Daah Nimefika Dar es Salaam mbona sifa nilizozipata ni tofauti

Daah Nimefika Dar es Salaam mbona sifa nilizozipata ni tofauti

Hata vidole havifanani mkuu ,Dar kuna matabaka matatu 1.Matajiri sana 2. Watu wa kawaida (standard level of living) 3. Watu mafukara aka walala hoi wanaosindikiza mji,asilimia kubwa ya hili kundi ni wazawa
 
Ulipata sifa gani? Maana kama ni dadapoa bado wapo ila kwa kificho kama ni mpenzi wa kaka poa nao wapo japo kiongozi wao wanagawa huduma segerea delicious.
Kamani ngada huyo jamaa kabana kias lkn ukitaka unapata tuu.
Kama ni bilcanas usijali walitudhulumu. Ila nyingine zipo.
Sa sijui ulitegemea nn
 
Dar kubwa kijana. Kuna sehemu ukipita utaona bora kolomije maana pombe zinapikwa vibaya kama kawe na kigogo walai hizo sehemu sijui kwa nn nako kunaitwa dar.

Ila jaribu kwenda posta, masaki, osterbay, mikocheni, upanga, nk ili walau uamini kuwa umeingia dar ila we umeenda sokoni ukatarajia kuona tofauti na kolomije hapana
 
Hata vidole havifanani mkuu ,Dar kuna matabaka matatu 1.Matajiri sana 2. Watu wa kawaida (standard level of living) 3. Watu mafukara aka walala hoi wanaosindikiza mji,asilimia kubwa ya hili kundi ni wazawa
Very true, namba tatu ndio imeshika kasi. Wengi ni wapangaji tena wa single bedroom(jiko, sebule, store) kila kitu humo humo.

Maeneo machache yana hadhi ya kulifanya liitwe jiji.
 
Umefika Dar ? Umeuona ule mnara wa askari ambao mbunge wako Goodlack Mlinga alitaka ubadirishwe liwekwe sanamu la Diamond? Kama hujafika hapo bado hujafika Dar Es Salaam
 
Wakuu nashukuru Mungu nimefika Dar taangu juzi lakini Sifa tunazozisikaga ni Tofauti kabisa Leo nimeweza kukatiza mitaa ya Karikoo Nimeshangazwa na Majitaka/Mavi yalivyozagaa mitaani Jana nilitembea Baadhi ya Mitaa inasikitisha.


View attachment 493878View attachment 493879
Hawajambo kwenu Koromije.?
Tatizo umekuja kwa shemeji yako aliyemwoa dada yako na wamepanga Bunju huwezi kuufaidi mji.!
Mwambie shemeji yako akutembeze uje huku Masaki uone watu wanavyokula pepo wakiwa hai.!
Sema mi mwenyewe mgeni kama wewe nimekuja kwenye msiba wa Chande
Narudi kwetu Dom kesho nikaendelee na biashara yangu ya majeneza.[emoji12]
 
Back
Top Bottom