Mambo yako ya huko US yaishie hukohuko, hivi unajua kuwa kuna watoto wa maskini waliozikosa hizo nafasi za polisi wakati wakiwa na vyeti halisi ambavyo wamevipata kwa jasho lao na nafasi zao zikichukuliwa na hao watu wanaotumia vyeti ya nephew na cousin zao?. Ni lini watoto wa hao maskini nao watapewa hizo nafasi za kufanya hizo kazi ili nao waonyeshe uwezo wao?. Kama hakuna haja ya kufwata vyeti basi tuachane na kuajiri kwa kufuata elimu, kama inavyotangazwa kwenye matangazo ya kazi. Police ni public institution, ni totauti sana na kazi zako unazofanya huko US ambazo unajiliwa kwa uzoefu wako. Comments kama hizi zinawakitisha watu kusoma shule na watu wanabaki kuamini kuwa kazi zinapatikana kwa mission town. Haya mambo mambo ya mission town na kujuana ndio yametufikisha hapa
Mkuu Jagamaster,
Labda hukunielewa kidogo, mimi sikuwa nasema watu wasisome but kuna unconvesional way za education ambazo mimi ndio nimepitia na kufanikiwa
Mimi nilimaliza Form 6 miaka ambayo kulikuwa na chuo kikuu cha Dar es salaama na Muhimbili tuu , nikapata division 3 kwenye PCM, competition ilikuwa kubwa sana kumbuka hakuna mbadala wa chuo kikuu cha dar.
Sikuchaguliwa kwenye Univercity, sikuenda Mission Town kama unavyosema watu wanafanya , nikaenda kuchukua Diploma in Computer Science, wakati huo hata chuo kikuu hawana Computer Science as a Degree, nikaajiriwa kwenye makampuni ya Serikali na Mashirika ya umma kama Developer .
Nikatumia mwanya huo kusoma vishort kozi vingi tuu, wakati napata experience, nika panda vyeo kutokana na juhudi na uwezo, nikaja Marekani nikaajiriwa kutokana na uzoefu wangu nikaendeleza kwa vi short course vingi mpaka management nikapada, nikakawa kwenye Niche market ya Data Warehouse and Business Intellingence.
Nimebuild a lot of those systems nikajifunda best tools in the business, sasa hivi hiyo technologia ndio inaingia kwa nguvu Africa na Tanzania BOT na TRA wanaprojects na wanatumia wataalamu kutoka nje hela wanazowalipa ni hakuna mfano.
Me and my team we can do they same stuff and even better for 1/4 the price, I can even be auditing kazi yao na nikafanikisha sana, but itakuwa vigumu kama huna Masters Bongo , Nilishazungumza na mmoja wa wakubwa na akakubali hilo ni tatizo kubwa sana sasa na ni vigumu kubadilisha huo mfumo.
Pia kuna wakati nilipokuja tuu nikawa na mawazo hayo ya kusoma nipeleka vyeti vyangu , wakaenda kuvievaluate pamoja na experiece wakasema mimi ni equivalent na mtu mwenye Four years univercity na nikitaka kusoma watanipa test then I go straight to Masters , huyo Prof akasema hata master utaweza kuinyanyasa sana
Watu kama sisi tuko wengi tuu na sio kwamba hatusomi ila hatujafuata mfumo unaokubalika pekee, tujifunze kwa wenzetu ndio maana wamefika mbali Singapore iliendelea hivyo hivyo , Marekani walipitia huko kwa kuangalia vyeti tuu