Dada kama huwezi kutengeneza kipato hata cha sh. 500 kwa siku hufai kuwa mshauri, mpenzi, mchumba au mke wa mwanaume yoyote

Dada kama huwezi kutengeneza kipato hata cha sh. 500 kwa siku hufai kuwa mshauri, mpenzi, mchumba au mke wa mwanaume yoyote

anaweza asiwe na uwezo wa kujiingizia kipato cha sh. 500 per day ila akawa na uwepo wa kupiga mizinga na kujipatia kipato cha sh. 50000 per day
 
Ila sometimes inaboa sana. Mwanamke anaomba mpaka hela ya pedi aisee. Mpaka hamu ya kuwa nae inaisha kabisa. Punguzeni/acheni kuomba vitu vidogovudogo vinawashushia sana thamani yenu
 
Zita andikwa ngonjera kwenye thread hii, yetu macho
 
Shiki
Happy new December month, (kwa heshima ya aliyeanzisha uzi ule) niende kwenye mada moja kwa moja,
kwanza naanza kwa kutoa wito kwa wanaume wenzangu, kuwa usikubalia kudate au kuwa kwenye mahusiano na mwanamke asiyeweza kuwa na mawazo hata ya kujiingizia sh 500 yake japo ya vocha kwa siku au kwa wiki.

Unaweza kukuta mdada anasema mimi siwezi date na mwanaume anayefanya kazi fulani, wakati yeye hata uwezo wa kujiingizia sh.500 hana kwa siku. sasa mimi huwa najiuliza yaani wewe pale kukuomba namba tu,tayari ujumbe unaofata nitumie salio maana kifurushi kimeisha sasa inamaana wewe huwezi kujinunulia hata salio la 500,.hiyo inamaana kuwa huwezi kuwa na mawazo hata ya kunishauri nini nifanye ili kipato kiongezeke ili maisha yaende, kwa sababu tafsiri yake ni kwamba kama huwezi kuwa na mawazo hata ya kutengeneza sh.100 kwa siku hivyo utakuwa na mawazo ya kuomba na kutumia tu na sio kuzalisha, kwa hiyo wewe nakuchukulia kama mfirisi tu.

Unakuta mdada umeanza kuwasiliana kwenye mitandao siku mnapanga kuonana anaomba nauli halafu sehemu yenyewe nauli yake haizidi 2000, kwenda na kurudi... sasa wewe tunaonana ili iweje... ukweli mimi ukiniambia nikutumie nauli hapo hapo huwa nakublock....

Kwa mfano kwa hapa Mwanza labda mdada anakwambia yuko Igoma na unamwambia basi tukutane mjini kati ujumbe unaofata eti nitumie nauli, yaani sehemu ya kutumia sh. 1000 nayo pia nikutumie nauli wakati ukifika nitatumia zaidi za sh.30,000 to 50000, kulingana na eneo tutakalokutania... ukiniomba nauli au vocha haraka sana unakula block, UKUBALI NDIO HIVYO HIVYO, UKATAE NDIO HIVYO HIVYO
Shikilia hapo hapo.
 
Kuna ka freedom flani hivi in a woman kanakuwepo with self-money from self hustle.
 
Dah kizazi cha wanaume halisi wanaoyaelewa majukumu yao kinapotea kwa kasi sana Mungu aturehemu

Mkuu wewe unachopaswa kuomba sana ni kuwa na mwanamke anayeweza kukupa support unayohitaji ili uweze kuosnga mbele na kufanya vitu vikubwa kwa jili ya familia yenu

Ukumbuke jukumu la kutunza familia matearilly hilo ni la mwanaume na si vinginevyo,mke akifanya anasiaida tu na sio kigezo cha lazima kwamba awe pia anatafuta kipato cha familia

Hivi unataka kuniambia mama wote ambao hawakuwa wakiingiza hata mia tao na ndio ambao wametulea na kutufikisha mpaka hapa tulipo,walikuwa hawana maana na msaada kwa baba zetu?

Shida siku hizi tumeshaona pesa ndio kila kitu,

Mkuu mind you pesa doesn't make a home but a house or a bungalow, and what makes someone complete and happy is not a house or a bungalow its a home,ndo maana wanasemaga home is sweet, sweet sweet home and only mwanamke anayeitambua nfasi yake anaweza kuifanya nyumba yako ikawa home na sio yule anayejua kutafuta pesa,

Pesa hailei watoto kuwa watu wema kwenye jamii Zaidi ya kuwapeleka shule na kuwanunulia vitu vya hapa na pale ambavyo ni so minor katika malezi ya mtoto kiujumla

Pesa haikupi peace of mind mkuu,ukichafukwa unachohitaji ni faraja maneno mazuri kutoka kwa mtu anayejali na uhakikisho wa kwamba unaweza kusonga mbele licha ya changamoto mia unazopitia

Kuna mambo mengi sana ambayo pesa haiwezi kufanya ile mke mzuri mwenye sifa zinazostahili anaweza kufanya na Maisha yakasonga

Acha kuweka kigezo cha mwanamke kuweza kutafuta pesa ndo kiwe kigezo kikuu,tafuta pesa mkuu,tafuta mwanamke anayejielewa na kujua nafasi yake katika familia,utaenjoy pesa zako na Maisha kwa ujumla,

Tofauti na hapo unaweza ukapamta mwanamke anayeweza kuingiza hata milioni kadhaa kwa mwezi ila ukaishia kuisikia Amani na furaha kwa majirani na usiache kuona rangi zote duniani.
Ngoja ni mtag yule member anayejiita nyoka mweupe aisome hii
 
Mkuu shida kubwa inatupata wanaume wengi wa sasa ni kutafsiri hili neno kazi,

Tumeshaweka vichwani mwetu kuwa kazi ni kufanya kitu kinachoweza kukuingizia pesa tu,

Hii tafsiri ndio inayobadilisha mfumo mzima wa Maisha na kufanya tusindwe kabisa kuuona mchango wa mwanamke asiye na kazi ya kuingzia kipato

Mkuu hivi unaijua kazi ya kuutunza mji wewe? Unaijua kazi ya kuhakikisha nyumba yako iko safi muda wote, kazi ya kutunza mazingira ya nyumbani kwako yapendeze wakati wote, si masika si kiangazi? Unaijua kazi ya kufikiria leo watu wangu home wale nini? Leo niwapikieje ili wale chakula waenjoy? Unaijua kazi ya kufua kila siku tena kama ndo wanaume tunaofanya kazi tumejilaza kwenye mavumbi na kujifutia magrease tunajifutia kwenye nguo zetu,watoto wanaojifunza kutambaa vile huwa wanabadilidha nguo hata mara tano kila siku?kukaribisha wageni na kuhakikihsa wanakuwa entertained wawapo kwako ili wewe baba mwenye nyumba yako upate sifa kuwa nyumba yako ni mahali salama na penye kufurahisha kuishi?

Sijui mtazamo wako juu ya haya maswala mengine ila nadhani ni wakati sasa tubadilike tusiamini kazi ni zile za kuingiza pesa

Wanawake (wale wanaojitambua na kuyatendea haki majukumu yao kama mama zetu,dada zetu ) wana mchango mkubwa sana katika familia zetu hata kama hawafanyi kazi za kuingiza pesa

Wanafanya kazi nyingi sana kuhakikisha sisi wanaume tunafurahia Maisha na kuenjoy

Pale unapojua ukifika home utapakuta pakiwa safi na utaweza kupumzika kwa raha na Amani

Utapata walau glasi moja ya juisi baridi safi made from wifey au kikombe kimoja makini sana cha uji wa maziwa safi huku ukisubiria msosi mtamu made from baby mama

Ile hisia nzuri ya kuamini watoto wako wako mikono salama pale ujuapo mama yao yupo kwa ajili yao akihakikisha anashuhudia kila hatua ya ukuaji wa mtoto wenu na kukupa ripoti kadha wa kadha juu ya maendeleo ya mtoto wenu na inapolazimu kujadili juu ya nini cha kufanya baada ya mama kugundua mtoto wenu ana shida Fulani na kukuletea ripoti

Mkuu nothing beats a good woman who uses all her power to make a home for her family,a place where everyone can enjoy have fun and feel safe and cared for.
Mkuu unakipaj cha kuandika na ushawish,nilikuwa upande ule ila nmekuelewa sana,nmerudi huku
 
Kuomba nauli sio sababu ya kwamba hawezi kutafuta hela au kwamba hana hela ni hulka yao kuomba na kutegemea. Yaani mwanamke ni parasite ya mwanaume. Hii dunia bila mwanaume haipo! Waulize walioa wake watafutaji hela yao ni yao na ya mwanaume ndio pesa ya familia. Alafu mbaya zaidi mwanamke anajifanya kukushauri kuhusu hela yako wakati yake haijulikani inakoelekea. All in all hii dunia ni ya sisi wanaume kwa hiyo ni wajibu wetu kuiendeleza ikiwemo hiyo ya kutegemewa hao parasites wetu wanawake!
 
Back
Top Bottom