Ni kweli ni mpenzi wako, lakini siyo kila kitu cha kwenye familia yako au ukoo wako anapaswa kujua vingine vibaki siri ya ukoo wako ili kuilinda heshima yako kwa huyo mwenza wako.
Punguza kusema kila kitu kuhusu Wazazi, ndugu zako kwa huyo mwenza wako maana kama hana hekima kuna siku atavitumia kama fimbo kukuchapia na itakuuma sana maana mlango ulifungua mwenyewe.
Unakuta mtu anamweleza mwenza wae madhaifu ya aibu ya mzazi wake, Ooo huyu baba yangu namjua achana naye akilewa huwa anaropoka ovyo au huwa anajikojolea hatuwezi kwenda naye mbele za watu, weee dada wewe, wee kaka wewe siku mkigombana kama mwenza wako hana hekima utajisikiaje akisema huna akili kama Baba yako anayejikojolea akilewa?
Mara mama yangu hivi, mara dada yangu sijui hivi, kaka zangu vile, hebu watunzie heshima ili huyo mwenza wako awaheshimu pia, kumbuka kadiri anavyojua madhaifu ya ndugu zako kupitia wewe kuna namna na heshima yako inashuka kwake anajua ni suala la muda tu huenda na wewe una chembe chembe za hivyo kuna siku utaropoka kama mama yako mana maji hufata mkumbo.
Jifunze kuwalinda ndugu zako, mwenza wako ajue madhaifu ya ndugu zako kwa bahati mbaya ila siyo wewe ndio msimuliaji loh!