Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

Tetesi: CUF: Lipumba kuwafuta uanachama wabunge wote wa kuchaguliwa majimbo yote ya Bara

CUF HAITAKUWA IMARA TENA! MISSION IMEKAMILIKA KWA 80+℅

CUF sasa inaishilia, ni kama mpango unakamilika, mpango mkakati umetengenezwa kimkakati zaidi, kuhakikisha CUF haina nguvu tena, ili kuleta unafuu visiwani. Wabunge wa majimbo wakishavuliwa uanachama, majimbo yao yatakuwa wazi, uchaguzi utarudiwa, kama hujui ni mpango,: kumbuka kauli ya juzi ya mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, pale aliposema' ikiwa wabunge wa CUF watavuliwa uanachama, tume imejiandaa kwa dharula yoyote na bajeti ipo! Akili kumkichwa' mkurugenzi wa tume anazungumzia uchaguzi mdogo kwenye majimbo ambayo bado yana wabunge! MISSION

Lipumba sasa anatambuliwa na kila taasisi ya sirikali, anatambuliwa na Bunge, anatambuliwa na Msajili, anatambuliwa mpaka na taasisi ya jikoni! MISSION

Kete kwa upande wa CUF Halisi ilikuwa imebaki moja tu (MAHAKAMA) baada ya makosa kufanyika nyuma! Ndiyo makosa yalifanyika mwanzo kabisa kwa upande wa Maalim Seif kumdharau Lipumba na kumuona ni mtu mmoja tu anayetapatapa kisha atatulia, hawakumuona mapema aliyekuwa nyuma ya Lipumba! Hili lilikuwa Kosa kubwa! Wamekuja kushituka na kuiona nguvu yake kipindi ameingilia bodi ya wadhamini ya CUF! Hapo ndo walishituka na kumbe tayari walikuwa wamechelewa! Walipaswa kumshughulikia mapema!
Sasa kete ya mahakamani nayo inaanza kufeli, kwa nini nasema inafeli?

1😛amoja na kesi ya kutomtambua Lipumba na kauli ya Msajili kuwa mahakamani! Bado Lipumba ameendelea na shughuli za chama kwa kujitanua hadi kufukuza wabunge bila woga na hakuna mhimili unaohoji!

2: Kutupiliwa mbali kwa mapingamizi ya wabunge wa CUF waliovuliwa uanachama, ni pigo kubwa kwa upande wa Maalim Seif! Hata wakirekebisha vifungu walivyotakiwa kuvirekebisha, wao wako mahakamani, Lipumba anaendelea na shuguli za chama huku akijipanga kuwaita na kuwahoji wabunge wa majimbo!

3: Kutotambulika kwa maazimio ya CUF upande wa Maalim wa kuwavua ubunge wabunge wawili ni pigo kubwa pia.

NANI ALAUMIWE

1. Mtatiro;
Ndiyo, huyu ni mtu wa kwanza kabisa kulaumiwa na wana CUF' atanisamehe. Yeye alipewa jukumu kuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Lakini amekuwa akifanya siasa za mtandaoni zaidi, kila Lipumba akifanya jambo, yeye huja kulalamika mtandaoni na hukomea kuandika tu bila ya kuelezea njia mbadala ( rejea post zake kwenye plofile yake) Sasa kama yeye kiongozi analalamika na kujibu mapigo ya Lipumba mtandaoni, wengine watafanyeje? Yeye huiongelea CUF baada tu ya Lipumba kufanya kisanga, Lipumba akiwa kimya' na yeye yuko kimya. Kwa hiyo amekuwa akicheza ngoma ya Lipumba!

2. Maalim Seif
Yeye namlaumu kwa kutochukua hatua mapema, Lipumba hakupaswa kupewa nafasi mapema, naye sasa amekuwa akijibu mapigo ya Lipumba tu badala ya Lipumba kujibu mapigo yake! Lipumba akiita Baraza lake, naye anaita lake, Lipumba akifukuza wabunge, naye anafukuza! Amechelewa sana!

NINI CUF YA MAALIM IFANYE?
Kwa sasa CUF ya Maalim imebanwa sana na Lipumba, na naona imebakiwa na option mbili tu!

1. Mahakama;
Mahakama pekee kwa sasa ndo imebaki kuweza kuamua kama CUF iwe ya Lipumba au ya Maalim. Na ikitokea mahakama ikaamua kuwa CUF iwe ya Lipumba, Maalim atabaki na option mbili tu, mosi kuungana na Lipumba au

2. Kuongeza nguvu CHADEMA.
Option ya mwisho kabisa kwa Seif ni kutangaza kuachana na siasa za CUF ya Lipumba na kuongeza nguvu upande wa CHADEMA. Faida kubwa kwa upande wa CHADEMA ikiwa hili litatokea, ni kupata wafuasi wengi Zanzibar bila chenga! Na hapo ndipo msemo usemao "Waliokuwa nyuma ya Lipumba waliruka mkojo wakakanyaga kinyesi" utatimia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchambuzi mzuri, ila sikubaliani na haya ya mwisho. Maalim akienda cdm ataenda peke yake kama EL. Nyumbu siyo wengi katika siasa za tz.
 
hiyo option no 2 ya kujiunga na chadema ifanyika kama mambo yatakuwa hivi mpaka 2020 hapo amwacie Lipumba chama ijifie nacho
 
Mkuu hio option namba 2 nimeipenda sana na ndilo linalotakiwa kutekelezwa na cuf maalim
Hapana watakuwa na aina yao ya CUF !kumbuka maalim hana interest kuu ya bara . Akichukua wabunge /wawakilishi wwake znz inatosha kuchukua dola zenji huku bara wakiiunga mkono ukawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanapenda kulaumu matokeo hawataki kuangalia chanzo cha tatizo. Tujiulize Lipumba kuachia uenyekiti wa CUF chanzo nini? Je kulikuwa na maridhiano vizuri ni nani ashike hatamu kuiwakilisha CUF kugombea uchaguzi mkuu wa 2015 au watu waliburuzwa ktk kufikia maamuzi hayo? Na kauli gani zilitolewa na walioshinda kumpitimpitisha mgombea wanae mtaka dhidi ya wale walioshindwa ktk majadiliano? Au ilikuwa ile umeshinda vita lakini mapambano bado?
 
Je CUF ikikosa wabunge RUZUKU watapata wapi?

May Allah bless Me and You
 
Katika maisha yangu yote namtumaini Mungu. Lkn mambo anayofanya lipumba namuangalia Mungu mbona unamuacha uyu bwana anatamba kiasi hiki.....
 
Fukuza Mtolea, hana faida yoyote wananchi wa jimbo la Temeke tunajuta kwanini tulimpa kura zetu. Lipumba fukuza huyu jamaa!
 
Ni kawaida kiongozi kua na watu watakaoendana na mkakati wako.

Anachofanya lipumba sio kigeni na ni cha kawaida kama mwenyekiti WA CUF.

Japo nia yake in OVU tangu mwanzo kwakua anatumika.

Ila yeye lipumba hataki chama chake kitumike na cdm, anataka kitumike na ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi kumbe unaweza kuwa Profesa na bado ukatumika vile vile. Nchi hii bhana duuu!!!
 
Fukuza Mtolea, hana faida yoyote wananchi wa jimbo la Temeke tunajuta kwanini tulimpa kura zetu. Lipumba fukuza huyu jamaa!

Hivi wale wanaomshabikia Lipumba wanasemaje kuhusu UKAWA? Wanasemaje kuhusu ushindi wa Maalim kule visiwani??
 
Unapaswa kwanza ujue lengo la walio nyuma ya Lipumba.
Walio nyuma ya Lipumba wanataka Kumfuta Maalim uanachama ili;
☞ kumkosesha platform ya kuongelea mambo ya CUF
☞Kudhoofisha madai yake ya urais wa Zanzibar ambayo yamefikia mahali pazuri kwenye jumuiya za Kimataifa.

Ili kujua Maalim afanye nini lazima kujiuliza kwanza ;
Je, walioko nyuma ya Lipumba wakifanikiwa kumfutia Maalim uanachama (Kitu ambacho watafanikiwa ) , Madai ya urais wa Zanzibar ya Maalim kwenye jumuiya za Kimataifa yataathirika kiasi gani?

Kama hayataathirika basi Maalim apractice kile wazungu wanasema -Stop, look, listen, think and wait .

Kama yataathirika basi Maalim anaweza kuchukua ushauri wako hapo juu.
kila neno uloandika lina uzito sana!.. i salute you!
 
Wasiwasi wangu ni kwamba CCM itapata wakati mgumu Mara dufu kuisambaratisha CHADEMA Visiwani kama inavyofanya kwa CUF ikiwa tu Maalim Seif na kundi lake wataamua kuhama chama

Sent using Jamii Forums mobile app
Me navoona kwa madai anayosimamia Maalim Seif hataweza hama kwa sasa labda ikifika 2020 ndipo atafanya maamuz magumu.
 
Lipumba anatesa kwa udhaifu wa viongozi wa CUF kutochukua hatua mapema
 
CUF HAITAKUWA IMARA TENA! MISSION IMEKAMILIKA KWA 80+℅



NINI CUF YA MAALIM IFANYE?
Kwa sasa CUF ya Maalim imebanwa sana na Lipumba, na naona imebakiwa na option mbili tu!

1. Mahakama;
Mahakama pekee kwa sasa ndo imebaki kuweza kuamua kama CUF iwe ya Lipumba au ya Maalim. Na ikitokea mahakama ikaamua kuwa CUF iwe ya Lipumba, Maalim atabaki na option mbili tu, mosi kuungana na Lipumba au

2. Kuongeza nguvu CHADEMA.
Option ya mwisho kabisa kwa Seif ni kutangaza kuachana na siasa za CUF ya Lipumba na kuongeza nguvu upande wa CHADEMA. Faida kubwa kwa upande wa CHADEMA ikiwa hili litatokea, ni kupata wafuasi wengi Zanzibar bila chenga! Na hapo ndipo msemo usemao "Waliokuwa nyuma ya Lipumba waliruka mkojo wakakanyaga kinyesi" utatimia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Option #3, Cuf ya Maalim ikae na Cuf ya LIPUMBA Wayamalize...
 
Back
Top Bottom