Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli kabisa. Lakini na sisi abiria tuwe wakali wakati tuko kwenye pikipiki.Tunasikotika kwa sababu abiria wanakuwa ni wahanga wasio na hatia
Ila na wao yanawapata ya kugongwa kwa kufuatwa wao kwenye njia zao. Sema mara nyingi wao ndio huwa watu wa fujoBodaboda walishafanya watu wengi kuwa sugu kuwasikitia! Mmi sidhani kama wana akili za kawaida. Pengine wachina wameweka mitambo kwenye hizo pikipiki ya kuwafanya wapate wehu!
Ilikuwa usiku alitaka kupita katikati ya boda boda mbiliUnaweza jiuliza kwenye 'lane' iyo alifata nini ila unaweza kosa majibu ya haraka.
Kwahiyo walokole hawaumwi, hawapti ajali, hawafi, hawana shida yoyote na ni matajiri.Tunasikotika kwa sababu abiria wanakuwa ni wahanga wasio na hatia
Wengine kweli wanajitakia. Huku kwetu wanaitwa TK1, wazee wa madedeWataisha sana wazee wa Nduthi
Hilo semi nadhani nahisi linapita tu wala halihusiki na hiyo Ajari ni picha tu ineikamata semi inamaliziaUnaona kuna semi kule mbele? Nadhali alitaka kulipita akiwa na 100km ndio akakutana na Howo
Yeah!! lakini unadhan inasaidia sasa? Binafsi nina tabia ya kutia risala fupi kila ninapopanda bodaboda ugenini! Maneno yangu ni simple tu ' boda hii miguu Kuna watu wanitegemea huko nitokako kwa rizki zoote unazozijua' kuwa makini!! Sasa mwezi wa 12 nipo sehemu nikachukua boda, hata dk moja hatukuchua ukafanya uzembe wa kuingia junction bila kuangalia tukavaana na boda mwenzie hadi unafika mtaroni ye kavunjika mkono mi nimevunja smartphone ila nilitoka salama.Ni kweli kabisa. Lakini na sisi abiria tuwe wakali wakati tuko kwenye pikipiki.
Mbona kama hukunielewaKwahiyo walokole hawaumwi, hawapti ajali, hawafi, hawana shida yoyote na ni matajiri.
Acha kila mtu aishi kwa imani yake. Kuna wakristo, waislam, wahindu, nk. Kila mmoja kwa imani yake ataishi.
Asante mtumishi. Mwenye masikio na asikie 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Yeyote anayesoma hapa, ajue anatembea na kifo kinammendea, mauti inatafuta namna yeyote ile imtafune, basi tu neema ya Mungu inatufunika, kama sio Mungu hakika tungeshakufa. unaweza usife kwa bodaboda, ukafa kwa kupiga chafya tu. namfahamu jamaa mmoja alikuwa na pesa sana, alipaliwa chakula akafa. wengine wanakufa kwa ugonjwa, wengine wanakufa kwa kupigana, wengine ajali za magari, wengi tumeendesha magari leo ila tumefika salama nyumbani, wengine wamelala hawajaamka usingizini hukohuko. kwa hiyo kifo kipo, ishi ukijua any time unaweza kufa au uanweza kuendelea kuishi.
shida wanadamu wengi wanaishi kwa kubeti, wanafanya bahati nasibu kwenye uzima wa milele vs jehanum. Kwa kuwa ukimkiri Yesu kwa kinywa chako kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako kuwa alifufuliwa katika wafu basi utaokoka. usiogope kifo, ogopa jehanum, ukifa katika dhambi moja kwa moja motoni. na hujui utakufa lini, au ukilala leo utaamka au la.
UFUNUO 14:13 IMEANDIKWA: 13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
duniani kuna KUFA KATIKA KRISTO NA KUFA BILA KRISTO. Ukifa katika Kristo manake umekufa katika utakatifu, uliokoka na ukaendelea kuishi maisha matakatifu ukijitakasa hadi unakufa ukafa ukiwa mtakatifu.
1WATHESALONIKE 4: 15 -18 INASEMA; Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Usidanganywe na mapadre na wachungaji au watu wa dini zingine zozote, wanaohubiri kwamba ukifa utaombewa ukiwa maiti ukasamehewa dhambi. usichelewe kuokoka ati hata ukifa katika dhambi utaombewa ukiwa maiti, pia usiogope kuhama dini yenye mapokeo nje ya Neno la Mungu ati kwa kuogopa utakosa padre wa kukuombea msamaha ukiwa maiti, Mungu hatambui icho kitu, ingekuwa hivyo hakuna ambaye angetakiwa kuokoka, wote tungetenda tu dhambi na tukifa tunaombewa na wanaotuzika, basi tunaenda ahera. padre wala mchungaji au shehe asikushike masikio na kukutisha kwamba ukiondoka kwake utakosa wa kukuombea, ni uongo wa shetani huo, na mtu asikudanganye ati ukihama dini au kanisa lako umeasi Mungu. kuna makanisa yana mapokeo nje ya Neno la Mungu, wanaabudu maria, wanaomba kwa wafu, wanakataa Roho Mtakatifu na kazi zake, wanaabudu dini kabisa hawamwabudu Mungu, watu kama hao wakimbie, dini au dhehebu kama hilo likimbie, nenda lile linalofuata Neno la Mungu.
wengi utaona wanaenda kwenye kaburi ati wanaenda kumwombea marehemu. ni utapeli wa shetani. Neno la Mungu linasema, ukifa, matendo yako yatafuatana na wewe, yaani siku ya kifo ndio deadline yako ya kutubu, hakuna mtu atakutubia badala yako ukiwa umekufa, ndio maana Yesu alisisitiza kwamba "tukeshe", hatujui siku wala saa. na kweli hatujui siku wala saa aidha ya kifo chetu au ya kurudi kwake, lazima tukeshe. alitoa mfano wa tajiri aliyejilimbikizia mali, akasema moyoni mwake kuwa sasa akae chini ale na kushiba, kumbe hajui usiku ujao roho yake inaenda kuchukuliwa. tukeshe wandugu. na wale ambao hawajaokoka, okokeni leo, mkijua kuwa mkifa bila kuokoka mnaenda motoni.
Aiseee! Tumbo la uzazi limenicheza😔i
Kumamamaake jamaa alikuwa anajiona yupo kwenye mbio za MotoGP ama dah bodaboda hawana akili kabisa yaan anavyolala nayo dah !Wataisha sana wazee wa Nduthi
nimependa Jina lakoKuishi ni Kristo,na kufa ni faida. Kama ukiishi, basi ishi katika Kristo, na kama kufa basi ufe katika Kristo.
Mhh hii picha ya mchongo ukiangalia vizuri. Kwanza hakuna hata damu wala nyama nyama zimetapakaa, pili hakuna hata mashuhuda pembeni wakishangaa, tatu mtu kanasaje hapo maana analingana na gari unene.Unaweza jiuliza kwenye 'lane' iyo alifata nini ila unaweza kosa majibu ya haraka.
Wote hao wa ninitena m nnao wa 3
nkimkosa uyu lazma nmpate yuleWote hao wa nini