Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Hukumu Ni Adhabu Hukumu ni Fundisho Kwako Mkosaji na Wengine! Mahakama Iko Sahihi! Atafute Bwana Wapeleke Hela ya Watu
Hiyo adhabu narudia siyo proportional na kosa lililotendeka. Mahakama kuu ilihamaki. Kwani Membe ndiye kiongozi pekee aliyewahi kudhalilishwa kwa matusi? Mbona walisha tukanwa hadi marais, tena wakati mwingine matusi ya nguoni.

Tusubiri maamuzi ya Mahakama ya Rufaa. Nina uhakika adhabu hiyo itapunguzwa kwa kiwango kikubwa sana. Ndiyo maana hata kabla ya muda wa siku 60 wa kuwakilisha hiyo rufaa haujamalizika, Membe ameenda kukazia hukumu na tayari dalali wa mahakama ameshateuliwa kunadi mali za Musiba. Askofu Mwamakula amesema hata kama watanadi kijiji chote cha Musiba, pesa hiyo haitapatikana.
 
Obvious! Mahakama ya Rufaa itapunguza amount, maana tuseme ukweli,hata leo hii mtoa rohoo Israel akikutokea na kuomba Rushwa ya B9 akuachie uhai wako ndani ya Mwaka bado huwezi iipata! Na mwisho wa siku atasepa na rohoo yako!!!
 
MAJIBU YA MHE. MEMBE KWA ASKOFU MWAMAKULA

Baba Askofu Salaam na Asante kwa barua yako ambayo umenitaka nimsamehe Musiba kwa sababu Amesalimu Amri na kwamba hana hela hata kama atauza kijiji.

Baba Askofu, sababu ulizozitoa hazina mashiko kwa sababu Musiba hajaniomba radhi, hajasalimu amri na amechelewa! Aidha hata kama hana hela kama unavyosema, anazo mali zisizohamishika na hizo zote zitapigwa mnada.

Musiba anajua kuwa siwezi kumsamehe kwa sababu nilimpatia nafasi tatu za wazi za kuomba radhi kwenye Chama, kwa barua ya kumtaka aombe radhi kwenye magazeti yake, na kabla ya kesi kuanza tulipata muda wa kulimaliza jambo hili nje ya mahakama. Nafasi zote hizo alizikataa.

Sitamsamehe kamwe na anastahili adhabu hiyo ili awe na adabu na iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kijinga kama hizo.

Nawashukuru Majaji wote wa mahakama kuu kwa uvumilivu na kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kunirudishia heshima yangu na kuuthibitishia umma kuwa katika nchi hii kuna uhuru wa Mahakama na uongozi unaoheshimu sheria.

Vinginevyo nakushukuru kwa barua na mawazo yako. Ubarikiwe.

BM
 
Kuna taarifa ambazo sio rasmi Sana zinadai mwandishi nguli nchini ndugu Musiba Hana chochote anachomiliki mjini zaidi ya simu ya mkononi na fenicha ndogondogo Kama vitanda na meza.
Mali zake nyingi zimeandikwa majina ya ndugu zake inasemekana bi mkubwa wake.
Bila shaka mahakama itabidi iende na adhabu nyingine
 
Siyo mbaya angalau ataambulia kukaa jela na akitoka atalipa taratibu
 
1681506261248.jpg
 
Hana akili yeyote. Jela inamsubiri.
Hukumu yake haikuwa na kipengele hicho! Ndiyo maajabu ya majaji waliotoa hukumu hiyo. Hawakusema iwapo Musiba atashindwa kulipa hiyo billion 9 kitu gani kitafuata, ni kifungo jela cha muda gani?

Hukumu ya mahakama kuu huko Geita dhidi ya mtu aliyemtukana raisi wetu Salmia ilitoa adhabu ya kulipa TSh 10 million au kifungo cha miaka sita. Mtu huyo alishindwa kulipa hiyo million 10 na hivyo kaenda jela ila siku atakapoipata hiyo ten millions ataachiwa kutoka jela. Sasa hukumu ya kimagumashi dhidi ya Musiba kwa kumtukana Membe ni 9 billion cash, akishindwa mali zake zote zinanadiwa na dalali wa mahakama ambaye aliteuliwa siku 5 baada ya hukumu. Full stop!
 
Mm namsihi mzee membe kama yupo humu au mtu wa karibu yake tumsamehe musiba Aliingizwa choo cha kike
 
Kuna taarifa ambazo sio rasmi Sana zinadai mwandishi nguli nchini ndugu Musiba Hana chochote anachomiliki mjini zaidi ya simu ya mkononi na fenicha ndogondogo Kama vitanda na meza.
Mali zake nyingi zimeandikwa majina ya ndugu zake inasemekana bi mkubwa wake.
Bila shaka mahakama itabidi iende na adhabu nyingine
Nilisema mwanzoni wakati Musiba akirukaruka, na wengine waliokuwa wana hemeka kwamba wamalize vita vyao vya kimatabaka huko huko kwenye Vikao vyao. Wameyaleta hadharani, wametengeneza matabaka mengine mapya- Sasa chuki zimewakumba Watanzania. Hakika sintoshangaa tukatoana macho na tukashonana midomo na kukatana vidole huko mbeleni. Nilinena

Kuhusu hili Suala, ni lazima tupime nani aliyekuwa na Mikono na Mifuko mirefu. Wapo wale wwnzetu huko wanaosema "Follow the Money" haijalishi za Musiba au za Membe. Hakika ningependa kuona suala hili likifuatiliwa kwa Umakini na wale wanaoitwa Investigative Journalist.....tukiacha wale wa "Iam the State"
 
Hivi musiba alishinda kesi alivyokata rufaa?
Au waliamua kukaa kimya maisha yaendelee?
 
Back
Top Bottom