UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,753
- 12,932
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!
Kila mwaka kumekuwa na madai ya walimu kuchangia katika michango mbalimbali ya shughuli za kiserikali kwa ushurutishwaji hasa na wakurugenzi wa Halamashauri ama manaibu wakurugenzi.
Moja wapo ya kilio cha muda mrefu kwa walimu ni hii kero ya Michango ya mbio za Mwenge kila mwaka.
Sasa kuna barua ambayo inasambaa mitandaoni kutokea huko Halmashauri ya mji wa Ifakara ikionekana kuwataka walimu kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya mbio za mwenge wa mwaka huu 2023,ambapo imesema kila mwalimu mkuu atachangia elfu 50,000/= na walimu wa kawaida itawapasa kuchangia elfu 5000/=.
Kibaya zaidi ukigoma kuchangia michango hiyo unaambiwa hutapewa vipaumbele kama hutapewa fursa ya miradi ya serikali inayowahusu walimu n.k, na kama mkurugenzi hajaridhishwa na adhabu hizo utaambiwa uandike barua ya kujieleza kwanini umegoma kuchangia maendeleo na utawekwa kwenye list ya walimu wanaopaswa kukomolewa,ni eidha utimuliwe kwasababu lukuki au uhamishiwe vijijini huko ndani ndani ili ukaipate fresh.
Huu ni uonevu mkubwa ambao kila mwenye akili timamu anapaswa kuupigia kelele kwa nguvu zote.
Wakati ambao watu wenye akili timamu tunapinga huu uonevu kuna Shirikisho la Umoja wa Walimu Tanzania almaarufu kama CWT ambao wao ndiyo wenye mamlaka ya kulipigia kelele suala hili.
Miaka yote Chama hiki cha Walimu kimeendelea kukaa kimya pale ambapo walimu wamekuwa wakionewa na serikali,Chama hiki huwa kinaibuka wakati kikiwa na migogoro ya kimaslahi hasa kipindi cha Uchaguzi wa ndani wa Chama wa kuwachagua viongozi, lakini tofauti na hapo hakina msaada kwa walimu zaidi ya kuisaidia serikali kutimiza malengo yake ya kuendelea kubaki madarakani.
Hivi Viongozi wa CWT mnaakili timamu kweli? Ni lini mtawapambania walimu waondokane na huu udharimu?,Hili suala halipo kisheria na ndiyo maana walimu wanalipigia kelele kila siku lakini nyie mmeendelea kupiga kimya huku mkipokea mafungu kutoka serikalini mkishibisha matumbo yenu na kujaza matako ili kila mpitapo basi watu wageuke kuwatazama mlivyoshiba pesa za dhulma!.
Walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu na bado mshahara ni mdogo lakini hapo hapo kwenye hako ka Mshahara na serikali pia bado inaendelea kuwakamua kila uchwao.
Hivi huo mwenge unafaida gani? Kama kitu kinaendelea kula pesa na Kodi za watanzania pasipo kuingiza pesa kina faida gani? Huo mwenge kwanini usiwekwe makumbusho uenda ukaliingizia taifa fedha kuliko hivi sasa kutumia fedha na gharama kubwa?
Hakuna mtu mwenye akili timamu leo ukamuuliza huo mwenge una faida gani akakujibu,labda awe mwendawazimu!
Nyie CHAMA CHA WALIMU ni MATAPELI mnaokula jasho la walimu na kuwanyonya!.
OMBI KWA WALIMU WENYE AKILI TIMAMU
Achaneni na CWT bali hamieni CHAKUWAHATA(Chama Cha Kulinda na Kutetea Haki za walimu Tanzania),Huko CWT mtanyonywa hadi mbaki na mafuvu!.
HIKI CHA MA CHA WALIMU HAKINA FAIDA KIFUTWE.
#Ukilala nayo hakikisha unaamka nayo!.
Ni hayo tu.