Dada yangu anakaribia kuolewa na Tapeli, Nichukue hatua gani?

Hivi huyu ndio wewe au.
 
Ulizingua tu kumrekodi mzee, sio poa kumrekodi mtu akilewa. Ni umbea sa kishamba sana.

Mwisho wa siku ili kuendelea kua sawa na sister wako muache bila kumwambia kitu, ajionee mwenyewe.
 
Mkuu sasa kama wewe kijana wa kiume kwanini uliendelea kufumbia macho mambo yote hayo, ulitakiwa wewe kijana ndiyo uwasaidie Wazazi wako kwa kuanza kuwatimua nyumbani hao Wajomba zako.
 
hahahahahahhahaha dada jack katishaaaaaaaaa holaaaaaaaaa!
 
hahahahahahhahaha dada jack katishaaaaaaaaa holaaaaaaaaa!
 
Mkuu hiyo chai.. Mbichi. Kwa sasa Tusker lager haipo Tanzania. Mimi nilikuwa mnywaji mkubwa wa hiyo beer kwa faida yako tu niliwahi kwenda hadi SBL kuhoji hapo kabla ilikuwa TBL. Nazungumzia miaka mitano nyuma. Wewe leo hii umeipata wapi?!!!
 
Huenda sista kapenda hizo swaga za jamaa. Muoneshe kavideo, waeleze na wakwe zake, ila uamuzi wa kuolewa muachie sista ako, kwani unaolewa ww?
 
Mkuu sasa kama wewe kijana wa kiume kwanini uliendelea kufumbia macho mambo yote hayo, ulitakiwa wewe kijana ndiyo uwasaidie Wazazi wako kwa kuanza kuwatimua nyumbani hao Wajomba zako.
SIWEZI kumfukuza mwanamume wake siwezi kutumia nguvu kwenye kuingilia kumfukuza kwenye nyumba ya baba wakati wazazi wenyewe wapo hai.
Mke wangu wifi yake dada amemshauri,binamu yetu wa kike amemshauri na marafiki zake wa kike wamemshaurib,huu ushauri anatakiwa ashauriwe na wanawake wenziwe na WAZAZI ambao wapo hai.
Kwanza shule tu walizingua kusoma wakaona shule haina maana wao ni warembo wanawake wazuri haina haja ya wao kusoma eti WATAOLEWA kwamba kuna mwanaume atakaye waoa ndio ANAWASOMEA wao wataolewa tu,tena wakasema mbona mama hakusoma na hana ajira ya serikalini lakini akaolewa na baba msomi na muajiriwa na wao wataolewa tu.
Wamesomeshwa shule nzuri za private za gharama na kitumiwa pesa za matumizi na kupelekwa matwisheni na mzee alikuwa tayari kuwasomesha hata kenya au uganda kama wangekuwa tayari kusoma,ila wakazingua huko boding badala ya kusoma kumbe wanaendekeza mapenzi wakaishia kupata div 0 O level ambayo haina hata cheti.
Biashara wamepewa mitaji wamehonga wanaume.
KUZALIA nyumbani na kumrundukia mama watoto wao waliozaa na majama huko mtaani,mama awalee watoto wao ndio kama wanashindana hivi.

WATAFUNZWA NA DUNIA .
Mimi nawa angalia tu,namuonea huruma mama yangu anateseka badala ya kupumzika ale uzew wake ila ndio anapambana kulea wajukuu na watoto.ILA MAMA naye anapenda hata baba naye anapenda wajukuu zake.
WAZAZI wenyewe ndio wanawadekeza,mimi siwezi kuingilia nikaonekana mbaya bure,mi naangalia tu nanyamaza kimya napita hivi napambana na mimi na mambo yangu binafsi na ya familia yangu.
Nilichofanikiwa ni kuwapeleka kwenye maombi kwa mchungaji LAIZER wakaombewa na huwa nawaombea nikipata muda ili Mungu aliyewaumba awasaidie.

SIDHANI KAMA UPUMBAVU una dawa,bora ujinga mtu akielemisha ujinga unaondoka ila upumbavu Mwalimu Nyerere alisema upumbavu ni kipaji ni kama urefu na ufupi.UPUMBAVU hauponi hauondoki mana mpumbavu anajua sio mjinga anajua kuwa anadanganywa anatapeliwa lakini bado anaenda hapo hapo.Ni kama nyumbu analiwa na mamba lakini bado wanaenda hapo hapo hata kama wanaona mwwnzao analiwa NYUMBU.
 
Vunga kwanza mzee...wakat wanatafutana ww hukuepo
 
dada lucy naye aliolewa huko moshi yani sio ndoa alipomaliza chuo cha ualimu wa chekechea hakurudi nyumbani akabaki kwq mumewe kijana.(boda boda na muuza mitumba)
Yule kijana akawa anampiga sana ,akampokonya cheti hataki afanye kazi wivu wa mapenzi,
anavuta mabangi anampiga kweli hata mtoto wao waliyezaa akawa anampiga sana ukatili kwa watoto.

2)KITUKO kimoja akamlazimisha wamfungie mtoto ndani wamuache peke yake halafu waende NIGHT CLUB kucheza mziki na kunywa pombe ,dada lucy kakataa akapigwa sana karibu amuue..mpaka majirani wakaingilia kati LUCY akatoroka usiku huo huo akaja nyumbani..

Lucy akawa anafanya mchezo akipigwa huko anatoroka anakuja nyumbani akikaa nyumbani kidogo anatoroka nyumbani tena anarudi kwa huyo jamaa.

jamaa akampokonya dada lucy simu akamzuia kuwasiliana na nyumbani wala mtu yeyote hata wazazi wake ,kwa muda wa miaka 2 ikabidi mama afunge safari kumfuata moshi akamkuta ,akamweka ndani lakini cha ajabu dada lucy akawa upande wa mume wake ana mtetea.(huko nyuma mama wa huyo jamaa na jamaa walishawahi kumpeleka dada lucy kwa mganga wa kienyeji sijui walichofanya)

3)Kingine ambacho mke wangu aliniambia ni kwamba hilo jamaa likawa linamlazimisha kumuingilia kinyume na maumbile dada lucy akikataa anapigwa kipigo cha mbwa koko..anatoroka anakimbilia nyumbani akirudi nyumbani anakaa kidogo ..mpaka wife akampeleka chuo cha ufundi wa mambo ya wanawake ..kasoma kidogo katoroka tena bila kuaga karudi tena kwa lijamaa.

Mpaka sasa dada lucy amesha achana na lijamaa ,kachukua watoto wake wawili na yeye kawarundika nyumbani wanalelewa na mama.

Sasa hivi dada lucy anapambana na biashara nimempa mtaji naona anajitahidi.Sasa hivi akili zimetulia nilimpeleka kwenye maombi na yeye kwa mchungaji laizer akaombewa ...
 
Dada ziyola huyu tumechangia baba mama tofauti,
Naye mumewe alimdanganya aache kazi,akamwambia hiyo kazi yako ya usekretari unayolipwa mshahara laki 3 kwa mwezi acha maana mimi nina hoteli hapa hotelini kwa siku unapata faida zaidi ya hiyo laki 3.
dada alipokuwa ana delay kuacha kazi ,akirudi kazini anampiga sana ,anamnyoa nywele na kuchana chana nguo za dada ,antuhumu huko kazini hana imani kwanini eti dada anaenda kazini amependeza eti wivu wa mapenzi eti hana imani na wanaume wa kazini ofisini.
Dada ikabidi aache kazi.
Dada alipo acha kazi tu akaanza kunyanyasa ,anamtukana matusi mbele ya wateja wa hoteli anampiga anamdhalilisha.
Ila dada alishauriwa asiache kazi hii hata mimi nilimshauri.
Kuna siku kafukuzwa kapigwa akakimbilia kwa wifi yake ,wifi yake akamshauri ulifunga ndoa ya kanisani,kazi amekusababishia uache kazi ,rudi komaa vumilia ,ilinusipoteze haki zako,za mali mlizichuma pamoja.
Hivyo sista anakaa kwa sababu ya mali huku ananyanyasika na kudharauliwa na kuaibishwa.
 
Olewa wewe
 
Huenda sister wako anafurahia vile jamaa "anaendesha" gari muda mrefu baada ya nyagi.
 
haya mambo magumu sana hasa ukiona anayefanyiwa ni ndugu yako

lakini naona kuna wadau wanajibu kejeli tu
 
Kuna wanaume wanatumia advantage ya wanawake kutokua na maamuzi sahihi kuwaharibia future zao.

kuna aina za single mother ambao ni wahanga wa wanaume kama hawa

kuna mwanamke anarubuniwa kanisani na mwanaume muhuni aliyeokoka kwa kuzuga….kwa kutokua na uwezo wa kuamua kwa usahihi anakamata mimba bahati mbaya au makusudi akiongozwa na imani….anapata mimba na kwa uoga wa kuishi kwenye maadili anaogopa kutoa mimba,anaishia kuishi katikati ya majuto ya kujua na kutojua anataka nini na ndio keshakua single mother.

ndio huyu sister wangu….anaamini sana watu na anaingia kichwa kichwa sana….mii baharia nikishauri naonekana ni wivu na siyajua mapenzi.

binafsi siyo mzuri wa kuongea nikaeleweka kwa mtu ambaye anashindwa kusoma ubongo na kupata yeye ninachomaanisha.Sababu huwa siwezi kutumia maneno mengi sana zaidi ya kuamua hasa kwenye mambo yanayonihusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…