Dada yangu anakaribia kuolewa na Tapeli, Nichukue hatua gani?

Dada anatoa pesa kulipa bills zote. Mpaka hapa unahisi dada yako hajui ukweli wa huyo bwana mkubwa?.

Mimi nahisi dada yako anaujua ukweli ila kwakua umri umesogea (age go) kajichukulia Kijana wake wafanye maisha kwaiyo wewe nyamaza tu!
 
dada kapenda kaka anaona wivu, kama hutaki aolewe na huyo jamaa muoe wewe?
 
Kisa chako kinafanana na cha dada yangu ya kwanza ,naye alikutana na tapeli ambaye alionywa kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano deep na kuzaa naye ,tena alionywa na binamu yetu wa kike,alionywa na marafiki zake wa kike kuwa huyo mtu aliyenaye ni tapeli lakini hakusikia,badala yake aliwaona wanaomshauri na kumuonya kama ni maadui na hawamtakii mema.

1)uongo wa kwanza ni kumdanganya hana familia hana mke hana watoto..kumbe ana watoto amezaa na wanawake wengi mbali mbali na kuwatelekeza na pia ana famili mke na watoto mkoa mwingine.

2)uongo wa pili ni kumdanganya anafanya kazi ,kumbe alitumbuliwa vyeti feki hana kazi

3)uongo mwingine ni kuazima gari kwa watu wake na kumleta nalo nyumbani kujifanya ni gari lake.
b) kwenda kumuonyesha site nyumba ya mtu akimuaminisha ni site yake nyumba yake anajenga ikiisha wahamie .

4)KIMTAPELI PESA yani dada JACK kweli unachukua hela kwa mama,unamuomba mama hela aliyovunja vikoba akakupa MILIONI KUMI na hela nyingine mbali mbali mama anakupa unaenda kuhonga mwanaume,badala mwanaume akuhonge wewe wewe unahonga mwanaume????
Jamaa linamdanganya sista alipe hela wamalizie kujenga hiyo site wahamie kumbe site hewa kumbe kiwanja cha mtu mjengo sio wake HUYU JAMAA TAPELI anamwambia dada ampe hela washirikiane kujenga hiyi nyumba site ili wahamie na dada jack anaenda kumpanga mama ampe hela kwa ajili ya kufanya biasahara mama anakomaa anampa hela dada jack,kumbe dada jack analipekekea lijamaa.

5)Baba alivyostaafu alinunua nyumba kadhaa nyumba moja alimpa dada jack akae na hakumwambia kwamba amempa ila alimwambia amempangisha alipe kodi,pia nyumba imepakana na barabara ya mtaa na nyumba mbele ina fremu dada jack alifungiliwa biashara ,JAMAA LIKAHAMIA kwa dada jack yani mwanaume anakaa na kuishi nyumba ya ukweni nyumba na wakala mtajibwa biashara ikafa.

6)Pamoja na hayo maujinga yote ila dada Jack ndio akawa hasikii anashauriwa na wanawake wenzake binamu na marafiki zake hasikii badala yake akawachukia wote wanaomshauri akabeba na mimba akazaa jamaa hana msaada anategemea dada jack aombe hela nyumbani kutoka kwa biashara za mama na baba ndio amuhudumie mwanaume wake aliyemfuga ndani.

7)Jamaa kazi yake ni kupiga picha akiwa ndani ya ndege anampanga sista kuna mchongo anausikilizia sista anaposti picha za jamaa yake eti kapanda ndege ana mishe mishe sijui picha za photos studio?mara jamaa liseme linataka kuinunua nyumba ya baba hiyo anayokaa jack amrudishie baba hela aliyoinunulia linunue na sista kama nyumbu ana amini kila uongo anaoambiwa na lijamaa,
MWISHO WA SIKU mtoto waliozaa na lijamaa ikabidi dada jack ampeleke nyumbani kwa mama ,yani wanazaa huko nje WANAENDA KUMRUNDIKIA MAMA watoto awalee.Na baba alivyostaafu aliwapa masista wote mitaji kama milion 10 kumi ila hakuna walichofanya zaidi ya kwenda kuhonga wanaume.Na bado wao na waume zao na watoto wao wanategemea mama na baba ndio awalee...na bado wanazidi kuzaa na kuleta watoto kwa mama awalelee.

Mwisho wa siku ilibidi baba aende kumfukuza yuke jamaa amtoe kwenye nyumba yake akimwambia JACK kama hutamuondoa hapo kwenye nyumba yangu huyo jamaa yako KESHO NAKUJA KUMTOA NIFUNGE nyumba yangu ,ndio jamaa likaondoka baada ya kumtapeli sista pesa nyingi.

NA BADO DADA JACK anliposti yani bado anlipenda .

CONCLUSION
Nilichojifunza WANAWAKE wamegawanyika katika MAKUNDI MAWILI kuna WENYE AKILI na KUNA WASIO KUWA NA AKILI.Wasiokuwa na akili ndio wengi kuliko wenye akili(nikisema wasiokuwa na akili namaanisha wanaofanya mambo yao kwa kifuata HISIA ZAO NYEGE KULIKO AKILI kuna wenye uwezo wa kufanya maamuzi yako kwa kuongozwa na akili sio hisia (YANI wapo wanawake wenye akili hawa ni wachache sana sana)na kama mwanamke hana akili HUWEZI KUMBADILISHA hata umshauri nini hawezi kubadilika kwa sababu HUO NI UGONJWA WA AKILI(TATIZO LIPO kwenye ubongo wake ,huwezi kumuumba upya wewe sio Mungu.
DAWA NI KUMUACHA AFUNZWE NA DUNIA.
 
mwanamke kama anakupenda ata umfanyie kitu gani kibaya unampiga sound kidogo basi anajaa, unachotaka kukifanya kitakutia aibu mwanawane. hawa dada zetu huwa wanaamini hisia zao kuliko ushauri hata kama dunia nzima itakua haiko upande wao

mambo ya watu walokwisha onana nyeti zao kaa nayo mbali utaonekana mchawi, usije sema hukuambiwa
 
Ngoja akuletee mjomba mwingine
awe singo maza pro
duh
 
NAKUBALIANA NA WEWE KWA 100%
1) Hata katika KUOA ukioa mwanamke ALIYEKUPENDA YEYE au a ayekupenda yeye zaidi kukuliko,ndoa kwa asilimia kubwa itakuwa na afya itastawi.
ILA UKIOA mwanamke ambaye hakupendi kivile kama wewe unavyompenda yeye yani moyoni mwake kuna NAMBARI moja yake wewe ni namba 2,3,...
Ndoa inaweza ikawa na machungu,kwa sababu moyoni mwake haupo labda amekukubali kwa sababu ya dhiki tu au material things au sababu kadhaa.
ILA UKIOA ANAYEKUPENDA YEYE kwa moyo wake wote...(ATAKUVUMILIA SANA). labda mambo ukiharibu sanaa kama JK alivyosema labda mambo yakiharibika sanaa ndio atashindwa kuvumilia ...ni tofauti na ambaye hakupendi hana uvumilivu na subira sana.
 
pesa si zako zinakuuma nini mkuu au hukupewa mgao na mzee? kila mtu na matumizi yake

CONCLUSION: Wanawake hawana akili linapokuja suala la mapenzi
 
sema vijana mnaotegemea pesa za wanawake kutamba kitaa mna roho ngumu sana kuliko nyamasingisi
 
Kwahiyo niko makini sana kwenye kujua nani ni nani na ninavyodeal naye nideal naye kwa angle gani.
Mkuu, sasa kuna haja gani ya kuja kutusumbua wakati unazijua angle zote za kushughulika na watu kama hao.
 
Oyaa mpange sister kabla hajarogwa damu yako io mkuu
 
pesa si zako zinakuuma nini mkuu au hukupewa mgao na mzee? kila mtu na matumizi yake

CONCLUSION: Wanawake hawana akili linapokuja suala la mapenzi
PESA ZA MAMA mama yetu mzee anatafuta pesa zake kwa shida kwa biashara ndogondogo halafu sista anakuja kumlaghai mama anampa pesa hizi milioni mbili mbili tatu,mara kadhaa anapewa na mama HALAFU dada Jack analipelekea lijamaa.
Bado lijamaa limekula mgao wa dada ile milioni 10 ya baba alivyogawa kwa wototo baada ya kustaafu,na ile milioni 10 ya mama alivyovunja kikoba kwa wakati tofauti.
Na bado mtoto wao waliozaa wamemleta kwa mama amlee.
Na bado hela za matumizi wanachukua kwa mama ,yani mizinga mingi dada jack anaomba kwa mama na baba kwa ajili ya kilipa lijamaa.
Biashara aliyofunguliwa wamekula mtaji na lijamaa lake dada jack hana biashara wamekula mtaji.
Bado na nyumba ya baba linakaa humo humo wanzalia mtoto humo humo kwe nyumba ya baba.
Bado linamdanganya mauongo kuwa linajenga ili na kwwnda kumuonyesha SITE HEWA kwamba nyumba inakaribia kuisha wahamie akazane kutafuta hela wamalizie nyumba kumbe site sio yake .
Bado lina familia huko Arusha na hapo mkoani limezalisha wanawake wengine kadhaa likiwatapeli kwa .
Halifanyi kazi yoyote lilitumbukiwa vyeti feki sawa lakini halijushughulishi na kazi yoyote zaidi ya kutapeli wanawake .
BADO DADA JACK analingangania NA KUONYWA KABLA HAJAZAA NALO na alionywa na binamu zake wa kike na marafiki zake wa kike ila dada jack akawachukia wote waliomshauri.
HANA AKILI KWA SABABU HAJIFUNZI
Mtoto wa kwanza pia alizalishwa nyumbani na mwaru koko ,analelewa nyumbani,mara ya pili kakutana na hili tapeli tena hajifunzi anazidi kurundika watoto nyumbani mama awalee na kumtia hasara mama awahidumie yeye na lijamaa lake

MAGONJWA NI MENGI lijamaa likimiambikiza magonjwa linapotea ndugu ndio watakao muuguza.

SIJUI KWA NINI BAADHI YA WANAWAKE hawana akili hata kidogo hata chembe ..ni kama nyumbu unajua kabisa kwamba unatapeliwa unadanganywa lakini bado unaenda unaelekea kibla uchinjwe vizuri.

NI HERI UKOSE MALI KULIKO KIKOSA AKILI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…