Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

Elections 2015 CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima! Vinginevyo, huo ndio mwisho wake

E
Muungano ni uhai wa Tanzania. Sasa jiulize how far will you go kulinda uhai Wako? Ukifanikiwa basi utakuwa umepata jibu.


Ethiopia na Eritrea zimevunja muungano
mbona zipo better zaidi?

mbona Checkslovakia imevunjika? na hakuna baya lilitokea?
 
Naona unajikanyaga tu,adui wa wazanzibar kwenye harakati hizi za kujikomboa kwenye makucha haya ya mkoloni anajulikana,wazanzibar wapo tayari kupambana nao liwalo na liwe.
Ukombozi gani unaouzungumzia zaidi ya yale Mapinduzi Matukufu yaliyoikomboa Zanzibar toka katika makucha ya mvamizi hasidi yule aliyefuushwa?!.

Huyu unayemuita mkoloni ndie mkombozi wenu kupitia muungano wetu adhimu vinginevyo mngeendelea kuchinjana kama kuku na kuvishana majiwe ya shingo na kutosana baharini!.

Tulipo ungana tulikubaliana wote wawili tungechangia uendeshaji wa huu muungano, lakini mpaka sasa mbebaji wa mzingo wote ni mtu mmoja tuu!, Watu wanapewa mishahara bure, polisi bure, jeshi bure, elimu bure, umeme bure!, na fedha za maendeleo asilimia 4.5% halafu leo ndio kwanza badala ya shukrani, unaitwa mkoloni!, ama kweli shukrani ya punda mateke!, fadhila mfadhili mbuzi, utauonja mchuzi lakini binadamu....!.

Pasco
 
kuulinda muungano kwa gharama yoyote!.

gharama yoyote inamaanisha hata kutomtangaza mshindi.........maalim hapendi muundo wa muungano neno gharama yoyote ndo linatu cost.
 
Wanabodi, baada ya kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, kuna watu wanadhani Chama cha Wananchi CUF, kina hiyari ya kushiriki uchaguzi huo au kutoshiriki, as if kushiriki uchaguzi wa marudio ni jambo la hiyari!, no way!, watakuwa wanajidanya!. CUF hakina option yoyote ya kuamua ama ishiriki ama isishiriki uchaguzi huo, kwa sababu ushiriki wa uchaguzi wa marudio sio suala la option bali ni jambo la lazima, watake wasitake ni lazima washiriki, kwa sababu kila kitu kiko vile vile kama mwanzo!, nikimaanisha hata wakisusa, picha na majina ya wagombea wao yatakuwepo kwenye karatasi za kura!.

Wenye option ya kuamua kushiriki au kutoshiriki uchaguzi huo ni wapiga kura, ndio wanaweza kuamua ama kujitokeza kushiriki kupiga kura, au kususa kupiga kura kwa kutokujitokeza, na mgombea hata kama atapata kura moja ya ndio, ndio atatangazwa mshindi!, hivyo kupiga kura au kutopiga kura ndio bado ni option!, lakini kushiriki uchaguzi huo sio option ni jambo la lazima!.

Iwapo CUF itatangaza kususia uchaguzi huo, tangazo hilo ndilo litakuwa tangazo rasmi la kifo rasmi cha kilichokuwa kinaitwa Chama cha Wananchi CUF, kwa sababu, ngome kuu ya CUF ni Pemba, kususia uchaguzi ni kuipoteza Pemba ambapo na ngome kuu ikiishakuangua, it is just a matter of time, chama chenyewe chote kielekee kaburini!.

Hata kama CUF watatangaza kususa, majina ya wagombea wa CUF tayari yako kwenye karatasi za kura katika uchaguzi huo, hivyo wakitangaza kususa, maana ni wagombea wa CUF hawatachaguliwa, hivyo kuipatia CCM ushindi wa mezani, ikiwemo kuitwaa ngome ya CUF kule Pemba na kuivunja uti wake wa mgongo, kwa CCM kuvitwaa viti vyote vya Uwakilishi Zanzibar na Pemba, ambapo pia huo ndio utakuwa mwisho wa SUK na CCM kutawala peke yake na kuhitimishwa kwa kifo rasmi cha chama cha wananachi, CUF!.

Nakiri kupandisha uzi huu kufuatia bandiko la mwana jf huyu


Hoja katika badhiko hilo mi kitisho cha CUF kuwa kisiposhiriki, hali ya amani na utulivu wa visiwa vya Zanzibar, utakuwa mashakani!. Maadam Zanzibarr sio nchi bali ni sehemu ya JMT, dhima ya muungano, ni undungu wa asili kati ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, lakini sababu halisi ya muungano ni kuipatia Zanzibar ulinzi na usalama, Zanzibar haina polisi wala jeshi, hivyo jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Zanzibar tuu, bali ni jukumu la JMT, haiwezekani sehemu moja ya JMT iwe katika hali tete, wakati JMT ni nchi moja, ulinzi na usalama wa JMT utakuwa mikononi mwa JMT!.

Hivyo CUF washiriki uchaguzi huu wa marudio, au wasishiriki kwa kuususia, it will not make any difference kwenye amani na utulivu wa Zanzibar kwa sababu jukumu la ulinzi na usalama wa Zanzibar, sio jukumu la Wanzanzibari wenyewe pekee, bali pia ni jukumu la serikali ya JMT, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Dr. Joh Pombe Magufuli!.

Zanzibar kama sehemu ya JMT, inayo assuarance ya Amri Jeshi Mkuu wa JMT, kuhakikisha kuwa Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, uliotangazwa, utafanyika kwa uhuru, amani, usalama na utulivu, mshindi atapatikana kwa haki, atatangazwa, ataapishwa na kuunda serikali nyingine ya Zanzibar yenye jina la SUK lakini wawakilishi wa CUF kuendelea kuitawala Zanzibar kwa uhuru na amani kabisa bila`wasiwasi wowote kwa ile falsafa ya kule ya Mapinduzi Daima!.

Demokasia ya kweli ni serikali ya watu, inayoongozwa na watu kwa manufaa ya watu hao!, (of the people, by the people, and for the people), ila demokasia hiyo haikuwe kiwango cha asilimia ya watu hao!, hivyo hata kama nchi ina watu milioni moja, serikali ikachaguliwa na watu 10 tuu, bado serikali hiyo itakuwa ni serikali halali kisheria, japo itakosa peoples legitimacy, kwa watu hao ndio watakuwa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kutokupiga kura!.


Kushiriki uchaguzi wowote, kwa kugombea nafasi yoyote ni hiyari, pia kuamua kutokushiriki katika uchaguzi pia ni hiyari, sambamba na kujiandikisha kupiga kura ni hiyari, kutokujiandikisha pia ni hiyari, na kujiandikisha kupiga kura na kisha kuamua kutokupiga kura pia ni hiyari, zote hizo ni demokrasia.Kama CUF itawashawishi wafuasi wake kususia uchaguzi huo, hiyo itakuwa ndio demokrasia yao!.

Kitendo cha CUF kushiriki uchaguzi wa mwanzo kunaifanya CUF ni lazima ishiriki uchaguzi wa marudio sio kwa hiyari ua kwa kupenda, bali ipende, isipende, ni lazima ishiriki uchaguzi huo!.

Hapa hakuna suala la choice. Na iwapo CUF watasusa kushiriki uchaguzi huo wa marudio, kususa huko kutakuwa ni kususa batili kwa sabu picha na majina ya wagombea wa CUF yataendelea kuwepo kwenye karatasi za kura!, hivyo kususa huko ndiko kutakao ipatia CCM ushindi wa mezani, tena this time CCM itashinda viti vyote vya uwakilishi Unguja na Pemba, na huu ndio utakuwa mwisho rasmi wa CUF. Kamwe CUF isikubali kuingia katika mtego wa kususia uchaguzi wa marudio!.

Turufu ya CUF kutishia kususa ni kwa kisingizio cha itabembelezwa ili kusitokea machafuko Zanzibar!. Kiukweli JK alikuwa ni mpole sana, hivyo Zanzibar imemchezea sana hadi kumtia vidole machoni katika yale mabadiliko batili ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010.

Kwa sasa Amiri Jeshi Mkuu ni Dr. John Pombe Magufuli, hii ni namba nyingine, huyu sio mtu wa mchezo mchezo au kuchezewa kama JK, hivyo CUF kama wanadhani watasusa na kubembelezwa, ili kuepusha machafuko Zanzibar, nawahakikishia this time watakuwa wame bugi step, hata wakisusa, hakutakuwa na vujo wala ,achafuko yoyote Zanzibar kwa sababu sasa ni zamu ya hapa hapa ni kazi tuu!.

Wanzanzibar, na Watanzania wote, chini ya Amiri Jeshi Mkuu, wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya JMT, tuna jukumu kubwa la kuilinda amani na utulivu wa eneo lote la JMT, ikiwemo Zanzibar, kwa gharama yoyote!, hii ikiwa ni pamoja na kuulinda muungano kwa gharama yoyote!.
Wasalaam
Pasco
Ngumu kumesa.........
 
Kama katiba mpya itakuwepo yenye kuzingatia, utawala bora, yenye demokrasia ya kweli, na ifuate mapendekezo ya wananchi. Huu upumbavu wa chama kimoja kujidai wamiliki wa nchi hii utakwisha. Mabavu ya hili li chama lililopo madarakani itakuja kutuletea matatizo makubwa sana ktk nchi hii.
 
Hivi Ninyi Mna Wazimu Eeee!!!? Kwa Sheria Ipi Hiyo!!!!?? Kama Kufutwa Kwa MATOKEO Ya UCHAGUZI Wa 25 Oct 15 Hakufuata Sheria Za ZEC, Katiba Na Sheria Ya Uchaguzi!!! IWEJE Kwa CHAMA Ambacho Kimeamua Kutoshiriki Batili Na Ukinyagwaji / Ubakwaji Wa Katiba Na Sheria, Eti Ndio Kiwe Hatarini!!!!!!??? Hivi Mnadhani Kwa Vitisho Na Hoja DHAIFU Kama Hivi, Ndio CUF Wataogopa!!!!!??? Mnajisumbua Buree!!!
 
E



Ethiopia na Eritrea zimevunja muungano
mbona zipo better zaidi?

mbona Checkslovakia imevunjika? na hakuna baya lilitokea?

Hata huu muungano hauna ubaya, una changamoto tu. Je tuvunje muungani kisa changamoto chache zinazoletwa na CUF? Halafu sidhani ni sawa kulinganisha muungano wetu na wa Czechslovakia na Ethiopia na Eritrea kwasababu misingi (sababu) za kuanzisha kila muungano ni tofauti.
 
Mkuu GHIBUU, tangu lini rais wa Zanzibar ni rais nje ya Zanzibar?!. Tanzania ni nchi moja tuu ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania bara na Tanzania visiwani, au Tanzania Zanzibar. Ndani ya Muungano, sehemu ya Zanzibar inajitegemea kwa utawala wake wa ndani, lakini nje ya Muungano, hakuna nchi ya Zanzibar, bali kuna sehemu ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya JMT!.

Uchaguzi wa Zanzibar ni mambo ya ndani, uchaguzi wa JMT uliisha kamilika, hivyo JMT haihusiki na uchaguzi wa ndani wa Zanzibar, ila Ulinzi na Usalama sio suala la ndani ya Zanzibar, hili ni suala la JMT, sasa kama uchaguzi wa Zanzibar utaleta tishio lolote la ulinzi na usalama, JMT ipo kuhakikisha hili halitokei!.

Sio tuu rais wa Zanzibar, bali wale wakuu wote 4 wa Zanzibar wanaotembea na vingora, wakija baa au wakisafiri kwenda nje ya nchi, balozi za JMT huwa wanawapatia heshima stahiki.

Pasco
Mkuu pasco

Zanzibar kuna mambo hayako katika orodha ya muungano, hivyo inajiwakilisha wenyewe. Popote pale.
Ndani ya Zanzibar kuna Balozi ndogo ambazo za mataifa ya nje, ingawa zanzibar sio huru kimataifa lakini inatambuliwa ni nchi na ndio maana Balozi zipo zanzibar.

Mkuu huyu rais asiweza kwenda nje ni rais wa aina gani? Huyu rais wasio mtambua nje ni waina gani, hawa mawaziri wetu wasio tambulika na mataifa ya nje ni mawaziri wa aina gani?

Ukisikia kufa kwa zanzibar ndio huku, tumezoea kuona mabalozi wa Tanzania kuja kumuona rais na Makamu wa kwanza na pili. Sijui baaada ya huo uchafuzi nani watatutembelea. Hii serekali itakuwaje? Naona itakuwa Wilaya.

Nikuulize

Ikiwa wananchi wa Zanzibar watasusia kupiga kura zaidi ya asilimia 50 uchaguzi na vyama kususia uchaguzi utakuje huu uchaguzi kisheria?

Mkuu hayo ni mambo ambayo ninayo yafikiria.
 
Mm huwa nawatahadharisha sana watanganyika,moto wanao uchochea ukija kuwaka wasidhani watanganyika watabaki salama zanzibar.
Acha na mimi nikutadharishe wewe mbaguzi, usidhani na nyie mtabaki salama. Vitisho kama hivi havisaidi na nia zenu uovu za kuvunja muungano hazitafanikiwa.
 
Hoja ya Pasco ni nzito, asibezwe. Uhai wa chama cha siasa unapimwa kwa wingi wa wanachama na iwakilishi kwenye vyombo vya mamuzi kama udiwani na ubunge. Endapo cuf watasusa, watakosa madiwani na wawakilishi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Ni sawa na kujifuta kisiasa. Je, uamuzi huo utakuwa na tija kwa cuf . Hapana.

Natumaini viongozi wa cuf wataweka pembeni hasira na kutumia busara na hatimaye kuamua kushiriki uchaguzi. Treni ya jecha inataka kuanza safari. Atakayeshindwa kupanda ataachwa. Asilalamike. Serikali ya muungano haitaruhusu wataotaka kufanya vurugu. Na ukweli ni kwamba bila cuf siasa za zenj zitapooza sana. Hatutaki pia hilo litokee.
Hakuna Kitu Kama Hicho Mkuu!! Mwanzo Nilikuwa Nadhani Mleta UZI Na Ww Mchangiaji Ni WATU MAKINI MNO, Ktk Kuchambua Na Kujenga HOJA Zenye Mashiko, But Kwa UZI Huu Na Ujengaji Hoja Wako, Yanipasa Kubadili Fikra Zangu Kabisa!!! Kumbe ELIMU Ya MTU Sio Utitiri Wa VYETI Au Kuishi Mazingira Hayo!!!! Bali Ni Ule UWEZO Wake Wa Kutafsri ELIMU Yake Ktk Vitendo Na Maelezo Yake!!!! SASA Subirini 27 Na 28 Jan 16! CUF Watatoa Tamko Lao Rasmi La Kutoshiriki UCHAGUZI Huo Batili!!!! ALAFU Tuje Tuone Hayo Maneno Yenu Yaliojaa Taka Choo!!! KAMA Mngekuwa MNAJITAMBUA, Msingejaribu Kuleta Uzi Huu Na Hoja Mbovu Hivi!!! MAANA CCM Wasingeweka Nguvu Ktk Kujadili Suala La UCHAGUZI Kurudiwa Kwa Kuwakusanya Viongozi Wao WASTAAFU Kujaribu KUMSHAWISHI Mh. Maalim Seif Akubali KUREJEWA Kwa UCHAGUZI!! SI Wangekuwa Wametangaza Tu Tarehe Basi, Kwa Vile CUF Watake Wasitake, Lazima Watashiriki Tu!!!! KWA Kuwa Hilo HALIWEZEKANI, Ndio Maana Walikuwa Wakimshawishi Akubali!! SASA Hayo Maneno Yenu Yenye HOJA DHAIFU Mnayatoa Wapi? Kama Si Ktk Vilabu Vya Pombe Ya Komoni!!!!!
 
Kila siku najiuliza hili swali
watu wanaosema 'tutaulinda muungano wetu' kwa gharama yoyote

exactly wanamaanisha nini?
why huu muungano ulindwe kwa nguvu?


Hilo kaulize nchi zilizoungana kama Uingereza, Marekani, Uchina na Taiwani, Ujerumani, AK n.k
 
Back
Top Bottom