KERO Dada yangu amefariki kwa kuishiwa Oxygen baada ya Muhimbili kufosi kumpeleka Mloganzila

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwanza nitoe Pole kwa mtoa mada ila kwa mujibu wa maelezo yako hapo hao madaktari hawana kesi. Wenye kesi ni hao wanaohusika na ambulance na huyo nesi .Daktari hahusiki na kuangalia ambulance kama haina oksijeni kila mtu hospital ana majukumu yake
 

Ukipata mwanasheria mzuri, utawanyoosha vizuri sana, na fidia juu, usiwaache hao washenzi, yaani una vithibitisho vyote, hakika unaweza kuvitumia ili kuwasaidia watanzania wengine ili uzembe huu husijirudie, narudia tena tafuta mwanasheria, kesi ushashinda hii na somo watapata.
 
Sijui tunakusaidiaje mtu ambae unasema mwenyewe siku ya dada yako ilikuwa imefika, na hata ufanyeje huwezi kumrudisha.

Una li imani kama hilo, unalalamika nini sasa, tunakusaidiaje ?
 
Mimi ,wewe mtoa post, na binadamu wengine wote tutafariki tu. Lakini ikitokea mtu anafariki kwa uzembe wa mtu kama ulivyo eleza hapo juu inapaswa awajibishwe ili iwe funzo kwa wengine wenye tabia kama izo. HAKI ITENDEKE😡
 
Tukio ilikua ni MNH? au hospital nyingine?
 
TLS IPO KWA AJILI YAKO,

MUONE MWAMBUKUSI ,

NDIYO HAWEZIKURUDISHIWA UHAI WAKE,

LAKINI DADA YAKO ALIKUWA NA WANAOMTEGEMEA NANI ATAWATUNZA?

FIDIA YA MALIPO INAHUSIKA
 
Pole ndugu,ila kumbuka cancer ikifikia stage kubwa kifo hakiepukiki. Kwa hiyo kama mgongwa amekufa kwa kukosa oxygen ni obviously alikuwa stage mbaya kiasi kwamba hata angebaki hapo muhimbili asingesurvive muda mrefu. Nadhani ocean road ilitakiwa wawape counselling nzuri juu ya mgonjwa wenu.
 
Poleni sana mkuu, hili swala ungelifikisha mahakamani iwe fundisho kwa madaktari wengine,
Vitu vyengine wanapenda kujifanya wao ndo wataalamu na hawataki kusikiliza ushauri wa mtu.
Mungu awatie nguvu ndugu zetu🙏
 
Pole sana ndugu, kwakweli ni uzembe wa hali ya juu sana. Mambo ya kusema hii sio kazi yangu yapo sana serikalini, ikitokea mtu anafanya uzembe basi wangine wanamwangalia tu eti kwakuwa sio kazi yao.

Serikali iwawajibishe watu hapo kwa huo uzembe.
 
Daah! Poleni sana lakini mngeenda mamlaka husika hapo Muhimbili na kuwasilisha malalamiko yenu na hao wahusika kama ingebainika kweli walifanya uzembe hadi kifo kutokea wangewajibishwa.
Hakuna cha kuwajibishwa washenzi sana wale system nzima ya pale IPO corrupted usipotanguliza rushwa au uwe na connection inakula kwako.
 
Pole sana mkuu,kuna vitu vinaumiza sana,hivi katika situation kama hii mtu akijichukulia sheria mkononi ukamcharaza ngumi za kutosha daktari mmoja utakuwa umetenda kosa...
 
Mkuu' pole sana Boss wangu kwa kuondokewa na mpendwa wako....

Usharudi tu' ni kwamba unaweza kuwa kwenye changamoto, namaanisha kwasababu ya tatizo lililotokea lakini jitahidi sana kuwa mtu wa kutunza usiri uliopewa na taasisi lakini kutunza usiri wa mpendwa wako ....

Kuachia Documents hewani namna hiyo 😳 si sawa hata kidogo
 
Saratani ilikuwa imefikia hatua gani?
Hata kama saratani ilikuwa ni hatua mbaya sana,njia iliyotumika kumondoa marehemu ni ya kikatili sana,hakuna kitanda,wakati hela ilishatolewa,vipi kuhusu swala la Oxygen nalo kwanini isiwekwe ya kutosha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…