Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
- Thread starter
- #21
Ni maamuzi yake mteuzi, mwache afanye kazi yake
Hatukati, bali ni vyema akiifanya kwa utashi zaidi na kwa maslahi mapana ya umma🫡
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni maamuzi yake mteuzi, mwache afanye kazi yake
Ukiwa na marais wabovu wateule wao wanakuwa wabovu zaidi.Habari gani wana jamvi, leo nimekaa nikawa napitia baraza la mawaziri pamoja na sifa za wateule hao katika sekta mbalimbali kisha nikakutana na document moja hivi ikizungumzia mawaziri wa Afya nchi mbalimbali Africa. Nilipomaliza kuisoma hiyo document kwanza nikajiuliza, ni nani aliyeandaa doc hiyo na nini kilimpelekea kuiandaa🤔? (Ukiwa na D mbili utaelewa kwanini nilijiuliza hivi)View attachment 3082328
View attachment 3082326
View attachment 3082327
View attachment 3082329
Baada ya kupitia doc hii nikakumbuka ule uzi wa ‘ CV YA Jenista Mhagama Naibu Waziri wa Elimu 2014-2015' hapo ndo nikachoka kabisa na kujiuliza swali la mada tajwa hapo juu, “Ni vigezo gani vinatumika kuteua mawaziri katika sekta mbalimbali hapa Tanzania🤔?”
Nilijiuliza hivyo kwasababu, katika mazingira ya sasa, ambapo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya kama vile magonjwa ya kuambukiza, upungufu wa lishe, na huduma duni za afya, uteuzi wa viongozi wa sekta ya afya ni jambo lenye umuhimu mkubwa.
Kama tulivyoona hapo juu katika hizo picha, katika nchi nyingi za jirani viongozi wa sekta ya afya wanateuliwa kwa kuzingatia sifa na uzoefu wao wa kitaaluma. Kwa mfano, nchini Kenya, Waziri wa Afya, Dkt. Debra Mulongo Barasa, ana shahada ya udaktari wa Tiba ya Ndani na Magonjwa ya Kuambukiza, pamoja na uzoefu wa zaidi ya miaka 18 katika taaluma ya afya. Dkt. Mulongo amefanya kazi na mashirika ya kimataifa kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO), akitoa msaada wa kiufundi na kuongoza utekelezaji wa mipango ya afya katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Aidha, Rwanda ina Waziri wa Afya, Dkt. Sabin Nsanzimana, ambaye ana PhD katika Epidemiolojia na uzoefu mkubwa katika utafiti wa afya ya umma na mpango wa kupambana na VVU/UKIMWI. Dkt. Nsanzimana amekuwa mhusika mkuu katika kubuni na kutekeleza mikakati ya kiafya nchini Rwanda, ikiwa ni pamoja na kusimamia juhudi za kudhibiti janga la COVID-19.
Kwa upande mwingine, Waziri wa Afya wa Tanzania, Jenista Joackim Mhagama, hana sifa za kitaaluma katika afya, jambo ambalo limenifanya nijiulize kuhusu vigezo vilivyotumika katika uteuzi wake. Wakati tunaweza kupongeza uzoefu wake katika nyanja nyingine za uongozi wa umma, ni muhimu kutathmini ikiwa nafasi ya uongozi katika sekta ya afya inahitaji mtu mwenye ujuzi maalum na uzoefu wa kitaaluma ili kuhakikisha mafanikio na maendeleo endelevu.
Tutakumbuka ni jana tu, ambapo hata humu kuna mdau alihoji juu ya uwezo wa Waziri huyu katika sekta hii muhimu kupitia uzi wa ‘Hotuba ya Jenista Mhagama wakati wa mkutano wa WHO Africa huko Brazaville‘. Ni kweli inawezekana ni kiongozi mzuri lakini si kwa sekta muhimu kama hii.
Kwa mantiki hii, ni wakati mwafaka kwa Watanzania kufikiria umuhimu wa sifa na uzoefu wa kitaaluma katika nafasi nyeti za uongozi. Je, tunapaswa kuboresha mifumo yetu ya uteuzi ili kuhakikisha kuwa viongozi wetu wana uwezo wa kutatua changamoto zinazokabili sekta ya afya? Ni muhimu kwa taifa letu kusonga mbele na kuhakikisha kuwa tunateua viongozi wenye ujuzi na uwezo wa kuboresha huduma za afya kwa Watanzania wote.
Nadhani JF na majukwaa mengine ya mijadala yanaweza kuwa sehemu nzuri ya kuendeleza mijadala muhimu kwa mustakabali wa sekta ya afya na nyinginezo nchini Tanzania.
PIA SOMA: ‘Sekta ya Afya Siyo ya Kufanyia Mchezo na Mzaha.’
Mi napita zangu ….. 🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿
Inatafakarisha sanaa aiseeKujua kusoma na kuandika
Kuwa mwana CCM.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aisee ngoja niibandike hapaSasa kwanini uzi wa hotuba ya Waziri huko Brazaville umekuwa blocked hatuwezi kufungua?
Acheni mambo yenu JF.
Nadhani kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya sheria zetu ili ifike wakati sasa na sisi tuwe tunawafanyia vetting hawa mawaziri wetu.
The likes of akina Dr. Ngugulile tunawaacha au kuwaweka pembeni hadi wanapata kazi WHO huku sisi thamani zao tunazibeza.