Dada yangu anakaribia kuolewa na Tapeli, Nichukue hatua gani?

Mkuu unamfukuza tu ila inategemea na tamaduni zenu zinasemaje kuna jamii nyingine zinaishi kwa mfumo dume sasa kama wewe jamii yako siyo ya mfumo dume ndiyo maana umeshindwa kumfukuza ila naamin ungekuwa unatokea kwenye jamii ya mfumo dume ata huyo shemeji yako having weza kukaa kwenu na Vijana wakiume mngemfata na kimtimua Wazazi wenu wangefurahi na kuwa pamoja na nyiny na wangejisifu wana vijana wakiume wamezaa. Mimi nyumbani kuna Dada yangu amezalishwa nje ya ndoa na mtoto akamleta nyumbani sasa sisi vijana wa kiume tunaishi mbali na Nyumbani sasa kumbe mzee kila siku ana mwambia Mama huyu mtoto aende kwao sitaki kumuona hapa lakini cha kushangaza watoto wetu hawafukuzi kwasababu ni kwao.
 
Kwani anatapeli mbunye?
Acha unaa wewe. Eboo!
 
Usikute Tapeli kunako uwanja wa fundi seremala anasimamia kucha! hata ukimsanua dada yatakuwa yanaingia huku na kutokea huku na si ajabu tapeli akawa anafikishiwa Taarifa.
 
Mkuu hiyo chai.. Mbichi. Kwa sasa Tusker lager haipo Tanzania. Mimi nilikuwa mnywaji mkubwa wa hiyo beer kwa faida yako tu niliwahi kwenda hadi SBL kuhoji hapo kabla ilikuwa TBL. Nazungumzia miaka mitano nyuma. Wewe leo hii umeipata wapi?!!!
mkuu,mambo mengine mengi kadhaa hayapo kama unavyoyasoma…hata hiki unachokisoma sasa hivi hapa,kwahiyo usikaze sana fuvu.
 
Noma sana!
 
ningemfukuza kwenye nyumba ya baba aliyonunua akampatia akae halafu mimi nikamfukuze wakati baba mwenyewe aliyenunua nyumba yupo hai,na mama mwenyewe anayempa jack hela za kwenda kuhongea yupo.
Niliona italeta chuki na uadui dada yangu atanichukia na kuniona mimi mbaya .
Hata sasa nyumba imeshakuwa ya dada jack rasmi baba amempa yake,na bado huyo jamaa yuko naye na status anamposti anamuita my hero mara my number 1...japo hakai pale ndani toka amefukuzwa, ila leo na kesho unawakuta pamoja utaonekana mbaya .
 
Naunga mkono hoja.
 
Dada yako akija kuharibikiwa huko utakuwa mzigo wenu. Mwambie kiutu uzima ila umuache afanye maamuzi mwenyewe. Video muonyeshe ila usimtumie. Siku yakimkuta ya kumkuta asije sena j
Hukumwambia
 
umeandika visa vyako vyote vitatu kwa uchungu sana, na inaonekana wewe ni mtu mwenye hekima sana

kwakua wazazi wako hai na wao ndiyo wanashiriki kwenye upotevu wa watoto wao isipokua huyo wa mwisho aliyeachishwa kazi, basi siku wakitangulia mbele ya haki, huo mzigo utakua wako na kaka zako
 
mwambie ukweli ila mwachie maamuzi afanye mwenyewe,huyo ni dada`ko akipatwa na janga kwenye hiyo `ndoa utalia naye,maana kila mchuma janga hulia na wa kwao
 
Hapo kuzuia dada yako asiolewe na Tapeli olewa wewe na jamaa kisha baada ya mwaka omba talaka.
 
Hili linawakuta wanawake wengi. Na mimi nina kisa cha dadanhu ila sitakishare.
Na wakiwa katika mikono ya tapeli ni kama wamepofuka hawaoni kabisa hata mambo yaliyo wazi.
 
Unajua dada yako aliumiza wanaume wangapi waliokuwa serious lakini akawatapeli na wengine wakaumia isivyo kawaida.Mwache aolewe na yoyote hata awe tapeli wa kiwango gani.Malipo ni hapa hapa duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…