Cyprian Musiba Anadaiwa zaidi ya Tsh13 bilioni kwa amri za Mahakama Kuu, iwapo atashindwa kulipa ni nini hatma yake?

Cyprian Musiba Anadaiwa zaidi ya Tsh13 bilioni kwa amri za Mahakama Kuu, iwapo atashindwa kulipa ni nini hatma yake?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Cyprian Musiba, kulingana na kiasi kikubwa cha fedha anazodaiwa kuzilipa, kwa kupitia amri za mahakama kuu, ni nini madhara yake iwapo hana uwezo wa kuzilipa na hana mali za kuuzwa ili kupata Tsh 13 bilioni?

Mimi ninaona dalili za Cyprian Musiba kukimbilia ughaibuni .

D129D7FF-D5FE-4FEC-80F1-70B28D65B750.jpeg
 
Kama hana uwezo wa kulipa kiasi hicho adhabu yake ni kwenda Jela na Mdai anapaswa kugharamia gharama za chakula kwa kipindi chote atakachokuwa gerezani

Kwenye hizi Kesi za madai inaweza kuwa hivi Kama mdaiwa hajalipa:-

1. Unaomba Mahakamani kukazia hukumu huku ukiambatisha Mali unazozijua za mdaiwa ili mahakama iziuze ili ulipwe fedha unazodai.
Mahakama itazikamata Mali hizo kwa kutumia mabroker wake na kuziuza ili ulipwe.

2. Kama Hana Mali zozote unaweza kuitaka mahakama iamue mtu huyo unayemdai akae jela kwa gharama zako hadi atakapokulipa fedha unazomdai
 
Hiki kipengele cha pili ni cha ajabu kweli, kwa nini isingekuwa afungwe gerezani na kufanya kazi za umma mfano kufagia barabara, kufyeka majani na kukata miti/matawi, kusafisha vyoo vya umma kwenye maofisi ya umma, mahospitali etc etc??
 
Haki ya nani Membe kwa kumkomesha atalipa hizo gharama za jela. Membe Kwa hasira aliyo nayo nakwambia atalipa wala hakamati Mali. Musiba ana Mali gani za billion 6. Karume naye 7.5 BN na Prof Tibaijuka 80m za mboga.

Hapa iwe funzo kuwa kukubali kutumika kisiasa iko siku utatembea ni vijambo na ushuzi tu vinatoka. Huyu Musiba alijuona Mwamba. Waliomtumia ni wengi tu siyo yule aliyekwenda zake tu Bali wako wengine. Mbona hatusikii wakimtetea? Kawaida toilet tissue ukishaitumia inatupwa. Tujifunze na tujifunze tena.
 
Hiki kipengele cha pili ni cha ajabu kweli, kwa nini isingekuwa afungwe gerezani na kufanya kazi za umma mfano kufagia barabara, kufyeka majani na kukata miti/matawi, kusafisha vyoo vya umma kwenye maofisi ya umma, mahospitali etc etc??
Alafu hiyo fidia mdai alipwe na serikali sio
 
Yeah iko hivyo .. otherwise mdai akishindwa kumgharamia mfungwa gerezani mahakama inamuachia huru
Sasa hizi kesi zinamaana gani kumfungulia mtu wakati kiasi unachodai mdaiwa hawezi kulipa? Sikupoteza muda tu kama mwishoni mdaiwa anaachiwa huru ten, yaani umdai mtuhumiwa then umlipie kifungo Tena!!
 
No problemo. Mbowe akitoka Ukonga atamlipia.
 
Mbowe kwa sasa anapanga mipango ya kumkomboa Sabaya gerezani kutumia makomondoo pindi yeye mwenyewe atokapo gerezani
 
Leo ni siku ya giza katika ulimwengu wa uhuru wa habari. Musiba hilo deni ni dogo sana katika watu wanaoamini katika uhuru wa habari na kujieleza.

Wape namba marafiki zako wakubwa waanzishe kampeni mitandaoni ya kuchangia faini.

Ebu imagine vigogo hawa waanzishe kampeni mitandaoni ya kumchangia mwandishi Musiba aliyepigwa faini sababu ya kufanya kazi yake ya uandishi.

Lissu, Fatma Karume, Maria Sarungi, Zitto, Jenerali Ulimwengu,Msigwa, Lema, Mnyika,Mange Kimambi, Kigogo, Kubenea,Mbowe atume mwakilishi, Maxence Melo, Membe mwenywe, bwana mdogo Nondo.

Hakika hata msaa 10 HAYATAPITA HELA ITAKUWA IMEPATIKANA NA DEMKRASIA ITAKUWA IMELINDWA NCHINI
 
Back
Top Bottom