Daaah, bodaboda bodaboda...inauma sana

Daaah, bodaboda bodaboda...inauma sana

Yeyote anayesoma hapa, ajue anatembea na kifo kinammendea, mauti inatafuta namna yeyote ile imtafune, basi tu neema ya Mungu inatufunika, kama sio Mungu hakika tungeshakufa. unaweza usife kwa bodaboda, ukafa kwa kupiga chafya tu. namfahamu jamaa mmoja alikuwa na pesa sana, alipaliwa chakula akafa. wengine wanakufa kwa ugonjwa, wengine wanakufa kwa kupigana, wengine ajali za magari, wengi tumeendesha magari leo ila tumefika salama nyumbani, wengine wamelala hawajaamka usingizini hukohuko. kwa hiyo kifo kipo, ishi ukijua any time unaweza kufa au uanweza kuendelea kuishi.

shida wanadamu wengi wanaishi kwa kubeti, wanafanya bahati nasibu kwenye uzima wa milele vs jehanum. Kwa kuwa ukimkiri Yesu kwa kinywa chako kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako kuwa alifufuliwa katika wafu basi utaokoka. usiogope kifo, ogopa jehanum, ukifa katika dhambi moja kwa moja motoni. na hujui utakufa lini, au ukilala leo utaamka au la.

UFUNUO 14:13 IMEANDIKWA: 13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

duniani kuna KUFA KATIKA KRISTO NA KUFA BILA KRISTO. Ukifa katika Kristo manake umekufa katika utakatifu, uliokoka na ukaendelea kuishi maisha matakatifu ukijitakasa hadi unakufa ukafa ukiwa mtakatifu.

1WATHESALONIKE 4: 15 -18 INASEMA; Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

Usidanganywe na mapadre na wachungaji au watu wa dini zingine zozote, wanaohubiri kwamba ukifa utaombewa ukiwa maiti ukasamehewa dhambi. usichelewe kuokoka ati hata ukifa katika dhambi utaombewa ukiwa maiti, pia usiogope kuhama dini yenye mapokeo nje ya Neno la Mungu ati kwa kuogopa utakosa padre wa kukuombea msamaha ukiwa maiti, Mungu hatambui icho kitu, ingekuwa hivyo hakuna ambaye angetakiwa kuokoka, wote tungetenda tu dhambi na tukifa tunaombewa na wanaotuzika, basi tunaenda ahera. padre wala mchungaji au shehe asikushike masikio na kukutisha kwamba ukiondoka kwake utakosa wa kukuombea, ni uongo wa shetani huo, na mtu asikudanganye ati ukihama dini au kanisa lako umeasi Mungu. kuna makanisa yana mapokeo nje ya Neno la Mungu, wanaabudu maria, wanaomba kwa wafu, wanakataa Roho Mtakatifu na kazi zake, wanaabudu dini kabisa hawamwabudu Mungu, watu kama hao wakimbie, dini au dhehebu kama hilo likimbie, nenda lile linalofuata Neno la Mungu.

wengi utaona wanaenda kwenye kaburi ati wanaenda kumwombea marehemu. ni utapeli wa shetani. Neno la Mungu linasema, ukifa, matendo yako yatafuatana na wewe, yaani siku ya kifo ndio deadline yako ya kutubu, hakuna mtu atakutubia badala yako ukiwa umekufa, ndio maana Yesu alisisitiza kwamba "tukeshe", hatujui siku wala saa. na kweli hatujui siku wala saa aidha ya kifo chetu au ya kurudi kwake, lazima tukeshe. alitoa mfano wa tajiri aliyejilimbikizia mali, akasema moyoni mwake kuwa sasa akae chini ale na kushiba, kumbe hajui usiku ujao roho yake inaenda kuchukuliwa. tukeshe wandugu. na wale ambao hawajaokoka, okokeni leo, mkijua kuwa mkifa bila kuokoka mnaenda motoni.
 
Ni watu waliojikinai hawa.
Hawaithamini zawadi ya uhai.
 
breki zao honi siku hizi,

ninsikitisha sana:4weirdW:

hata hivyo tusisite wala kuchoka kama familia ya waTanzani na JF, kukumbushana mara kwa mara wajibu wa kila moja kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Na kwamba wanaotumia barabara ni wengi. Asiwepo hata moja anaedhani yuko pekeyake barabarani, au yeye pekeyake ndie mwenye haraka kuliko wengine. Madhara yake ni makubwa na mabaya sana, na miongini mwake ni pamoja na hili la kwenye picha.

ni vizuri na kua makini wawepo barabarani, na kujiepusha na mwendo mkali usio na tija yoyote.
daima waepike kutumia vilevi matahalani visungura waendeshapo bodaboda zao:MODS:

inahuzunusha sana na inasikitisha sana, kupoteza kijana, ndugu, jamaa au rafiki mwenye familia yake, nguvu na afya yake kabisa, tena siku ya sikukuu kwa mtindo wa ajali kama hiyo.

inatafakarisha sana inahuzunusha sana...

R.I.P Gentleman:4weirdW:
 
Back
Top Bottom