Mkuu sasa na sisi ambao hatuenda tuu chuo shauri chuo kilikuwa kimoja tuu sio kwamba tulifeli tumeweza kujiendeleza na tukawa na kwa "Professional Development" tunaweza kujiita "college equivalent" ?
Academic qualifications na perfomance achievement ni vitu viwili tofauti na mara nyingi hutokana na msingi wa awali.kama alivyochangia member mmoja mtu anaweza kuwa awarded kulingana na msukumo wa kiu yake lakini asijipime uwezo wake kurudi nyuma kwa elimu aliyonayo.siku za nyuma kwa mfano wanafunzi waliofaulu vema sayansi na hesabu walipelekwa shule za ufundi kama moshi tech au ifunda tech then akifaulu form four vizuri anajiunga tech college for full technician certificate miaka 3.. Baada ya ajira anaweza kurudi for advanced diploma ambayo waliiconsider equivalent na first degree lakini kiajira ni tatizo ukicompare na mtu aliyesoma secondary a level siyo ya ufundi akajoin universty kwa degree ya engineering.hawa watu wawili ukiwaweka katika mizania ya utendaji utawatambua tu..yupi ana msingi na yupi amehitimu.
eliesikia
Tena umenikumbusha vizuri sana , wakati tunachukua hiyo diploma ya Computer science , mashirika yalisponsor wafanyakazi wao kusoma wote walikua na degree, mkuu kilaza mimi kama ulivyoniita tukawa tunakula sahani moja , ikifika kwenye programming duu kilaza mimi inabidi nifukuze watu kwenye computer yangu hayo maswali, projects zilipofika kwenye finals inabidi uchague kati ya "system designing" au "programming" , duu
wakakimbilia wengi mteremko system designing , kilaza wa form 6, project yangu ikawa mfano, kuenda kazini ndio basi zikija training short training nakutanao tena wakati wa labs nakumbuka baada ya lunch , mwalimu ananitumia kuwasaidia labda mini ni wakina bills au zuku basi tuu mfumo uliniangusha
Wanaova pete na cheni mbona wengi tu. mnamkumbuka CISCO MTIRO?jama yupo smart sana ,semeni wazi kama nyie ni mapolisi au jeshi mlioaathirika kwa kugushi vyeti.Kama cheni mbona MKAPA raisi anakubwa zaidi au JOHN MALECELA WAZIRI MKUU MSTAAFU MZEE WA MVUMI
CV ya nini boss, au unataka kumpa kazi?
inasikitisha sana,,,,,hapa ndipo tatizo lilipo,,,,,,kwani haijulikani kwamba taarifa za nida ni za wazi na zitasomwa na kila mtu hata maadui,,,,,,,uzalendo wetu ni upi,, weledi wetu ni upi,,,,,,tumeshindwa kulinda identity yetu kama taifa,,,,,,wanausalama,,,jeshi kuficha taarifa zao ni kughushi,,,,,,huwezi ona tofauti ya kuficha na kughushi,,,,nadhan,,hili ni tatizo linapaswa lishughulikiwe,,,kwa,kutoa elimu,,,nakuto vi ,,,attack kisaikolojia vyombo vya usalama,,kuvidhalalisha na kuvidunisha,,,,kiujumla,,,,,,,,tujenge utmaduni wakuheshim,,na kulilinda taifa hili ni letu sote,,,,Mkuu philemon,
Maelezo yako yanajenga dhana potofu ambayo inaweza kutumika kutetea uhalifu wa kugushi kwa kivuli cha mwavuli wa usalama wa taifa.
Vitambulisho vya kitaifa ndiyo msingi wa usalama wa taifa lenyewe hivyo taarifa zinazohitajika hapo ni zile za msingi na halisi zisizochakachuliwa kwa namna yoyote ile. Haikubaliki na ni ajabu kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na uzalendo kwa nchi yake kukubaliana na dhana hii.
Utambulisho fake unaoweza kutumiwa na wanausalama kwa shughuli maalum hauna uhusiano wowote na wala hautarekodiwa katika kumbukumbu zinazohifadhiwa na mamlaka ya vitambulisho vya kitaifa!
Watanzania walio wengi wenye ufahamu wa kawaida tunajua kabisa kwamba vyeti vya kugushi vipo vingi na utamaduni huo unaendelea kwa sababu ya mawazo ya kipuuzi tu ya kutukuza vyeti katika usaili na hata kuteuwa au kupandisha vyeo wakati wenye vyeti hivyo hawana kitu kichwani. Hali hii ina uhusiano wa moja kwa moja na umasikini wa kitaifa unaotokana na maamuzi ya kijinga.
Ili tuendelee lazima tuwe wakweli, tusahihishe makosa yaliyofanyika kwa njia za busara badala ya kutafuta visingizio vya kijingajinga tu kuhalalisha upuuzi!
alikuwa chakula!
Mkuu Jagamaster,
Labda hukunielewa kidogo, mimi sikuwa nasema watu wasisome but kuna unconvesional way za education ambazo mimi ndio nimepitia na kufanikiwa
Mimi nilimaliza Form 6 miaka ambayo kulikuwa na chuo kikuu cha Dar es salaama na Muhimbili tuu , nikapata division 3 kwenye PCM, competition ilikuwa kubwa sana kumbuka hakuna mbadala wa chuo kikuu cha dar.
Sikuchaguliwa kwenye Univercity, sikuenda Mission Town kama unavyosema watu wanafanya , nikaenda kuchukua Diploma in Computer Science, wakati huo hata chuo kikuu hawana Computer Science as a Degree, nikaajiriwa kwenye makampuni ya Serikali na Mashirika ya umma kama Developer .
Nikatumia mwanya huo kusoma vishort kozi vingi tuu, wakati napata experience, nika panda vyeo kutokana na juhudi na uwezo, nikaja Marekani nikaajiriwa kutokana na uzoefu wangu nikaendeleza kwa vi short course vingi mpaka management nikapada, nikakawa kwenye Niche market ya Data Warehouse and Business Intellingence.
Nimebuild a lot of those systems nikajifunda best tools in the business, sasa hivi hiyo technologia ndio inaingia kwa nguvu Africa na Tanzania BOT na TRA wanaprojects na wanatumia wataalamu kutoka nje hela wanazowalipa ni hakuna mfano.
Me and my team we can do they same stuff and even better for 1/4 the price, I can even be auditing kazi yao na nikafanikisha sana, but itakuwa vigumu kama huna Masters Bongo , Nilishazungumza na mmoja wa wakubwa na akakubali hilo ni tatizo kubwa sana sasa na ni vigumu kubadilisha huo mfumo.
Pia kuna wakati nilipokuja tuu nikawa na mawazo hayo ya kusoma nipeleka vyeti vyangu , wakaenda kuvievaluate pamoja na experiece wakasema mimi ni equivalent na mtu mwenye Four years univercity na nikitaka kusoma watanipa test then I go straight to Masters , huyo Prof akasema hata master utaweza kuinyanyasa sana
Watu kama sisi tuko wengi tuu na sio kwamba hatusomi ila hatujafuata mfumo unaokubalika pekee, tujifunze kwa wenzetu ndio maana wamefika mbali Singapore iliendelea hivyo hivyo , Marekani walipitia huko kwa kuangalia vyeti tuu
..ngoja tumuulize babaye Riz-1 lazima atajua tu kilichomsukuma kumuweka yule bwana pale!!...Subirini atakuja tu!!Mkuuu tafuta degree please.....
Post kubwa kama huyo Maimu lazma uwe na elimu kubwa, hakuna longolongo hapo..... Hata hapo USA mtu kama Paneta ni shule kubwa, Prof...zz
Hivi ugomv wa wasio na elimu na wenye elimu utaisha lini?? Haaaaaaaa
Kwa kuwa una experience ya kutosha nakushauri usome upate degree then masters n'k, Hiyo diploma haitoshi, usidhani kuwa vyeti siyo muhimu exeprience ndiyo muhimu. Ukiwa umesoma vizuri yaani una vyeti stahiki kwa elimu, muda mfupi ukiingia kazini unapata exerience na kuchapa kazi vizuri. Kwa hiyo vyeti kwanza then experience.
Watanzania na Waafrika tuachane na kasumba ya kufikiri vyeti vingi vya kubandika ukutani ndivyo vinavyofanya kazi bila kuangaliwa uwezo wa mtu. Si kila aliyesoma ameelimika, na si kila aliyeelimika ana uwezo wa kuongoza. Kuongoza ni bongo la mtu. Mababu zetu walikuwa machifu wakubwa ambao hawakujua kusoma na kuandika, lakini waliweza kufanya organization nzuri na hata kupigana na wakoloni na kuwashinda, CV zao na bongo lao na uwezo wao.
Kasumba hii ndiyo inayoturudisha nyuma kimaendelea kwa kufikira kusoma ndiko kuendelea. Wenye kujua zaidi siku hizi wanasomelea kile anachotaka kufanyia kazi kwani wengi wanasoma bila malengo ili mradi awe na sifa ya kwamba amemaliza chuo kikuu au phd na kuishia kutangatanga bila kazi, nini tatizo kusoma bila malengo.
Nimeshuhudia nchi za ulaya na Marekani wengine huchukua mafunzo ya muda mfupi (short course) na baada ya hapa huajiriwa moja kwa moja kwa vile wamechukulia mafunzo katika taaluma inayohotajika kazini na mara wanaanza kutia pesa mfukoni mwao. Lakini wale wanaohitimu vyo vikuu wengi wanahangaika kupata kazi kwani elimu yao ni ya jumla jumla ambayo makampuni yakiwaajiri inabidi yaanze kuwafunza kazi tofauti na aliyechukua kozi mfupi maalum kwa ajili ya kazi hiyo. Ingawa kuna baadhi ya kazi zinahitaji kiwango fulani cha degree, lakini si hoja ya kuashiria uwezo wa kuongoza katika madara.
Tuachane na ukiritimba wa kufikira CV ndizo zinafanya kazi kumbe ni kasumba tu ya Watanzania na Waafrika.
Nilishajaribu walikuja Diaspora duu wanakwambia wanataka masters, huyo Dickson Maimu mwenyewe wanaojaribu kumsema huku alikua Treasury enzi hizo eighties , Mainframe Developer unacheza na Dump Terminals tuu, command line tuu hakuna GUI kama siku hizi ukitaka hata kusave file unaandika sentensi nzima ya Code, one of Smart guys ameandika systems nyingi tuu ndio hako ka vitambulisho, he can manage na kama ni kushika spanner kwenye Editor anaweza vilevile hamdanganyi mtu
Kwa kuwa una experience ya kutosha nakushauri usome upate degree then masters n'k, Hiyo diploma haitoshi, usidhani kuwa vyeti siyo muhimu exeprience ndiyo muhimu. Ukiwa umesoma vizuri yaani una vyeti stahiki kwa elimu, muda mfupi ukiingia kazini unapata exerience na kuchapa kazi vizuri. Kwa hiyo vyeti kwanza then experience.