Dada yangu ameniambukiza UKIMWI na hataki tena kunisaidia

Dada yangu ameniambukiza UKIMWI na hataki tena kunisaidia

Mimi ni Binti wa miaka 23, ni mwanafunzi wa mwaka watatu chuo, nilikua naishi kwa dada yangu ambaye ndiyo alianza kunisomesha tangu nilipomaliza kidoago cha sita baada ya wazazi wangu kufariki. Baada ya kuja kwa dada iniliona tabia mbaya za shemeji, alikua hahudumii chochote, anampiga sana dada na kila kitu anafanya dada, mpaka ada za watoto, shemeji alikua akimuomba pesa akikataa anampiga.

Nilikaa nikiwa chuo mwaka wa kwanza mwishoni mwishoni shemeji alikuja kwangu, akaanza kuniambia ni kwanini anampiga dada yangu, alikua ananiambia kuwa anmapigakwakua dadayangu ni mkorofi, kiburi na ni mchawi anamloga ndiyo maana hafanikiwi. Aliniambia mambo mengi ya Dada ambayo yalinifanya ni mchukie dada,a kaniambia anataka kutoa pesa lakini dada yangu hataki kwani ni mchawi.

Nilijikuta nakua karibu na shemu mpaka tukaanzisha mahusiano, akawa ananipenda ikafikia hatua tunafanya mambo waziwazi, dada alijua tukawa tunagombana lakini shemeji ndiyo alikua ni kila kitu akawa anampiga ananyamaza. Sasa mwaka jana mwezi wa nane nilipata ujauzito, shemeji aliniambia nibebe mimba kwani ananipenda na anataka mtoto na mimi.

Kweli nilibeba mimba, lakini nilipoenda kupima kiliniki nikaambiwa kuwa nimeathirika hivyo nianze kutumia dawa, nilichanganyikiwa ila nilipomuambia shemeji hakujali. Nilimuambia dada akaishia kuniambia kuwa mbona yeye kaathirika muda tu anatumia dawa shemeji ndiyo aligoma kutumia dawa.

Niliumia sana kwani dada yangu kaniambukiza UKIMWI makusudi, alijua kuwa mume wake anaumwa lakini hakuniambia. Shida nyingine Kaka nikuwa Dada yangu kaondoka hapa nyumbani katuachia nyumba mimi na shemeji, nyumba ina jina la dada na ina hati kabisa, shemeji alitaka kuiuza lakini akashindwa, sasa shemeji hana pesa amekua mtu wa hasira.

Kaka natakiwa kulipa ada ya chuo nililipa kidogo lakini sasa hivi shemeji hana pesa na dad ahataki kunilipia na nimjamzito, nisaidie kaka uongee na dada yangu umuambie kuwa nimejutia kwani sina namna. Kaka yeye ndiyo anatakiwa kunisaidia kwani ni kama yeye ndiyo aliniambukiza, alijua mume wake ana UKIMWI lakini hakuniambia, najua nimemkosea Kaka lakini nayeye amenikosea kwani mimi ni mdogo wake alipaswa kunilinda.

NB: Mnaoishi kwa ndugu zenu tulieni, ukiona mpaka shemeji yako kakutongoza basi jua kuwa huyo ni mshenzi wa washenzi, aisee hivi visa vimekua vingi sana. Najua wakati mwingine ni ngumu kukataa mkishasikia pesa ila jithaminini, hao wanaume ni washeni, yakiwakuta wanawaacha na aibu halafu hamna kitu, visa hivi ni vingi mpaka basi, aisee mnawakatisha tamaa ndugu zenu kuwasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pumbauu kweli wewe!! Ndio mambo ya kengeza kuita chongo kisa umependa? Kafie mbele huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uliliwa kimasihara.
Angalizo:wadogo wa wake zetu rahisi sana ku date nao.
 
Hii ndiyo mshahara wa kutembea na mume wa Dada yako ako. Umejiambukiza mwenyewe wala siyo dada yako.
 
Ulijua unamkomoa dada yako eeghh? Tamaa mbele mauti nyuma. Mtu mmezaliwa na kukua pamoja, huo uchawi kautoa wapi?? University Student? Naomba supu ya konglo nongeze nguvu
 
Nilidhani ni mimi tu nikiyechanganywa na hizi kaka, dada, kumbe ni wengi

Mwaka wa pili/tatu chuo kikuu huyo
Mara dada mara kaka mara shemeji..yaani full mvurugano..A university student!! Jesus christ

Anyway,stori inafundisha kuwa usipende kulindwa wakati wewe kulinda hupendi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jinga sana sana kwa nini huutaki ukimwi sasa?
 
virusi vinamchanganya mtima
Mara dada mara kaka mara shemeji..yaani full mvurugano..A university student!! Jesus christ

Anyway,stori inafundisha kuwa usipende kulindwa wakati wewe kulinda hupendi
 
Dada ndio kakuambukiza? Acha iendelee tu kuwa ni hadithi....
 
Mimi ni binti wa miaka 23, ni mwanafunzi wa mwaka watatu chuo. Nilikua naishi kwa dada yangu ambaye ndiyo alianza kunisomesha tangu nilipomaliza kidato cha sita baada ya wazazi wangu kufariki. Baada ya kuja kwa dada iniliona tabia mbaya za shemeji, alikua hahudumii chochote, anampiga sana dada na kila kitu anafanya dada, mpaka ada za watoto, shemeji alikuwa akimuomba pesa akikataa anampiga.

Nilikaa nikiwa chuo mwaka wa kwanza mwishoni mwishoni shemeji alikuja kwangu, akaanza kuniambia ni kwanini anampiga dada yangu, alikuwa ananiambia kuwa anamapiga kwakuwa dada yangu ni mkorofi, ana kiburi na ni mchawi anamloga ndiyo maana hafanikiwi. Aliniambia mambo mengi ya dada ambayo yalinifanya ni mchukie dada; akaniambia anataka kutoa pesa lakini dada yangu hataki kwani ni mchawi.

Nilijikuta nakuwa karibu na shemu mpaka tukaanzisha mahusiano, akawa ananipenda ikafikia hatua tunafanya mambo waziwazi. Dada alijua tukawa tunagombana lakini shemeji ndiyo alikuwa ni kila kitu akawa anampiga ananyamaza. Sasa mwaka jana mwezi wa nane nilipata ujauzito, shemeji aliniambia nibebe mimba kwani ananipenda na anataka mtoto na mimi.

Kweli nilibeba mimba, lakini nilipoenda kupima kiliniki nikaambiwa kuwa nimeathirika hivyo nianze kutumia dawa. Nilichanganyikiwa ila nilipomuambia shemeji hakujali. Nilimuambia dada akaishia kuniambia kuwa mbona yeye kaathirika muda tu anatumia dawa shemeji ndiyo aligoma kutumia dawa.

Niliumia sana kwani dada yangu kaniambukiza UKIMWI makusudi, alijua kuwa mume wake anaumwa lakini hakuniambia. Shida nyingine ni kuwa dada yangu kaondoka hapa nyumbani katuachia nyumba mimi na shemeji, nyumba ina jina la dada na ina hati kabisa, shemeji alitaka kuiuza lakini akashindwa, sasa shemeji hana pesa amekua mtu wa hasira.

Kaka natakiwa kulipa ada ya chuo nililipa kidogo lakini sasa hivi shemeji hana pesa na dada ahataki kunilipia na ni mjamzito, nisaidie kaka uongee na dada yangu umuambie kuwa nimejutia kwani sina namna. Kaka yeye ndiyo anatakiwa kunisaidia kwani ni kama yeye ndiyo aliniambukiza, alijua mume wake ana UKIMWI lakini hakuniambia, najua nimemkosea kaka lakini na yeye amenikosea kwani mimi ni mdogo wake, alipaswa kunilinda.

NB: Mnaoishi kwa ndugu zenu tulieni, ukiona mpaka shemeji yako kakutongoza basi jua kuwa huyo ni mshenzi wa washenzi, aisee hivi visa vimekua vingi sana. Najua wakati mwingine ni ngumu kukataa mkishasikia pesa ila jithaminini, hao wanaume ni washenzi, yakiwakuta wanawaacha na aibu halafu hamna kitu, visa hivi ni vingi mpaka basi, aisee mnawakatisha tamaa ndugu zenu kuwasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dada yako hajakuua... we si umesema kua ukikua na mahusiano kisiri siri then mkaweka wazi... so may be hata angekuambia angekua kachelewa.....
IMG-20200120-WA0002.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom