Dada wa kazi atoweka na watoto wawili mara baada ya kwenda dukani

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mohammad Kassim ambaye ni Baba Mzazi, ametangaza kupotelewa na Watoto wake wawili ( wanaoonekana pichani ), ambao wamepotea jana jioni majira ya saa kumi na mbili maeneo ya Temeke Jijini Dar es salaam wakiwa na Dada wa Kazi.

Akizungumza Kassim amesema Dada huyo wa kazi ambaye jana ilikua ni siku ya tatu tangu kuanza kufanya kazi kwenye Familia hiyo, aliondoka na Watoto hao akiaga kuwa anakwenda nao Dukani lakini wakatokomea moja kwa moja.

Soma Pia:
“Aliowachukua Watoto ni Dada wa kazi aliyekaa nao kwa siku tatu tu, inaonekana kuiba Watoto ndilo lilikua lengo lake kwasababu baada ya kutokomea simu yake haipatikani na hata wale waliomuunganisha kupata kazi kwetu nao simu zao hazipatikani, tunaomba Watanzania watusaidie kusambaza taarifa hizi” - Kassim ameiambia AyoTV.

“Tunaomba yeyote mwenye taarifa za Watoto hawa aende Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nae au anipigie kwa namba yangu 0744-555-574” - Kassim.

Screenshot 2025-01-13 170315.png

Soma: Watoto walioibwa na dada wa kazi wapatikana kwa mganga Dar
 
Hivi kwanini mtu ateke watoto?

Watoto wana thamani gani, wanauzwa, wanatolewa viungo ama nini?
 
Mohammad Kassim ambaye ni Baba Mzazi, ametangaza kupotelewa na Watoto wake wawili ( wanaoonekana pichani ), ambao wamepotea jana jioni majira ya saa kumi na mbili maeneo ya Temeke Jijini Dar es salaam wakiwa na Dada wa Kazi.

Akizungumza na @AyoTV_, Kassim amesema Dada huyo wa kazi ambaye jana ilikua ni siku ya tatu tangu kuanza kufanya kazi kwenye Familia hiyo, aliondoka na Watoto hao akiaga kuwa anakwenda nao Dukani lakini wakatokomea moja kwa moja.

“Aliowachukua Watoto ni Dada wa kazi aliyekaa nao kwa siku tatu tu, inaonekana kuiba Watoto ndilo lilikua lengo lake kwasababu baada ya kutokomea simu yake haipatikani na hata wale waliomuunganisha kupata kazi kwetu nao simu zao hazipatikani, tunaomba Watanzania watusaidie kusambaza taarifa hizi” - Kassim ameiambia AyoTV.

“Tunaomba yeyote mwenye taarifa za Watoto hawa aende Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nae au anipigie kwa namba yangu 0744-555-574” - Kassim.

View attachment 3200914
Mungu tusaidie Jamani Daaa!
 
Mohammad Kassim ambaye ni Baba Mzazi, ametangaza kupotelewa na Watoto wake wawili ( wanaoonekana pichani ), ambao wamepotea jana jioni majira ya saa kumi na mbili maeneo ya Temeke Jijini Dar es salaam wakiwa na Dada wa Kazi.

Akizungumza Kassim amesema Dada huyo wa kazi ambaye jana ilikua ni siku ya tatu tangu kuanza kufanya kazi kwenye Familia hiyo, aliondoka na Watoto hao akiaga kuwa anakwenda nao Dukani lakini wakatokomea moja kwa moja.

Soma Pia:
“Aliowachukua Watoto ni Dada wa kazi aliyekaa nao kwa siku tatu tu, inaonekana kuiba Watoto ndilo lilikua lengo lake kwasababu baada ya kutokomea simu yake haipatikani na hata wale waliomuunganisha kupata kazi kwetu nao simu zao hazipatikani, tunaomba Watanzania watusaidie kusambaza taarifa hizi” - Kassim ameiambia AyoTV.

“Tunaomba yeyote mwenye taarifa za Watoto hawa aende Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nae au anipigie kwa namba yangu 0744-555-574” - Kassim.

View attachment 3200914
Weka namba ya simu ya huyo dada na namba ya simu ya dalali aliyemuunganisha, atapatikana.
 
Kwahiyo hao waliomleta ni watu ambao anafahamiana nao kwa simu tu?

Okay TCRA wafuatilie mawasiliano ya mwisho aliyofanya huyo dada. Na pia picha yake huyo dada iwekwe.
 
Alafu vidada vya hivyo vinajifanyaga vinajua dini hivyo

Kila dakika salamaleko na ushungi juu kumbe vizi tu

Pole sana kwa Baba na Mama waliopotelewa na watoto
 
Back
Top Bottom