Dada yangu anapitia mateso makali sana sababu ya kijana wake kushika Dini hadi imemfanya amekuwa mjinga

Kwa ufupi ni kwamba uyo jamaa hana dini na ajiandae kwenda kuchomwa kwenye moto Mkali wa jahanamu kama asipobadilika.. uislamu ni vitendo siyo maneno kwa mujibu wa Quran tukufu na sunnah za mtume Muhammad s.a.w uyo jamaa hana dini anapoteza muda bure tu uko kwenye darsa
 
Hv Kuna mtoto wa mkubwa yoyote,ambaye ni shekh,mchungaji?
Watoto wa mwinyi,karume,kikwete,Kuna ambaye ansvaa don't touch na makubazi akishinda akitembea kusambaza dini?,kwa Nini kama ni jambo la maana sana Hawa viongozi hawana hata mtoto anayefsnya hivyo,?
Watoto wao ni marubani Qatar,madokta bingwa,wafanyabiashara wakubwa!
Hakuna anayefsnya upuuzi wa dini?
 
Najiuliza huyu dogo kaacha kazi sababu ya kuzuiwa kuvaa kanzu, mfano angepata kazi jeshini au kwenye migodi angechimbq na kanzu?
 
Amenasihiwa sana lkn naona hawa ni mtihani kwa kweli, haelewi yeye ni kushinda kutwa msikitin, hata huo wajibu wa kujua darja la mzazi wake haelewi hata kidogo
 
Mwanaume kidogo uwe na KIFUA kuna mambo yalitakiwa ubaki nayo ili umsitiri ndugu yako sio kila kitu cha kuongea tu.
 
Afukuzwe kazi, ni bora sheria itungwe mzazi kupata 50% ya pesa alizotumia kumsomeshea mwanae kuanzia alipokuwa form one hadi chuo kwakuwa dogo alikuwa akijitambua
 
Huo msimamo wa kidini na kiburi na madharau Kwa mzazi wake anadhani Mwenyezi Mungu anapenda? Au ndio anajidanganya kuiona mbingu kwa namna Ile? Huyo dogo anapuyanga.
 
Apo alipoteza ela tu inaonekana dogo udaktari sio passion yake adi akavukuzwa shule pale ingetosha ajue passion yake ni ipi matokeo yake amepoteza ela eti kisa mtoto awe kama yeye
 
Najiuliza huyu dogo kaacha kazi sababu ya kuzuiwa kuvaa kanzu, mfano angepata kazi jeshini au kwenye migodi angechimbq na kanzu?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
samaleko..!
Kinachokuuma wewe ni hiyo mikopo
Mwacheni dogo ameamua kufuata njia ya mnyenziiMungu..
 
Ni aibu kuyaanzishia mada maisha ya mwanadamu mwenzio aliyechagua njia yake bila kuvunja sheria ya nchi.

Nikuulize wewe mleta mada, mama yake kijana amekupa ruhusa kuja mitandaoni kushare family matters zake?.

Unajua upande wa pili wa shilingi wa kwa nini huyo kijana kaondoka bila kufukuzwa kazi?

Fuata maisha yako, kusoma kasoma yeye na ndevu zake, halafu unataka baada ya hapo ndevu azinyoe yeye.

Dogo atatoboa tu kwa kufanya anachokipenda usimpangie.

So far mpaka sasa hakuna disciplinary procedure yoyote ambayo dogo ameipata kazini, zaidi ya kupigwa majungu tu!

Wewe kwa akili zako unadhani angekuwa ni daktari wa kike sister wa kanisa katoliki anavaa mavazi yake kazini wangemfukuza kazi?- Nimeshakutana na masister wanafanya kazi ktk taasisi zisizo za kanisa na wanavaa mavazi yao, mbona hawafukuzwi kazi?.

Hoja hapa ni Islamophobia tu hakuna jingine.
 
Naam akhiy, jazaakallahu khayran
 
Poleni aisee, si suala la kucheka. Shule za boarding hizi na vyuo hasa vya diploma vinaweza kukuletea mtoto ukajiuliza huyu ni wangu kweli? Heri huko uni hawana muda sana wa mambo ya kijamii.
 
Kijana yupo sahihi maana kusoma na kuwa daktari na kuendelea kumjua Mungu sio Jambo jepesi

Wengine tumeshuhudia watu hawajui Mungu wafiraji na Mashoga na wengine wanauza uchi sawa na bure so huyo kijana yupo sahihi Sana kumjua Allah na kufanya ibada

Kuhusu dada yako kulalamika Sana ,kabla hujaamuua kuzaa unabidi kujipanga kulea na kusomesha mtoto wako


Kama dada yako anazimia kisa mil 8-9 Mwambie aweke namba yake tumchangie kulpa Deni lake
 
Kuna best yangu aliacha kupasua mende mtihani wa taifa form 6 biology, kisa alikuwa radicalized huko msikitini kwao, tulikuwa tunasoma wote baadae akahamia huko mazima, nilikuwa namwona na container lake anakuja kuchukua msosi au kama kuna mwalimu class anatokea, alikuwa amepauka ngozi sijui kwanini. It was so sad, na akazungusha yai matokeo ya from 6, wakati alikuja na division 1 ya point 8 sijui.
 
Huyo alishalinganiwa yakamwingia siyo muda mrefu mtamsikia ametoweka kuelekea kusikojulikana kujiunga na makundi ya kigaidi duniani. Ukiona dini inakufanya badala ya kuwa mnyenyekevu kwa wazazi ndugu na jamii unakuwa jeuri ujue ndani yako hakuna Allah.
 
Wa wapi wewe? Majukumu ya kusomesha ni ya mzazi sio ya baba au mama,harafu acheni kusomesha watoto kwa lengo la watoto kuja kuwapeni misaada,M 7 kitu gani,harafu waandika kwa herufi kubwa unatufokea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…