Irene Mallya anamtafuta Mama yake Happiness Mallya, mfanyabiashara wa Kariakoo mkoani Dar es Salaam, ambaye hajulikani alipo tangu ilipotokea ajali ya kuporomoka kwa jengo Jumamosi Novemba 16, 2024.
Irene amezungumza na TBC Digital katika eneo hilo la ajali Kariakoo ambapo shughuli za uokoaji zinaendelea na kusisistiza kuwa Mama yake Happiness hajapatikana hadi muda huu.
“Mama alinipigia asubuhi Jumamosi nilikuwa mbali na simu nilipokuja kupiga sikufanikiwa kuwasiliana nae nikajua tu atakuwa kwenye vikao na wafanyabiashara wenzake”. amesema Irene
Amesema baada ya hapo alipokea taarifa kutoka kwa ndugu yake aliyepigiwa simu na mama yake, lakini kwa sasa simu yake haipatikani.
Yes kikubwa kama oxygen wanapata wanaishi, mwili wa binadamu unastahimili sana unadhoofika lakini unaishi tuombe Mungu waliobaki watolewe leo. Tuseme Amiiin