CWT mnaomvimbia kichwa Rais jifunzeni unyenyekevu wa Shaka Hamdu Shaka mtafika mbali vyeo ni dhamana ya muda Tu

Miccm inacharuana, safi sana.
 
Sio kila mtu ana shida kama huyo Shaka. Kwanza hii tabia ya wazanzibari kupata madaraka huku, wakati Wabara hawakubaliwi Zanzibar bado tunawacheck sana.
Mkuu unafahamu lakini makubaliano ya Muungano?
 
Mlipoiondoa JKT ya kila kijana kwenda mlikuwa mnazalisha haya makasiriko.

Uzalendo haupimwi kwa teuzi bali mfumo wa makuzi kijamii
 
Ww ndio unafahamu makubaliano ya ule uhuni. Wajinga ndio waliwao.
Ingawa napinga uhuni wa CCM lakini naheshimu Muungano wetu

Kama kuna issues zizungumzwe yajengwe tuishi kama ndugu
 
Hebu tujifunze kuchagua maneno na pia na namna bora ya kuyatumia. Kutumia maneno kama "kumvimbia kichwa, kukataa, kususia" na mengine kama hayo ni kutokuwatendea haki wahusika. Nafikiri maneno yaliyopaswa kutumika ni kuwa "hawakuridhia ama hawakuwa na utayari katika kukasimiwa majukumu hayo"

Ni dhahiri hao ni watu wenye maadili mema mpaka kuweza kufikiliwa kuwa wanafaa katika teuzi hizo za ukuu wa wilaya. Pengine wana hoja nzito kuhusu mgongano wa maslahi kwa nafasi za uongozi wanazozishikilia kwa sasa, hali iliyopelea kushindwa kuwa na utayari.

Si jambo la maana kuanza kuwahukumu kwa utovu wa nidhamu hadharani wakati hutujui chochote kuhusu maudhui ya majibu yao kuhusiana na kukosa kwao utayari.

Na hilo ni jambo la faragha kati yao na mamlaka yao ya uteuzi. Hivi unatambua sababu iliyopelekea maDC wengine kutumbuliwa, pengine wanajihisi hawana uwezo kwa majukumu waliyopewa na mamlaka yao uteuzi.

Pengine kazi wanazofanya kwa sasa zina marupurupu kwa kulinganisha na nafasi za uDC, pengine wengine ni kwa kutaka tu 'peace of mind", pengine ni kwa sababu ya "security of tenure", pengine ni kwa sababu ya "organization citizenship" pengine zinaweza zikawa nyingi, lakini majibu yao ya kukosa utayari ndiyo ni jambo la msingi kulitambua.
 
Ingawa napinga uhuni wa CCM lakini naheshimu Muungano wetu

Kama kuna issues zizungumzwe yajengwe tuishi kama ndugu
Sahihi kabisa, Sisi Leo ni Ndg, lazima tuuheshimu na kuuthamini Muungano wetu
 
Ingawa napinga uhuni wa CCM lakini naheshimu Muungano wetu

Kama kuna issues zizungumzwe yajengwe tuishi kama ndugu

Mkuu una haki ya kuheshimu chochote ikiwemo huo muungano maana ni haki yako. Lakini kero ambazo hazitatuliwi miaka dahari, ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
Mkuu una haki ya kuheshimu chochote ikiwemo huo muungano maana ni haki yako. Lakini kero ambazo hazitatuliwi miaka dahari, ni utapeli kama utapeli mwingine.
Faida za Muungano ni kubwa kuliko huo ujinga unaowaza kiongozi
 
Kwa mara yakwanza kaliba ya ualimu imeonesha uthubutu na kujitambua
 
Sio marupurupu pengine wanajambo na wameibana sehemu serikali
 
Kiufupi wamefanya kosa la uhaini yaani wamemdhalilisha na kumhujumu mkuu wa nchi. Haina tofauti na kushiriki kuipindua serikali halali
 
Mimi hapo ndio nimewashangaa; bado wapo kwenye system halafu wanaikataa system!!. Kwakweli hawakushauriana vizuri na naamini yupo aliyeburuzwa na mwenzie.Yaani nadhani watajua hawajui
 
Sio kila mtu anaishi kwa kujipendekeza kama shaka na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…