Daah Nimefika Dar es Salaam mbona sifa nilizozipata ni tofauti

Daah Nimefika Dar es Salaam mbona sifa nilizozipata ni tofauti

Unajua dar asilimia kubwa wake kwa waume wadada kwa wakaka hadi watoto ni wambea wanapopularize mji ila hakuna kitu
 
Ni kawaida hiyo Dunia nzima ni hivyo, unachokisikia siyo uhalisia, ukifika utashangaa!
Weeee,upo serious kijana?maana naskia marekani huyo Beverly hills ni hatari,kwahiyo inawezekana sio kweli?[emoji17] [emoji17] [emoji17] [emoji17] [emoji17]
 
Wakuu nashukuru Mungu nimefika Dar taangu juzi lakini Sifa tunazozisikaga ni Tofauti kabisa Leo nimeweza kukatiza mitaa ya Karikoo Nimeshangazwa na Majitaka/Mavi yalivyozagaa mitaani Jana nilitembea Baadhi ya Mitaa inasikitisha.

Hayo siyo muhimu kwao kaka, wako bize na kina [HASHTAG]#Makonda[/HASHTAG] na kina [HASHTAG]#romakatoliki[/HASHTAG].
Hivyo vinyesi mitaani, kuishi kwenye mabonde, mashimo barabarani, wachuuzi barabarani, usafi, usafiri wa wanafunzi, ukatili kwa watoto na kina mama SIO MUHIMU KWAO..HII NDIO DAR ES SALAAM!
 
Weeee,upo serious kijana?maana naskia marekani huyo Beverly hills ni hatari,kwahiyo inawezekana sio kweli?[emoji17] [emoji17] [emoji17] [emoji17] [emoji17]


Ni kweli ni hatari lkn ukifika labda hata wewe utajiuliza hilo swali, ile b.hills niliyokuwa naiona kwenye movie za Hollywood ndiyo hii au kuna nyingine? Ishanitikea mimi mara nyingi sana!
 
Bro haiwezekani katika mkusanyiko wa watu zaidi ya mil 6 wote wakawa level ya juu. Kuna average joes na mafukara kabisa. Hii ni global trend, hapo Nairobi kuna maeneo kama Eastleigh na na Kibera slums, ukifika unaeza ukatoka machozi wanadamu wanaishi kama mende, lkn tunaambiwa Kenya ni 2nd world country.

Izunguke Dar ufike maeneo ya watu wa average kama salasala, uende maeneo ya wenye nazo huko kunduchi, ufike city centre nk. Hizi picha hapa chini zote ni Dar.
e2200cfe3e179d2354f00af9557692dd.jpg

Na hautaamini kuwa hapa ni Detroit, Marekani
Hii picha nilitaka kubisha kwa kusema Dar gani hiyo ina open space kumbe ni jangwani hapo
 
Ww umefikia Tandale kwa Tumbo unategemea nn ? Kinondoni huku mkuu
 
Back
Top Bottom