themagnificient
JF-Expert Member
- Dec 13, 2016
- 1,033
- 3,720
Dada yangu 49 years now ameajiriwa kwenye Hospitali Binafsi kubwa sana hapa Dar, ana kijana wake wa kiume ambae ndio alitegemea aje hata aonyeshe njia maana watoto wake wengine ni tia maji wote wanamsumbua huyu ndio alijua atakuja kumfuta machozi, Cha kwaza kijana wakati yupo form six tu walifukuzwa shule yeye na wenzake 4 sababu ya kuanzisha makundi ya kidini yenye misimamo isiyoeleweka na kufanya vurugu, ikabidi Dada amtafutie shule nyingine private kwa gharama kubwa kumnusuru.
Dogo akamaliza Advance akaaply Chuo cha udaktari Tanga huko, hali ilivyokuwa ngmu maana Baba yake hakuwa na msaada wowote Dada akakopa sh milioni 5 pale kazini kwake kwa ajili ya kumsomesha tena hiyo milioni 5 iliisha, ikabidi awe anapambana kuongezea hela sehemu nyingine, Dogo akapiga kitabu akamaliza kwa tabu sana.
Mwaka 2020 Dada kwa sababu ni Mkongwe pale kwenye Hospitali anayofanya kazi akafanya juu chini kumuombea nafasi na moja kwa moja Dogo akapata nafasi ya kuajiriwa kama Daktari
Balaa likaanza Dogo baada ya kuajiriwa tu akawa anakuja kazini Amevaa Nusukanzu, Kobazi na Kibarakashia huku Anafuga Ndevu kama Osama, hadi akawa anatisha waajiri wake ikabidi Sister aitwe haraka sana akaambiwa kuwa Huyu kama ni mwanao basi kaa nae umkanye mara moja kuwa Yale hayakuwa mavazi sahihi kwa mfanyakazi akashauriwa kuwa avae mavazi official ambayo yapo kwenye muongozo kwa mujibu wa kazi.
Sister na sisi wajomba zake ikabidi tumuite Dogo tumkanye kuwa Uongozi wa pale wamemkanya ajirekebishe ile ni Hospitali kubwa na ni lazima afuate miongozo, Dogo akawa mbishi na alipoona anazongwa sana kwa lile swala akaacha kazi kabisa kwa Hasira akaenda mikoani huko akawa anajihusisha na mambo ya kidini.
Kuanzia kipindi hicho Dada yangu ni presha za kupanda tu na kushuka, Juzi kati hapa hadi akazimia maana kijana alikengeuka akawa hamuheshimu na hana maisha ya kueleweka tena na ukiangalia amechoma zaidi ya milioni 7 kumsomesha na hadi leo hii hana kiwanja wala nyumba, amepanga.
=====================
=====================
NINEONA BAADHI YA WATU WAKIMLAUMU SISTER KUWA JUKUMU LA KULEA MTOTO NI LAKE HIVYO HAKUTAKIWA KULALAMIKA KUWA DOGO HAMSAIDII
JAMANI NIWAAMBIE TU MTU MWENYE JUKUMU LA KUSOMESHA NA KULEA KWA ASILIMIA KUBWA NI BABA LABDA AWE AMEFARIKI, NA DOGO BABA YAKE ALISHAKIMBIA MAJUKUMU HIVYO ALITAKIWA AJUE MAMA YAKE AMEENDA KUKOPA KARIBIA MILIONI 8 KUREPLACE JUKUMU LA BABA YAKE HIVYO ALITAKIWA DOGO ANAPOMALIZA SHULE AANGALIE KUWA MAMA YAKE HAKUWA NA HZO PESA NA ALIJITOA MUHANGA KUREPLACE NAFASI YA BABA YAKE ILI ASOME SO DOGO ALIPOMALIZA ILIKUWA NI MUHIM KUSAIDIANA NA MAMA YAKE MNAOSEMA KUWA DADA ASILALAMIKE NGOJENI YAWAKUTE