Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

Kuchaguliwa tena? sijui kama itakuwa rahisi kwani CCM sio Ile ya 2015 sasa hivi watashinda hata kwa nguvu yaani ni ubabe usipime. Maalim Ana option moja ampigie magoti lipumba akubali amezidiwa kete yaishe

Sent using Jamii Forums mobile app
Atakuwa anaipigia magoti CCM. Itakuwa kosa kubwa sana kisiasa.
 
option namba mbili ni the best option kuna maeneo yameanza kupwaya CDM hvy kuongeza nguvu ni mhm sana
 
Ilikufa KANU chama tawala na watu wakapeta,uhuru huyo hapo anafanya yake.Hmwatu wanabadilisha timu tu kama kwenye mpira then harakati zinaendelea
 
Mnaodhani seif akihamia cdm atakuwa na nguvu ileile mnakosea,

Seif akihamia cdm ameua kila alichokuwa akikipigania zanzibar, anachotaka seif na wazanzibar walionyuma yake ni Zanzibar huru! Kuitawala Zanzibar chini ya cdm hakutakuwa na tofauti na Zanzibar chini ya ccm.

Bado rais wa Zanzibar atapaswa kuwajibika kwa mwenyekiti cdm bara sawasawa na ilivyo kwa ccm leo, cdm inaweza kumfuta uanachama muda wowote iwapo atakwenda kinyume na cdm bara hivyo bado Zanzibar itaongozwa na bara kama ilivyo sasa,

Seif kama anatoka cuf atengeneze chama kingine kisha akisambaze bara huku nguvu kubwa au madalaka yote yakiwa Zanzibar, kisha chama hicho kipya kitaungane na ukawa ili kujieneza bara kwa kutumia nguvu ya cdm bara pia kitapata uungwaji mkono. Na kwakuwa cuf haitakuwa na nguvu tena Zanzibar na bara ikikosa uungwaji mkono itakufa kifo kitakatifu, huku chama kipya cha seif kikichukua nafasi ya cuf bara na visiwani na kwa njia hiyo Lipumba na cuf yake watabaki kama kupe kwenye ngozi ya ngombe iliyichunwa tayari.

Lakini hatua hii itategemea uaminifu wa cdm, kama cdm watamgeuka yeye na chama chake kipya watakufa kifo kitakatifu au watabaki kuwa chama cha Zanzibar pekee,

La pili seif achukue hatua sasa ili apate nafasi ya kutosha kukijenga chama chake kabla ya wakati wa kampeni na uchaguzi.

Tatu akubali kupoteza madai yake ya urais wa zanzibar na wabunge wake wote maana kwa katiba yetu uharali wa madai ya kuibiwa urais anakuwa nayo akiwa mwanachama wa cuf other wise hawezi kupigania nafasi ya urais wa cuf ukiwa mwanachama wa chama kingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasikitikia sana viongozi wanaoshindana na nature.Mabadiliko katika maisha ya binadamu huwa hayaepukiki hasa wakati wake unapofika.Suala la CCM kuchokwa halichochewi na vyama vya upinzani bali ni wakati wenyewe umekwishafika kwa hiyo watu wanatafuta mlango tu wa kupitia.Hata visingekuwepo vyama vya siasa lazima watu wangetaka mabadiliko tu.Kulikuwa na Saul,Farao,Caesar na viongozi kibao lakini wote wamebaki kwenye vitabu vya historia.Napenda kumshauri ndugu yet Nduli B asitumie nguvu na gharama kubwa kuurudisha nyuma muda bali asome alama za nyakati.Hata kama utatoa betri kwenye saa jua haliwezi kuacha kutembea eti kwa sababu saa yako imesimama.JIFUNZE KUTAFAKARI BABAA.
 
Mwenye nguvu na mamlaka awafute haraka tujue nani ni nani na yupo na anafanya siasa kwa manufaa ya nani!Inachosha na kuharibu akili kusikia siasa za fitina kila siku!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali langu lilikuwa na maana ya kutaka kujua kama Lipumba ana nia ya kuimarisha ushirikiano wa UKAWA au la, na je, anaamini kuwa Maalim ndiye aliyeshinda katika uchaguzi wa 2015 kule visiwani??
 

Usomi wa Lipumba kama ndio unaomwelekeza kufanya ayafanyayo basi hauna tija yoyote.
 
INAONEKANA HUYO ALIYENYUMA YA LIPUMBA ANABARAKA ZOTE KUTOKA CHADEMA, KWASABABU KILA NIKIANGALIA KINACHOENDELEA CUF HIVI SASA CHADEMA NDIO WANUFAIKA WAKUBWA..!!

Mie naona wanafaikaji wakubwa ni CCM wala sio CHADEMA.
 
We umeiona CUF wakati wa uchaguzi juzi tu? Unajua bara CUF imejengwa na nani? Unakumbuka container la visu wewe? Unakumbuka Ngangari na Ngunguli ya inspector Omari Mahita?
Hiyo CUF ya Ngangari na Ngunguri haikupata zaidi ya wabunge wawili huku viti vya Kilwa, Mwanza na Tanga vikiliwa na le-profesale
 
Hiyo CUF ya Ngangari na Ngunguri haikupata zaidi ya wabunge wawili huku viti vya Kilwa, Mwanza na Tanga vikiliwa na le-profesale
Hapa kuna kitu mnajifanya hamkioni...
Kilichopelekea Cuf na Chadema kuvuna viti vingi vya ubunge ktk uchaguzi mkuu uliopita sio nguvu ya Lowasa bali ni Ukawa ambao ni matokeo ya Profesa na Dr. Slaa.
Lowasa ndiye aliyekuja kuharibu uelekeo wa Ukawa.
Ndiye chanzo cha migogoro ndani ya Cuf.
Suala la Cuf kuwa na wabunge wawili bara ikiwa ni dhambi basi dhambi hiyo haiwezi kumuacha salama Maalim Seif kwani ndiye mtendaji mkuu wa dhughuli za chama.
Sawa sawa na mafaniko yaliyopo Chadema huwezi kuyatenganisha na Dr.Slaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…