CV za Mawaziri wa Afya kutoka nchi baadhi za Afrika

CV za Mawaziri wa Afya kutoka nchi baadhi za Afrika

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Habari gani wana jamvi, leo nimekaa nikawa napitia baraza la mawaziri pamoja na sifa za wateule hao katika sekta mbalimbali kisha nikakutana na document moja hivi ikizungumzia mawaziri wa Afya nchi mbalimbali Africa. Nilipomaliza kuisoma hiyo document kwanza nikajiuliza, ni nani aliyeandaa doc hiyo na nini kilimpelekea kuiandaa🤔? (Ukiwa na D mbili utaelewa kwanini nilijiuliza hivi)

IMG_6513.jpeg

IMG_6514.jpeg
IMG_6515.jpeg

IMG_6516.jpeg

Baada ya kupitia doc hii nikakumbuka ule uzi wa ‘ CV YA Jenista Mhagama Naibu Waziri wa Elimu 2014-2015' hapo ndo nikachoka kabisa na kujiuliza swali la mada tajwa hapo juu, “Ni vigezo gani vinatumika kuteua mawaziri katika sekta mbalimbali hapa Tanzania🤔?”

Nilijiuliza hivyo kwasababu, katika mazingira ya sasa, ambapo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya kama vile magonjwa ya kuambukiza, upungufu wa lishe, na huduma duni za afya, uteuzi wa viongozi wa sekta ya afya ni jambo lenye umuhimu mkubwa.

Kama tulivyoona hapo juu katika hizo picha, katika nchi nyingi za jirani viongozi wa sekta ya afya wanateuliwa kwa kuzingatia sifa na uzoefu wao wa kitaaluma. Kwa mfano, nchini Kenya, Waziri wa Afya, Dkt. Debra Mulongo Barasa, ana shahada ya udaktari wa Tiba ya Ndani na Magonjwa ya Kuambukiza, pamoja na uzoefu wa zaidi ya miaka 18 katika taaluma ya afya. Dkt. Mulongo amefanya kazi na mashirika ya kimataifa kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO), akitoa msaada wa kiufundi na kuongoza utekelezaji wa mipango ya afya katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Aidha, Rwanda ina Waziri wa Afya, Dkt. Sabin Nsanzimana, ambaye ana PhD katika Epidemiolojia na uzoefu mkubwa katika utafiti wa afya ya umma na mpango wa kupambana na VVU/UKIMWI. Dkt. Nsanzimana amekuwa mhusika mkuu katika kubuni na kutekeleza mikakati ya kiafya nchini Rwanda, ikiwa ni pamoja na kusimamia juhudi za kudhibiti janga la COVID-19.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Afya wa Tanzania, Jenista Joackim Mhagama, hana sifa za kitaaluma katika afya, jambo ambalo limenifanya nijiulize kuhusu vigezo vilivyotumika katika uteuzi wake. Wakati tunaweza kupongeza uzoefu wake katika nyanja nyingine za uongozi wa umma, ni muhimu kutathmini ikiwa nafasi ya uongozi katika sekta ya afya inahitaji mtu mwenye ujuzi maalum na uzoefu wa kitaaluma ili kuhakikisha mafanikio na maendeleo endelevu.

Tutakumbuka ni jana tu, ambapo hata humu kuna mdau alihoji juu ya uwezo wa Waziri huyu katika sekta hii muhimu kupitia uzi wa ‘Hotuba ya Jenista Mhagama wakati wa mkutano wa WHO Africa huko Brazaville‘. Ni kweli inawezekana ni kiongozi mzuri lakini si kwa sekta muhimu kama hii. (Video👇🏼)

View: https://youtu.be/_UUqj0rB8Uc?si=z5wqiJYMg4x-h4Qr

Kwa mantiki hii, ni wakati mwafaka kwa Watanzania kufikiria umuhimu wa sifa na uzoefu wa kitaaluma katika nafasi nyeti za uongozi. Je, tunapaswa kuboresha mifumo yetu ya uteuzi ili kuhakikisha kuwa viongozi wetu wana uwezo wa kutatua changamoto zinazokabili sekta ya afya? Ni muhimu kwa taifa letu kusonga mbele na kuhakikisha kuwa tunateua viongozi wenye ujuzi na uwezo wa kuboresha huduma za afya kwa Watanzania wote.

Nadhani JF na majukwaa mengine ya mijadala yanaweza kuwa sehemu nzuri ya kuendeleza mijadala muhimu kwa mustakabali wa sekta ya afya na nyinginezo nchini Tanzania.

PIA SOMA: ‘Sekta ya Afya Siyo ya Kufanyia Mchezo na Mzaha.’

Mi napita zangu ….. 🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿
 
Unayatambua majukumu ya waziri katika wizara husika?
 
Leo meiona kwenye zoezi la kuvesha nishani wanajeshi baadhi hizo education background zao ni mungu tu ndo anajua. Kwa wenzetu ukigusa background education ya colonel unaweza kimbia vivo hvyo kwetu stanza waziri hana utaalamu wa wizara husika lazima awe mapambio hata jambo liwe serious ataleta utani.
 
Kuna namna hii nchi hatupo serious kabisa🤦🏽‍♂️​
 
Leo meiona kwenye zoezi la kuvesha nishani wanajeshi baadhi hizo education background zao ni mungu tu ndo anajua. Kwa wenzetu ukigusa background education ya colonel unaweza kimbia vivo hvyo kwetu stanza waziri hana utaalamu wa wizara husika lazima awe mapambio hata jambo liwe serious ataleta utani.
😂 Yn mbele ya rais ety CV ya mtu inasomwa ety alianza shule ya msingi mwaka blaah blaah kisha akajiunga sekondari blaah blaah kisha blaah blaab 😂
 
Swali zuri sana hili, Kisima anataka kusema kuwa ni sawa kuwa na waziri wa Afya ambaye hana historia wala background yeyote inayohusiana na masuala ha afya🥲 (Health career background = non)
H nchi tunachezewa sana, kisa kujuana ndio wanapeana vyeo.
 
😂 Yn mbele ya rais ety CV ya mtu inasomwa ety alianza shule ya msingi mwaka blaah blaah kisha akajiunga sekondari blaah blaah kisha blaah blaab 😂
Haki mecheka kuna Cv ilisoma pale nkasikia shule msingi mara sekondari mara sekondari mara paaap quba mara srilannka nkabaki kusema bado safari yetu ndefu mnoooo gusa background eductaion ya mkuu wa majeshi wa marekani unaweza lala na viatu. Sio kosa lao ndo mana wanasiasa enzi zile walikua wakiwatuma kufagisa nilikua nawamaind sana kwa ule ujinga nshukuru hayajajitokeza enzi za mama. Viongozi wetu hawa wengi likija suala la elimu yao vigugumizi vingi mnoo na hao ndo wakwanza kuwatuhumu wenzao kwamba hawana akili.
 
Mm sijui Kingereza vzr, ila kuna video flan hv ya Profesa Ndalichako anaongea english 🙌 ile video kiboko aisee 😂
 
Back
Top Bottom