Curriculum Vitae kwa kiswahili ni nini?

Curriculum Vitae kwa kiswahili ni nini?

Vitae mi najua maanake ni life, neno la kilatini hilo
 
Hii ni kopi na pesti kutoka kwenye istilahi zilizosanifiwa na bakita.
[TABLE="width: 734"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]Wasifu[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Mkuu huwezi kutumia kiswahili chepesi kidogo hapo kwene red tukuelewe vizuri? Hili li lugha letu ligumu jamani dah!!
 
Mkuu huwezi kutumia kiswahili chepesi kidogo hapo kwene red tukuelewe vizuri? Hili li lugha letu ligumu jamani dah!!
Mkuu tatizo tumezoea kutumia sana viingereza sasa hadi tunajikuta lugha yetu wenyewe inakuwa ngumu tena.

Istilahi (Terminology) = Msamiati unaotumika katika uwanja maalum, kama vile biashara, lugha, sheria n.k
Sanifiwa (Standardized) = (katika lugha) kuyarasimisha maneno mapya katika lugha husika ili yatumike katika matumizi ya kawaida ya lugha.
 
Kiswahili na maneno yenye asili isiyo kiswahili.
 
Mi nnavojua ni Wasifu Kazi
Kutokana na kanuni za uundaji istilahi, hili neno ni refu sana, ukiangalia dhana ya neno chanzi lenyewe CV basi istilahi ya kiswahili inafaa iwe wasifu (wasifu ni maelezo binafsi kuhusu maisha yako, na kimsingi ndo malezo yapatikanayo katika CV). Kwa hiyo wasifu ni istilahi sanifu ya kiswahili.
 
Ni uelewa 2 mkuu wala hakuna kombe! Naomba nkuulize kuna mising yyt ya uundaji wa istilah?
 
Sorry nnajifunza, kwa mfano ilo neno CV 2natumia msingi gan?
 
Ahhh kumbe mtu akifa wanakuwa wanasoma cv yake wanaposema wasifu

maneno huwa na maana nyng...co moja..vlevle muktadha ndo hutoa maana ya neno..'wasifu' wa mtu kwenye mazko ni tofaut na 'wasifu' utakoombwa wakat unaomba kaz!!!!
 
Back
Top Bottom