Dada wa kazi adaiwa kuua mtoto wa mwajiri wake

Dada wa kazi adaiwa kuua mtoto wa mwajiri wake

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyakazi wa ndani, Ashura Suka kwa tuhuma za kumuua mtoto mdogo wa mwajiri wake.

Akizungumza na HabariLEO jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema tukio hilo ni la Agosti 23 mwaka huu saa 10:30 usiku katika Kata ya Iloganzala wilayani Ilemela.

Alisema mtoto mwenye umri wa miezi 11, Kelvin Kastus, mkazi wa IIoganzala, aliuawa kwa kuzibwa pumzi kwa kutumia shuka na mfanyakazi huyo wa ndani mwenye miaka 15 ambaye ni mkazi wa Nyamanoro.

Muliro alisema chanzo cha mauaji hayo, kinachunguzwa na upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure kwa uchunguzi wa daktari.

Aliwaka wazazi na walezi wenye watoto wadogo, kujenga utamaduni wa kuajiri watu wanaowafahamu tabia, mienendo na malezi, kwani ni hatari kumwachia mtu usiyemfahamu vizuri akulelee mtoto mdogo.
 
Oh poleni wazazi...Pia kuajiri umri wa miaka 15(under 18) Ni kosa pia
Maana hajafika level ya kujitambua kimajukumu
 
Hiyo saa 10:30 usiku mzazi alikuwa wapi? Au mtoto analelewa na mfanyakazi hadi mida ya usiku?

Wazazi tuwajibike.
 
Ishi na mfanyakazi wa ndani kirafiki ukijua unawatoto ndani. Mnanyanyasa watoto wa watu alafu unataka amlee mtoto wako vizuri. Mnapenda kuishi na wafanyakazi alafu wachoyo wa chakula ndani, ww ule nyama mfanyakazi ajipikie matembele
 
Na nyie waajiri achen kuwanyanyasa wadada wa kaz ishin nao kama ndugu na siyo watumwa
 
Sijajua huyo mtoto kulala na binti wa kazi mama alikuwa wapi. Je mama ni nesi alikuwa shifti ya usiku au ni nini kilisababisha mtoto alale na huyo msaidizi wa nyumbani.

Kama mama ni nesi , kwa asili ya kazi yake alitakiwa awe na msaidizi wa nyumbani ambaye ni mkubwa kidogo kwa umri au aliyezaa kabisa ili kuhimili usimbufu wa mtoto usiku pindi anapokuwa yupo shifti ya usiku. Huyo binti aliyeua (miaka 15) ni mdogo sana kuachiwa jukumu la kumlea mtoto mchana na kulala naye pia. Japo kitendo alichokifanya ni kibaya sana kwa malaika asiye na hatia.

Wazazi hasa kinamama, hili jambo ukilichunguza sana utakuta sababu ni mama mwenyewe kutokuwa makini na malezi ya mtoto wake bila kujali umri wa binti anayeachiwa jukumu la kumlea mtoto.

Kwangu mimi hata huyo binti mwenyewe bado ni mtoto pia, je anaweza kuhimili vipi changamoto za malezi ya mtoto peke yake wakati mama hayupo nyumbani?
 
Kama msichana wa kazi ana akili timamu (sio mgonjwa wa akili) na unaishi naye vizuri kwa kumpa mahitaji yake kwa wakati, sidhani haya tunayoyalaani yangekuwa stori kwenye jamii.
 
Haya MATUKIO ni matokeo ya matendo ya hao maboss wao.
 
Serikali na sekta binafs liangalie hil wazaz waruhusiwe kwenda kazin na mtoto ila kuwe na kituo maalumu cha kulelea karib na ofisi. Ajira hamna ila zipo mtu waweza kufungua kituo kwa kuwashkia wazaz watoto wao wakitoka kazin wanawafata
 
Habari ya kusikitisha sana.Najiuliza huo usiku wazazi wote walikua night au inakuaje mana tukio limetokea alfajiri
 
Mfanyakazi wa miaka 15 ni mdogo hasa kwa majukumu ya kulea mtoto maana ye mwenyewe akili zake za kitoto. Ila kitendo cha kuua ni kukosa utu
 
Wasaidizi wa ndani, unaweza kumpenda kama mwanao na bado akakufanyia vituko! Wasio na experience ndo watashangaa! Kwa binadamu wa kawaida, hata ukiumizwa vipi, si sababu ya kuua kiumbe mdogo namna ile asiye na kosa! Huyu ana roho ya mauaji tu hata akipendwa na hata akiwa mkubwa! Ukute mama alikuwa shift ya kazi, labda nesi au hata kazi yoyote ile! Tusiwe wepesi wa kuhukumu, wakati hatujui hali halisi ya mahali pa tukio.
 
Bado haitoshi kumtia hatiani mfanyakazi wa ndani,,
pengine mtoto alikufa kwa mapenzi ya MUNGU ,,lakini sababu kimetokea akiwa na mfanyakazi tayari ni tatizo,,,
Mtoto achunguzwe na haki itendeke,,
Asiangushiwe house girl jumba bovu..
Na wazazi wa mtoto iweje wamuache mtoto mdogo wa miezi 11 alale na house girl,
Wao walikuwa na shughuli gn kwa muda huo..
 
Back
Top Bottom