Bisansaba
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 292
- 109
Sorry nnajifunza, kwa mfano ilo neno CV 2natumia msingi gan?
Kisawe cha CV katika kiswahili ni Wasifu, kwa hiyo hapa ametumia mbinu ya tafsiri sisisi, sijui unayajua haya mambo mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sorry nnajifunza, kwa mfano ilo neno CV 2natumia msingi gan?
Kisawe cha CV katika kiswahili ni Wasifu, kwa hiyo hapa ametumia mbinu ya tafsiri sisisi, sijui unayajua haya mambo mkuu.
Mkuu Tunajifunza pamoja, kulingana na uelewa wangu nitasema kama ifuatavyo:Bisansaba
nimewahi kukutana na istilahi zikanitatiza. Kuna shajara na bango kitita, haya yakitumiwa na istilahi kama randama, mwisho huleta tashtiti. Nini tafsiri sisisi yako katika mtanzuko huo, tusaidie tafadhali.
Pili, unaposomwa wasifu wa marehemu una maana ni CV yake? Kwa lugha za kigeni wasifu wa marehemu ni eulogy.
Sasa tunatofautisha vipi wasifu wa marehemu na wasifu wa CV ya mtu.
Shukran sana.Mkuu Tunajifunza pamoja, kulingana na uelewa wangu nitasema kama ifuatavyo:
Shajara ni kitabu ambacho mtu anatumia kurekodi kumbukumbu zake za kila siku, kisawe chake cha kiingereza ni Diary,
Bango kitita ni gombo lenye karatasi kadhaa ambalo hutumika kufanyia uwasilishaji (Katika vikao, darasani, n.k) mara nyingi mwasilishaji hutumia maka peni kuandika katika karatasi zake (Hii ni maana ya msingi).
Randama hili huwa nalisikia sana bungeni, nadhani ni neno la kisheria, kwa kweli siwezi hata kulifafanua.
Kuhusu wasifu CV na wasifu wa marehemu, mi nadhani kitakacholeta tofauti ni Muktadha. Kimsingi dhana ni ile ile huku kwenye CV ya mtu kinachoongelewa ni sifa za mhusika kulingana na muktadha husika, na kwenye wasifu wa marehemu kinachosomwa ni sifa zake njema hata kama kuna mabaya aliyofanya hayo hayatasemwa. Umesema wasifu wa marehemu kwa kiingereza ni eulogy, sasa hii tukitafuta kisawe chake katika kiswahili ni taabini ambapo tukifanya tafsiri rejeshi ina maana hii "narration of remembrance of a deceased (usually delivered forty days after the death of the deceased)". Sasa sijui kama tunaweza kutumia taabini badala ya wasifu wa marehemu.
"gombo" ni neno la Kibiblia, lenye maana ya karatasi ya vitabu vya zamani walivyoandika Manabii
Mkuu gombo ni kitita cha makaratasi yenye ukubwa wa kutosha na huwa hukunjwa kwa kuviringishwa kurahisisha ubebaji, njia hii ilitumika zamani kuhifadhi maandishi, hasa ya kidini.
Kuhusu mtanzuko nadhani alimaanisha mtanziko ikiwa na maana kutojua cha kufanya hasa katika kufanya machaguo baina ya vitu viwili kisawe chake ni dilemma.
ubarikiwe mkuu kwa hili darsaMkuu Tunajifunza pamoja, kulingana na uelewa wangu nitasema kama ifuatavyo:
Shajara ni kitabu ambacho mtu anatumia kurekodi kumbukumbu zake za kila siku, kisawe chake cha kiingereza ni Diary,
Bango kitita ni gombo lenye karatasi kadhaa ambalo hutumika kufanyia uwasilishaji (Katika vikao, darasani, n.k) mara nyingi mwasilishaji hutumia maka peni kuandika katika karatasi zake (Hii ni maana ya msingi).
Randama hili huwa nalisikia sana bungeni, nadhani ni neno la kisheria, kwa kweli siwezi hata kulifafanua.
Kuhusu wasifu CV na wasifu wa marehemu, mi nadhani kitakacholeta tofauti ni Muktadha. Kimsingi dhana ni ile ile huku kwenye CV ya mtu kinachoongelewa ni sifa za mhusika kulingana na muktadha husika, na kwenye wasifu wa marehemu kinachosomwa ni sifa zake njema hata kama kuna mabaya aliyofanya hayo hayatasemwa. Umesema wasifu wa marehemu kwa kiingereza ni eulogy, sasa hii tukitafuta kisawe chake katika kiswahili ni taabini ambapo tukifanya tafsiri rejeshi ina maana hii "narration of remembrance of a deceased (usually delivered forty days after the death of the deceased)". Sasa sijui kama tunaweza kutumia taabini badala ya wasifu wa marehemu.
ubarikiwe mkuu kwa hili darsa
Wasifu...
Mkuu huwezi kutumia kiswahili chepesi kidogo hapo kwene red tukuelewe vizuri? Hili li lugha letu ligumu jamani dah!!
Mkuu Tunajifunza pamoja, kulingana na uelewa wangu nitasema kama ifuatavyo:
Shajara ni kitabu ambacho mtu anatumia kurekodi kumbukumbu zake za kila siku, kisawe chake cha kiingereza ni Diary,
Bango kitita ni gombo lenye karatasi kadhaa ambalo hutumika kufanyia uwasilishaji (Katika vikao, darasani, n.k) mara nyingi mwasilishaji hutumia maka peni kuandika katika karatasi zake (Hii ni maana ya msingi).
Randama hili huwa nalisikia sana bungeni, nadhani ni neno la kisheria, kwa kweli siwezi hata kulifafanua.
Kuhusu wasifu CV na wasifu wa marehemu, mi nadhani kitakacholeta tofauti ni Muktadha. Kimsingi dhana ni ile ile huku kwenye CV ya mtu kinachoongelewa ni sifa za mhusika kulingana na muktadha husika, na kwenye wasifu wa marehemu kinachosomwa ni sifa zake njema hata kama kuna mabaya aliyofanya hayo hayatasemwa. Umesema wasifu wa marehemu kwa kiingereza ni eulogy, sasa hii tukitafuta kisawe chake katika kiswahili ni taabini ambapo tukifanya tafsiri rejeshi ina maana hii "narration of remembrance of a deceased (usually delivered forty days after the death of the deceased)". Sasa sijui kama tunaweza kutumia taabini badala ya wasifu wa marehemu.
Mkuu wewe ni mwalimu wa ISIMU au??