CV ya Dickson Maimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Niko mkuu Marekani sasa si unajua tena usipokua na degree hata uwe wapi hakipandi ? Ndio maana naandika kiswahili mkuu sasa na niko miaka kama kumi na tano bosi
 
Mkuu sasa na sisi ambao hatuenda tuu chuo shauri chuo kilikuwa kimoja tuu sio kwamba tulifeli tumeweza kujiendeleza na tukawa na kwa "Professional Development" tunaweza kujiita "college equivalent" ?

Kaka mwanzoni ulisema ulifeli div 3 ndio maana ulikosa chuo.. Waxungu wakiona mtu kafaulu level yake wanaamini ya juu ataweza pia lakini ukishindwa level yako basi watajua tuu ww kilaza. Afu baaasi. Zuka na Bills walifanya kweli kwenye SAT ndio maana walienda Havard. Simply they ar so capable... Ndugu jitahidi usome hata hivyo vyeti unavyopigia chapuo. Kimsingi kukosa kazi sio mwanzo au mwisho wa maisha lakini kusoma ni lazima
 
@ eliesikia

Mimi sikusema nimefeli form 6 ila sikuchaguliwa tu kwenda mlimani, kuna watoto wa wakubwa walipata division four na wakafanya mipango wakaenda chuo kikuu na walifaulu vizuri tuu na mmoja alikua rafiki yangu , hivyo huo mfumo wa kumpima mtu kwa masaa matatu ya mtihani haukuwa mzuri, narudia sihitaji hiyo degree kabisa ila nimekuuliza ukiniita college equivalent utakua umenipendelea ?
 
eliesikia

Tena umenikumbusha vizuri sana , wakati tunachukua hiyo diploma ya Computer science , mashirika yalisponsor wafanyakazi wao kusoma wote walikua na degree, mkuu kilaza mimi kama ulivyoniita tukawa tunakula sahani moja , ikifika kwenye programming duu kilaza mimi inabidi nifukuze watu kwenye computer yangu hayo maswali, projects zilipofika kwenye finals inabidi uchague kati ya "system designing" au "programming" , duu
wakakimbilia wengi mteremko system designing , kilaza wa form 6, project yangu ikawa mfano, kuenda kazini ndio basi zikija training short training nakutanao tena wakati wa labs nakumbuka baada ya lunch , mwalimu ananitumia kuwasaidia labda mini ni wakina bills au zuku basi tuu mfumo uliniangusha
 
Last edited by a moderator:

Well said Inkoskaz@, tunahitaji vijana wenye uelewa mkubwa na upambanuzi kama wako. Anayesoma kwa kuunga vipande vipande anakuwa na uelewa mkubwa, kwani kila akishafanya kazi anaona mapungufu ya utendaji wake, hapo anaenda kujazia. Mwenye kujengeka kwa utaratibu huo ni mzuri sana, kwani amejitahidi kupitia hatua muhimu kuruka vihunzi na kusawazisha mabonde. Hana shinda kurudia chini kuchukua alichokikosa.

Waliokwenda mfululizo hadi elimu ya juu hujisikia kama ni kujidhalilisha kurudia kozi ndogo za certificate, ingawa anaona inahitajika na ni muhimu kwake. Hapo ndipo tunapohitaji kubadilika.
 


Wanirudisha nyuma yakhe, kwani hata mie nilipokuwa chuoni huko mwaka wa kwanza tu, tena semester ya kwanza tu mmoja wa classmates wangu aliponiona nawaacha mbali mno katika masuala ya computer, akaenda kuongea na mume wake. Kumbe mtoto wao alikuwa anahitimu highschool, na walikuwa wameshakusanya mambo mbalimbali kutengeneza kitabu cha wahitimu. Wakaniomba niwafanyie kazi hiyo. Nilishangaa kidogo wazungu waniombe wakati natoka Afrika.

Nikakubali kwa kuwa nilikuwa na uzoefu wa publishing niliyofanya Tanzania ingawa nilizoea zaidi Apple computer, basi design ya kitabu kwa ufundi wangu wote waliniita nime mmoja wa wageni pale shuleni siku ya graduation. Baada ya muda nilimiminiwa maombi ya kujiunga na publishing ya vitabu vya shule. Nilichokubali ni kufanya kazi kwenye gazeti kubwa kwa vile lilikuwa na benefits ninazotaka.

Nilipoanza kazi huko nilikutana na wahitimu wa Master na wenye PHD, lakini hawakufua dafu na wakawa wananiomba niwafundishe uzoefu wangu ingawa wakati huo sikufikia kiwango cha degree, ni kozi za kuungaunga hapa Tanzania, lakini Marekani ilikuwa chanda cha dhahabu. Hapo ndipo nilipopata ufahamu zaidi kuwa elimu ya chuo kikuu ni ya jumla jumla tu, mie niliyekuwa na uzoefu wa kazi kufundishwa kazini Tanzania na vikozi vidogo vika na dhamani ya kupata kazi bila kuchakaza kandambili.

Kwa vyo vyote elimu ya vyuo vikuu inampanua mtu kiakili, kujiamini na kufanya uchambuzi hakikishi, lakini si dhana ya kujihakikishia utendaji, kwani ni elimu ya nadharia zaidi kuliko vitendo. Ndio maana elimu ya vyuo vikuu zaidi ni maishano ya hoja hasa kiwango cha graduate.

 
Candid Scope

Umesema sawa , sijui kwanini wanafikiria nawaambia watu wasisome I don't know wanaipata wapi hiyo, mimi nilikua tuu nataka kufafanua kwamba utendaji sio lazima upitie conventional way ya education , mimi Maimu mwenyewe hatufahamiani sijui kama ana degree au hana ila nilikua namsikia alivyokua hazina kwenye payroll system ya serikali , wakti huo payroll karibu serikali yote zinatoka huko, kama mmoja alivyosema ka integrate system hizo, hao ndio walikua kaka zetu wamrtutangulia kwenye kazi na alikua na sifa nzuri sana ya kazi, hata niliposikia kachaguliwa NIDA nikajua kwa uzoefu wake atafanikiwa , sikujua hata alikwenda Vizazi na Vifo na kufanya kazi nzuri nazungumzia 89 kama sikosei alikua hazina na sijui hapo alikua ashakaa miaka mingapi , hapo kwa hesabu za karibu ana experience ya zaidi ya miaka 20
 
Last edited by a moderator:
jama yupo smart sana ,semeni wazi kama nyie ni mapolisi au jeshi mlioaathirika kwa kugushi vyeti.Kama cheni mbona MKAPA raisi anakubwa zaidi au JOHN MALECELA WAZIRI MKUU MSTAAFU MZEE WA MVUMI
Wanaova pete na cheni mbona wengi tu. mnamkumbuka CISCO MTIRO?
 
CV ya nini boss, au unataka kumpa kazi?

MTOA HOJA ANA HOJA YA MUHIMU SANA..ingekua huyu bwana anafanya mradi ambao ni privately funded, then hamna haja ya kujua elimu au hata ueledi wake, BUT huu ni mradi wa serikali na unatumia pesa za walipa kodi wa TANZANIA hivyo ni HAKI ya kila mtanzania kujua uwezo wa watendaji wake hasa mkurugenzi, Elimu inaweza kuwa si kipimo kizuri cha utendaji lakini ni INDICATOR muhimu sana. Kwa iyo kwa faida ya walipa kodi na wanyonge wa tazania ambao wamechoka ufujwaji wa pesa katika miradi ya namna hii MWENYE CV ya huyu bwana AIWEKE.

Msukumo wa kuufuatilia huu mradi unatokana na mambo mengi sana hasa ukizingatia kuwa tuna matatizo mengi sana ya muhimu ambayo tungeweza kuyashughulikia kwanza kwa izo Billion 230 za huu mradi then vitambilisho vikafuata hata mwaka 2050 kwa sababu wote tunatambua kuwa watoto kusomea chini ni janga, shule kukosa vyoo ni janga, wakinamama kujifungulia nyumbani ni janga,upungufu wa madawa hospitali ni janga, na katiba mbovu ni janga..JE KUTOKUWA NA VITAMBULISHO NI NJANGA?????????? INAUA??? ukishajiuliza hayo then utajua kwanini tunataka CV ya huyu bwana
.
 
Maimu alichokosea ni kulisemea jeshi lakini ukifanywa uuuchunguzi huru aibu itakuwa kubwa ,achilia mbali maneno ya vitisho kama usalama wa taifa, military intelligence, na hofu za kujengwa kwenye thread hii
 
inasikitisha sana,,,,,hapa ndipo tatizo lilipo,,,,,,kwani haijulikani kwamba taarifa za nida ni za wazi na zitasomwa na kila mtu hata maadui,,,,,,,uzalendo wetu ni upi,, weledi wetu ni upi,,,,,,tumeshindwa kulinda identity yetu kama taifa,,,,,,wanausalama,,,jeshi kuficha taarifa zao ni kughushi,,,,,,huwezi ona tofauti ya kuficha na kughushi,,,,nadhan,,hili ni tatizo linapaswa lishughulikiwe,,,kwa,kutoa elimu,,,nakuto vi ,,,attack kisaikolojia vyombo vya usalama,,kuvidhalalisha na kuvidunisha,,,,kiujumla,,,,,,,,tujenge utmaduni wakuheshim,,na kulilinda taifa hili ni letu sote,,,,
 

Kwa kuwa una experience ya kutosha nakushauri usome upate degree then masters n'k, Hiyo diploma haitoshi, usidhani kuwa vyeti siyo muhimu exeprience ndiyo muhimu. Ukiwa umesoma vizuri yaani una vyeti stahiki kwa elimu, muda mfupi ukiingia kazini unapata exerience na kuchapa kazi vizuri. Kwa hiyo vyeti kwanza then experience.
 
Mkuuu tafuta degree please.....


Post kubwa kama huyo Maimu lazma uwe na elimu kubwa, hakuna longolongo hapo..... Hata hapo USA mtu kama Paneta ni shule kubwa, Prof...zz

Hivi ugomv wa wasio na elimu na wenye elimu utaisha lini?? Haaaaaaaa
..ngoja tumuulize babaye Riz-1 lazima atajua tu kilichomsukuma kumuweka yule bwana pale!!...Subirini atakuja tu!!
 
we unashangaa...,sio huyo tuu na malima jee umemsahau...?kila kidole petee....halaf bado hotelini aliibiwa za dhahabu ..ndo mwaziri wetu huyoo,,,,!
 

Nakushukuru kwa ushauri , ninavyo vyeti vyakunitosha tuu sihitaji hiyo degree nimepitia njia nyingine kupata elimu yangu na kwa sasa sifanyi kazi ya kuajiriwa tena ila nilikua tuu naeleza hayo Mawazo mgando kwamba lazima uwe nayo ili uwe na ufanisi sio kweli
 

Naanza kupata wasi siku hizi...yaani mtu akiulizwa CV inaanza story hoo mara ohoo.. nini bana !
Kwani cv nini kwa kiswahili....Si ni wasifu/ historia ya maisha ya mtu.
So hata yule ambaye hajasoma ana cv yake. mfanao

Jina lake kamili/ Mwaka alikozaziliwa/ Mahali alikozaliwa/ Shule aliyosoma-Primary nk
Sehemu alizofanyia kazi..

Sasa wapi na wapi...wekeni cv yake kama inajulikana acha chenga chenga.. kama ni cheo cha kupeana pasi ijulikane vvile vile.


Sawa sawa wajameni .......

Hya leta cv ya Dickson Mwaimu.. msihofu
 

Well said mkuu, hila hapo kwenye red nadhani umeghafilika kidogo - kama kuna GUI kuna haja gani tena ya kuandika CODE ya kusave file kwa kutumia CLI? One more thing, hivi kwenye 1980s Treasury ilikuwa na Mainframe au Minicomputer - 'am just curious! Thanks.
 

Ni kweli mkuu asikudanganye mtu, vyeti kama siyo vya kugushi ni vya muhimu sana, mtu kama amesoma vizuri ni rahisi sana kukabiriana na changa moto za kila sampuli ukiwa kazini hata kama huna handon experience katika nyanja husika, itakuchukua muda mfupi kujipanga na kukabiliana na kila kitu kwa kujiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…