawa nchi zingine kwa wingi?.

Tanzania zaidi ya 98% ya dawa zetu zinatoka India, Kenya ni aina kama nne ya dawa (Non Essential medicines).

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyang'auz washasahau 80% ya bidhaa zao wanazoexport hasa matunda utokea kwetu tena wananunua local,yakifika kwao wanayafunga kwenye na chapa juu!
 
Tanzania wamenyekea lakini... Rafiki yangu huko Monduli ambaye ni mkulima aliniambia jana huu ujinga wa Magufuli unawafka mwisho sasa....

Soko lao kuu ni Kenya, wakikosa soko itakuwa balaa ...
Soko si kenya pekee!! Hata hivyo inawezekana kuhifadhi mazao hata kwa mwezi mmoja wakati unaandaa mpango wa soko jingine. Lakini haiwezekani kukaa na njaa wakati ukitafuta mahali pengine pa kununua chakula. Utalazimika kutumia pesa zaidi kipindi hiki kwa sababu ya upungufu wa chakula na bei kupanda juu.
Wote tunaathirika lakini kenya wanaathirika zaidi. Ndio maana tumeona vurugu na kuchoma matairi huko kenya lakini hakuna vurugu Tanzania.
 
Mzee, kabishane na TRA, BoT ndio hizi takwimu zao>>> iTanzania trade with Kenya turns into deficit Tangia mpate uhuru isipokuwa 2014-18, hakuna mwaka ambao mmeuzia Kenya bidhaa za jumla ya thamani ya juu zaidi ya mnazonunua kutoka Kenya. Mwaka jana mmepata deficit ya $35.8 million kwenye biashara na Kenya. Top export za Tz, mahindi, maharagwe, kamba za makonge. Top export za Kenya, madawa, sabuni, bidhaa zingine kutoka kwa viwanda. Una swali lingine?
Hizo tunazonunua kwenu sio basic necessity and there are many alternatives to that within our country. But Kenya has no alternatives within their country!
 
Hizo tunazonunua kwenu sio basic necessity and there are many alternatives to that within our country. But Kenya has no alternatives within their country!
Inafaa urudi shuleni ndio ufunze upya kwamba supply huwa inafata demand. Sio jambo la kubahatisha kwamba madawa ndio yamekuwa top export ya Kenya nchini Tz, yakifatiliwa na bidhaa zingine kutoka kwa viwanda vya Kenya. Tena bidhaa za Kenya mnazinuanua kwa wingi zaidi ya Kenya inavonunua kutoka Tz. Alafu hiyo ndio taswira kwenye nchi zote ukanda huu wa Afrika mashariki na ya kati. Inaitwa nchi ya viwanda sio viwonder.
 
Back
Top Bottom