Soko si kenya pekee!! Hata hivyo inawezekana kuhifadhi mazao hata kwa mwezi mmoja wakati unaandaa mpango wa soko jingine. Lakini haiwezekani kukaa na njaa wakati ukitafuta mahali pengine pa kununua chakula. Utalazimika kutumia pesa zaidi kipindi hiki kwa sababu ya upungufu wa chakula na bei kupanda juu.
Wote tunaathirika lakini kenya wanaathirika zaidi. Ndio maana tumeona vurugu na kuchoma matairi huko kenya lakini hakuna vurugu Tanzania.
ha ha kwani Tanzania ndiyo wanalima chakula peke yake..?
Kitu kitakachofanyika ni kuwa bei ya bidhaa kama vitunguu itaongezeka kwa sababu wakulima wa Kenya hawatakuwa wamezalisha vya kutosha... miezi mitatu tutakuwa tumeongeza ukulima...
Hapa Wakulima wanaomba mpaka ufungwe waweze kupata pesa, Chakula cha TZ kinaharibu soko...
Tena nchi kama Uganda hawana ujinga kama huu wenu... tutaongeza ununuzi huko..
Thamani ya trela moja ya bidhaa kama madawa ,ambazo ndio export kubwa ya Kenya nchini Tz, ni sawa na thamani ya trela ngapi za maharage na mahindi? 15,20,25,30? Tafakari hayo.