Dada yangu anapitia mateso makali sana sababu ya kijana wake kushika Dini hadi imemfanya amekuwa mjinga

Sasa huzuni ni kuwa mdogo wake hana kazi au ni hela aliyoipoteza kusomesha? Kifupi pesa ukishaitumia hovyo, kama ulihonga, ulinywea pombe, uliibiwa, uliingiza mahali sio sahihi hutakiwi kuiwaza, wewe fikiria jinsi ya kupata nyingine na uendelee kuitafuta,kwakuwa ile haitarudi tena hata kama utapiga kelele.....
 
Sijui kwanini mababa huwa wanadharaulika. Mzee wa watu alishamuona dogo na uchizi wake akaamua kumpotezea mkamuona fala mzee wa watu mkaenda kukopa kumsomesha dogo. Ukute mkatoa na kashfa kibao kwa mshua. Haya sasa mkakope tena mumtibie dogo afya ya akili.
 
ISHU NI MAISHA YA SISTER AMEPITIA LIFE GUMU SANA KUAZIA KWA WANAUME ALIOZAA NAO WOTE WALIKIMBIA MAJUKUMU AKAWA ANAELEA KIVYAKE NA UKIANGALIA PESA KARIBIA ZOTE ZA MSHAHARA WAKE AMETESEKA KULEA VIJANA WAKE HADI LEO AMESHINDWA HATA KUJENGA MWISHO WA SIKU HAO ALIOTEGEMEA KESHO WAMSAIDIE NDIO WAMEKENGEUKA
 
Anapaswa, kulipa kwanza MAHANGAIKO ya mzazi wake HAYA yanayoonekana. Kisha atafute UNABII wake. Mzazi anaugua kwa MADENI, mzazi ANAUGUA kwa mahangaiko ya mwanae.

Ni bora ampumzishe HANGAIKO MOJA.
 
Hayo ni mapito tu yataisha muombeeni kwa Mungu. Hayo mambo ya msimamo mkali ni mapepo tu.


kila mzazi huwa anajitoa ili mtoto baadae aje kumuangalia hata akikwama huwezi ukapata maisha usisaidie wazazi wako

Mtihani wallah
Kuna yule mama twaiba wa kariakoo yamemkuta kama hayo mtoto wake alienda chuo Southafrica amepotelea huko huko
Amelia mpaka na kumtafuta mpaka basi

Dini ni ugonjwa mbaya sana wa akili kuwahi kutoke duniani.

Angemfungulia msikiti au madrasa tu.
Mimi mwanangu nikiwa simuelewi namfungulia kanisa awe kama yule mchungaji wa kenya McKenzie

Hakika maana hapo kwa maelezo hayo huyo yupo tayari kwa lolote

 
Kipindi niko advance miaka ya 2000 hili vuguvugu la udini lilianza ghafla. Shule ya Serikali, kuna baadhi ya maustaadh wakakusanyana wakaanza kama kujitenga. I remember tulikua tunawaita alshakaki.

Jamaa walikuwa serious kwelikweli na dini, mixa wakikukuta mnyonge wanawataitisha madogo balaa, naskia kuna ambao walikua wanapelekwa kwenye mskiti wao na kuwalamba viboko kwa mfano wakikuta wamevaa zile suruali fupi n.k.

Jamaa ambao nilikuwa nasoma nao class moja baadhi wakaamua kujiunga huko, ghafla wakaacha kuingia class except kipindi cha BAM na GS. Maoni yao ni kwamba hawakubali kusoma Elimu dunia. Ni kafir!
In short tulikuja kumaliza bila wao kufanya mitihani kasoro hiyo mitihani miwili tu.

Naskia wamebaki huko kwa wambuli, wamejichukulia mabinti wa kimbulu wameoa wanadeal na miskiti tu.
Huwa najiuliza kuhusu mmoja wao aliekuwa anatokea Bukoba huko, safari ilivyo ndefu na wazazi walivyowekeza halafu ameishia kijijini hana ramani.

Sema nini, life ni kuchagua..
 
Aisee
 
Huyo dada yako ndio mwenye matatizo, anamfuatia mnoo mtoto wake ambaye kwa sasa ni mtu mzima.
Kijana ameamua kushika dini yake hiyo imekuwa nongwa, vipi angekuwa teja, mlevi au shoga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…