Dada na mdogo wake wananipenda bila kujuana

Dada na mdogo wake wananipenda bila kujuana

The Garang

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
2,880
Reaction score
4,830
Assalaam.

Nipo home napigiwa simu na dada ambaye ni kama family fiend wetu kutokana kwa wazazi wetu kushibana katika mambo mbalimbali. Simu ilikuwa ikinijuza ya kuwa kuna dada wawili wanakuna wanaomba niwasaidie kufanya application za chuo. Ikaisha hivyo.

Baada ya masaa kadhaa, nikaja fatwa kwenda kusaidia zoez la ufanyaji application. Walikuwa ni mabinti wawili, mmoja mfupi kiasi bonge bonge toto laini msuko juu plus miwani, na mwingine mrefu kiasi mwili wa kawaida short hair. Nimeingia sikusalimia kutokana na ubongo wangu kushindwa kutoa jibu la maaana niwape salamu ya Aina gani.

Basi nikaitikia wito wao, nikauliza vyuo walivyokuwa wanataka apply lakini kumbe mmoja wao kati ya wale wawili ndio alikuwa anahitaji kufanya application. Wakati naendelea na zoezi la application nikaja kugundua wale dadaz ni mtu na dogo lakini huwezi kufananishia jinsi wametifautiana.

Zoezi limeendelea hatimae sote tukawa comfortable na kila mtu, mazungumzo ya kawaida yakaendelea pale ikafikia kipindi nikawa nimemzoea mdogo mtu hadi nika finya kapua kake huku yeye akicheka tu, wakati hio dada mkubwa alikuwa amegeukia pembeni.

Zoezi likatamatika kwa siku hiyo nikapewa ujira wangu kwa usumbufu, SIKUCHUKUA naba yake japo wakat namsajili aliitaja lakini sikutaka niibe namba hadi niombe kwake ndio anipe. Siku ikaisha tukaagana.

SIFA ZAO.
Mdogo mtu ambae ndio alikuwa ana apply chuo alikuwa ni mchangamfu muongeaji sana viingereza kwa wingi na slang kama zote UPANDE WA pili dada hakuwa muongeaji na alionekana Yuko serious sana jambo ambalo lilinifanya nisi concentrate sana naye nakutumia mda mwingi na dogo mtu.

KUIPATA NAMBA YA DOGO .
Alikuja siku nyingine pamoja na mama ninae mjua kwa sura, huyo mama binti yake alikuwa jeshini hivyo alikuja nimsaidie ku apply kama nivofanya kwa huyu dogo ambae amekuja nae.
Zoezi lilikamilika vizuri, wakati naendelea huyu dogo akaniuliza kama kuna siku nimemtafuta nikamjibu hapana akanambia kuna namba ngeni imempigia ,nikakanusha ikaisha hivyo LAKINI nikasema chukuaa basi namba yangu [emoji1][emoji1] alichonijibu


Endelea na hii wakati naandika ingine.
 
Part 2

Nikamuhitaj aandike namba yangu[emoji1][emoji1] binti akshangaaa heeee , japo ckuongea nikiwa serious sana ,mie nikaona isiwe shida kwakuwa hata sikuwa na mpango nae.

Yule mama aliekuja nae, alikuwa anaweka mafile yake vizuri aliokuja nayo kwa ajili ya mtoto wake, wakati wa kuagana akamuuliza huyu dogo, vp umechukua namba ya kaka hapa???? dogo akajibu hapana. Akaambiwa achukue incase akihitaji msaada aweze nipata. NAMBA yangu akaichukua kihivyo.

Kutokana na simu yangu kuwa galasa kwa kipind fulan sikuweza wasiliana naye, kuna siku Niko online ikaingia text, mambo nkamjib poa nan, akasema mie fulan, tukachat pale huku akiniuliza mbona hukuwa ukijib text zangu nikamuambia simu yangu ilikuwa mbovu, akaelewa. Tukamaliza kwa mtindo huo.

KUANZA MAHUSIANO.
Usiku niko online sms inaingia, mambo nikamjibu ipasavyo akaniuliza usiku hhuu unachat na WIFI hapo ndo ikawa kwisha habari yake. Nikamjibu hapana akauliza tena wifi yukowap sasa nikamjibu hayupo, basi ikawa imeisha hivyo.

Siku zimeenda mtoto wa watu akaanza kunielewa mnyamwezi mdogo mdogo kama Mondy vile namie nikawa Nampa full attention sms zake znajibiwa chap zaidi ya kupiga menu ya m-pesa .MIE huwa cpendi sana kutongoza huwa nataka ufall mwenyewe kwanza ndio nimalize kazi, basi mpira ukajaa kwenye 18 za Messi nikascore kiulaini mtoto akatiki mapema sana.

Tumeendelea na mahusiano kama ambavyo huwa yanakuwa kwa watu wengi kipindi cha mwanzoni simu sms kila muda ,full kuimbiwa nyimbo za kina B2K za dini kama zote.

[emoji1][emoji1]mtoto alinipendaa aisee ikawa akikosa reply yangu basi ataliaa mtoto wa watu atahuzunika sana na full lawama ,nikajisemea huyu atajakoma mwenyewe ngoja apoee.

Tumeendelea tukajafahamiana vzuri, binti ka date na jamaa mmoja tu wakaja achana kisa jamaa alitaka tunda kabla ya ndoa[emoji1]. Kwa lugha ingine dogo alikuwa SEALED kama Jokajeusi anavotuhusia humu ndani. Haikuwa case life limesonga mambo yamekolea, tukaahidiana vingi vingi hadi majina ya watoto A na nanii sijuii.

KUANZA KUTOKUELEWANA.
Kila lenye marefu na mapana huwa halikosi mwisho Harmonize aliimba kwenye ngoma yake ya Nishachokwa.
Binti alienda chuo basi kila linalojiri akawa ananisimulia , continuous na mwaka wa mwisho wanavomsumbua. Inshort dogo ni mzuri ni kama vile kina Mboni Mhita sura yake na dimpoz kadhaa za kichokozi.

Kama wengi tunavoamini asiyekuwepo na jina lake halipo na fimbo ya mbali nyoka haiui abadan asilan. Maongezi yetu yakaanza kupungua, zile sms za asubuhi hakuna wala nn the same mchana the same jion na usiku. Mie nikachukulia poa coz ni mwanafunzi na kwao wako strictly kinoma UKIZINGATIA wako wawili tuu kwenye familia yao na yeye pekee ndiyo kafika level ya degree hivo ni mboni ya familia.

KUclear CHATS
Kuna kipindi alikuwa anaclear chats zetu kiasi kwamba kama kuna jambo tuliongea na hatukulimaliza kutokana na kuishiwa mb au chaji kuisha, nikifika kesho nikuanza kumuambja na upya.
Sikuwa na penda suala la kufuta chatting, hasa ukimuuliza lengo ni nini hatoa sabab za msingi hapo nikahisi napigwaaa. WASIWASI NDO AKILI MAMEEEN!!![emoji846][emoji846]

Sio mwepesi wa kutambua kosa na kuommba msamaha akikosea, hata ukijarbu kumuonesha kuwa kakosea wapi ajirudi aombe msamaha ,alikuwa anakaza .Nikaona hapa ntaja kupiga mtoto wa mtu buree na citak itokee hivo.
Kuna kipind nilimuuliza jambo akanikaliaa kimya akiwa ameni bluetick na akasepa online. Siku hiyo nikamuuandikia rasmi wakala kutoka kamati kuu kuwa ATAFUTE mwingine.

Zimepita siku akaanza visalamu vyake mambo lakin ckuwa najibu. Akaja akantumia picha zake nyiiiingi lakini sikuview ,ziliji download zenyewe nkazikuta kwenye gallery nikaview then nkapotezea.

SIKUMLA japo alikubali everything except sex , lakini kuna muda mkichat anakuja then anatoka. SIKUTAKA na sitotaka ku hit and run nikaacha kumbkumb mbayaa. I believe in KARMA upandalo ndo uvunalo ,ngoja abaki na bikira yake watafaidi wengine.

HALI ILIVYOSASA.
Bado tunachat lakini ni kama vile best friends tu ,anantumia picha zake anaenjoy company yangu, SIFIKIRII kurudisha majeshi nyuma japo ye bado ananielewa.

PART 3 inakuja kuhusu dada yake sasa
 
Mshatufanya hatuna akili kilicho kushinda kumaliza ni nini
Kaka nilikuwa nikiandika sio kuwa niliondoka online hapana soma part 2 wakati naendelea kaundika sehemu ya mwisho
 
PART3 NA MWISHO.

Dada yake tumeanza fahamiana vizuri kutokana na kuwa ye ni mwalimu by professional. Hivyo wakati mwaka jana zimetangazwa ajira ,nikawa namsaidia kujaza jaza. Tukaendelea juana mdogomdogo japo mara nyingi kama sio zote yeye ndo huwa anapiga simu akiwa na shida zake namsaidia anasepa.

Status zake nyingi alizokuwa anapost ni za kama mtu anaeteseka na mapenzi na wakati mwingine anapost Bible verses na Vi cartoon.

Huyu dada kanipita miaka 3 au 2 na nusu hivi, si muongeaji, hasuki ,kwa ufupi ni Ndugu zetu wanaosali JUMAMOSI. Basi ikifika ijumaa kwake ndo maandaliz ya ibada yao nk

KUANZA MAHUSIANO.
Wakati Niko na date na mdogo wake nilikuwa nimeshaona ishara za dada mtu kunikubali lakini sikupenda kuwa mix dada na dogo. Nikijua si vizuri kwa imani yangu, japo dogo mtu alitaka mapenzi yetu yawe Siri na ni kweli kwa huyo dada mdogo kwao wakali na dada mtu ni mkali ukizingatia wamepishana kama miaka 5 au 4 hivi.

Huyu dada katika kumkwepa kwepa wee siku akanichana live UNAJUA THE GARANG mie nakukubal sema we hujiamini[emoji1], sikushangaa kwa kuwa nishaona alama tayari lakin ye asijue kwa muda huo natoka na dogo wake naye ningeaamua kumuunganisha ningeunganisha wote.

Story yake ya mahusiano ananambia ameadate na mtu mmoja japo suala la kuwa SEALED hakutaka nambiaa.
Kwa wakati huo alikuwa kwenye complicated relationship kwan huyo bf wake ,alimuomba dada ampe tunda dada akazngua jamaa nae akazilaa mazima. BASI dada akawa anaumia sabab alimpenda yule mkaka sana sana so machozi na macho yake yakawa ndo marafiki wakubwa sana. Kwa wakati huo akasema anampotezea jamaa na kuhamishia mapenzi kwangu rasmi.

Story ni ndefu siwezi weka kila kitu hapa.

Penzi letu lilishamiri sana full malove kama yotee wakati huo dogo yuko skuli hajui lolote linaloendelea huku na dada nae hajui kuwa nimetoka na dogo wake.
Basi ikifika kipind anaenda kanisan huko atahitaj nimpe ombi langu mojawapo akaniombee bila kusahau kuniombea masomoni afyaa kipindi corona iko fire pamoja na kuhusu Milo sahihi kama ujuavyo ndugu zetu wasabato nk

KITUMBUA KUINGIA MCHANGA.
1.Kutofanya follow up ya maongezi yetu, mtaongea kwa simu then akikuambia atakupigia ngoja apike au afanye jambo Fulani ,hiyo imeshatoka call it a day.

2.Kurudia rudia mambo anayokatazwa, kama namba moja inavosema. utamtext hapo asikujibu then akija siku ingine hajibu kile ulichomuuliza mwanzo anataka aendelee na mambo take.

3.Kutokana na suala la umri kuwa umeenda hata kesho yuko tayar kupata mtoto ilhali mie sina ramani inayosomeka.

4. Ni mdada jamii ya kina Joyce Kiria wale wanaokuwa fooled na ma seminar ya kuwajaza upepo kanisani. Anataka awe kwanza na pesa yake mambo yake yakaesawa then ndo mengine yaendele. inshort hataki sapooti ya kifedha akiamini nitamnyanyasa.

5. Imani tofauti, kuna siku ali doubt kuwa kama home watakubal kuoa MSABATO mie nkamwambia asijali ni matakwa yetu but for real nsingeweza kuwa na mwanamke tofauti na imani/dhehebu yangu/langu najua tungekuja kukosana mbele juu ya hili jambo kwan mifano halisi ipo.

6.Ukiachana na late replies nk pia Ukimtext Ijumaa jioni na jmosi hapo huwez wasiliana nae kwani ni muda wake wa ibada[emoji1] hadi atakapopata ye time. Mie kwa upande wangu nisingeweza hili jambo piaa hawezi safiri siku jumamosi HATA IWEJE.

By now hatujatamkiana rasmi tuachane ila naona kila mtu saivi na mambo yake, it is about a month hatujawasiliana na anahide view status last seen bluetick, hapost lolote sijue kani mute au ka futa namba yangu[emoji1]

Ni mengi ndugu zangu lakin kwa ufup ni hivyoo.


Nawasalimu kwa jina la JF, shuhuda ziendelee.

MWISHO
 
Hii mistake niliifanya nimemaliza secondary kula dada na mdgo wake but walikuja kujuana wakaelewana waniache wote dogo mtu akapata mimba baadae af sister mtu akachukulia advantage ya kuendelea na mimi kisiri zile za kulana kimasihara😁.

Nilisema sita rudia hii tabia lakn wakati wakati nimemaliza advance ikatokea tena inshu kama hiyo wakat wa kuapply vyuo mtu na mdgo ake but mama tofauti baba mmoja waliingia target wote na kimasihara mchezo nilicheza vyema mpka leo awajui ila wanahisi hisi tu
 
Hii mistake niliifanya nimemaliza secondary kula dada na mdgo wake but walikuja kujuana wakaelewana waniache wote dogo mtu akapata mimba baadae af sister mtu akachukulia advantage ya kuendelea na mimi kisiri zile za kulana kimasihara[emoji16].Nilisema sita rudia hii tabia lakn wakati wakati nimemaliza advance ikatokea tena inshu kama hiyo wakat wa kuapply vyuo mtu na mdgo ake but mama tofauti baba mmoja waliingia target wote na kimasihara mchezo nilicheza vyema mpka leo awajui ila wanahisi hisi tu
[emoji1][emoji1][emoji1]ulicheza kama peleee
 
Back
Top Bottom